Hivi mtu anayeitwa Uchebe ni Msanii wa Sanaa gani?

kyanyangwe

JF-Expert Member
Oct 31, 2018
1,147
2,746
Last weekend nikiwa na washkaji zangu kiwanja flani hapa mjini,ghafla akatokea mtu mmoja kwenye meza yetu akajitambulisha kuwa yeye anaitwa Uchebe akawa anatuomba tumnunulie bia, tukamuuliza yeye ni nani akatushangaa tu imekuaje sisi hatumjui yeye na wakati ni mtu maarufu sana hapa Tanzania then akaondoka zake.

Sie tukaamua kugoogle ili kuona jamaa kama ni msanii wa Sanaa yoyote hapa Tanzania lakini hatukubahatika kuona kazi yake yoyote ya Sanaa.

So nikaona nije kuwauliza wakuu,huyu the so called Uchebe ni msanii wa Sanaa gani hapa Tanzania.

Capture%2B%252848%2529.PNG
 
Nimecheka sana... mambo matatu

1.eti kaomba bia mkamnyima (naimagine vyenye anaomba bia)

2. akawashangaa kwanini msimjue (naassume namna anavyowashangaa mpaka kufika anaondoka kwa fedheha na aibu)

3 mkaanza kuulizana yeye ni nani msimjue hasa mpaka mkagoogle lakini wapi!

JF sihami
 
Back
Top Bottom