Hivi mtu akipata degree za vyuo vikuu hawezi kazi nyingine mpaka aajiriwe? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi mtu akipata degree za vyuo vikuu hawezi kazi nyingine mpaka aajiriwe?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by mkulungwa, Feb 23, 2011.

 1. m

  mkulungwa Member

  #1
  Feb 23, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hali zenu wanajamii!!!

  Mwenzenu nina mdogo wangu kamaliza Chuo kikuu cha Dar Es Salaam mambo ya biashara. Miaka mitatu sasa anatembea kutafuta kazi hajapata hata kama ana first class. Nimemfungulia biashara pale kariakoo kusimamia mzigo toka china na kusambaza kwa wateja .. but kashindwa!! nashindwa nimfanyeje yaani mvivu na sopsop tu hataki vumbi.

  wadau nisaidieni mwenzenu, hivi ndivyo degree zote zinavyokuwa or ? kwanini iwe hivyo? faida ya degree sasa nini hasa first class?

  Mkulungwa
   
 2. Landala

  Landala JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 940
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Huyu inabidi umkalishe chini umfahamishe kazi sio lazima aajiriwe,nchi yetu watu wengi wanatoka kwa kujiajiri na pia tatizo la ajira hapa nchini ni kubwa inabidi akubaliane na huo mradi uliomfungulia kwani unaweza kumtoa.
   
 3. Landala

  Landala JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 940
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Huyu inabidi umkalishe chini umfahamishe kazi sio lazima aajiriwe,nchi yetu watu wengi wanatoka kwa kujiajiri na pia tatizo la ajira hapa nchini ni kubwa inabidi akubaliane na huo mradi uliomfungulia kwani unaweza kumtoa kimaisha.
   
 4. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #4
  Mar 12, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  wanaambiwa tangu wadogo "soma kwa bidii uje uwe mbunge au waziri"
   
 5. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #5
  Mar 12, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Sifikirii kama huyo mdogo wako alipata 1st class kama unavyotaka tuamini hapa. Kama kweli angekuwa na hiyo first class wala usingemsikia kwa sababu kusoma kunakupanua mawazo na kukujenga ufanye nini katika maisha yao.
   
 6. K

  Kakulwa Senior Member

  #6
  Mar 13, 2011
  Joined: Oct 10, 2008
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  elimu zenu za kukariri hizo..eti nikimaliza niwe afisa wa benki,meneja,mkurugenzi,nyumba gari ndani ya mwaka..ndiyo matokeo yake hayo
   
 7. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #7
  Mar 13, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,610
  Likes Received: 3,911
  Trophy Points: 280
  Wote mliochangia hii maada hapo juu asanteni sana hili swali ni very serious na nimefurahia michango yenu, hili ni janga na huyo dogo hayuko peke yake, Nganang'wa ameanza kueleza chimbuko lake , we need to discuss this deeply.
   
 8. m

  mzambia JF-Expert Member

  #8
  Mar 13, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Lkn first class hata u t.a pale chuo kakosa maana ajira ya haraka bongo ni ualimu tu hakuna nyingine ya haraka.

  Afu ndo hvo kwamba kila mtu anataka awe david silinde(mb mbozi)
   
 9. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #9
  Mar 13, 2011
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  <br />
  <br />

  Anaitwa chuma ulete huo! Nenda kwa ben mwaitege ufanyiwe mamobi uachane na kina chuma ulete!

  Teach one how to fish, don't give one fish every day!!!

  Mlikuwa mnapa samaki kila cku kakua bado mwendele kumpa unalalamika nn?
   
 10. Kiherehere

  Kiherehere JF-Expert Member

  #10
  Mar 14, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,804
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Nakugongea thanks kaka wewe ndo umenena
   
 11. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #11
  Mar 15, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Ukiona hivyo ujue ni wale wa madesa hao. Watu tunatafuta mitaji ya kujiajiri tunakosa wakati kuna mtu anachezea shilingi chooni? Ukiona hivyo ujue kuwa alikuwa na matarajio makubwa sana ya kukaa ndani ya mojawapo ya majengo mazuri hapa mjini. Full kipupwe na gari yake hapo kwa park. Tatizo lake ni kutokubali matokeo na kukataa kujipanga upya. Nenda nae slowly tu mtafika
   
 12. Loly

  Loly JF-Expert Member

  #12
  Mar 15, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 485
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  Nikwambie kitu Mkulungwa siku zote kwenye haya maisha kuna maskini, maisha ya kati na matajiri haijalishi umesoma au hujasoma sasa basi ukiona mtu anapenda saaana kuajiriwa jua natural huyo maskini na siku akipata hiyo ajira maisha yake ni kati tuu hivyo usimlaumu sana mwambie akuangalie wewe na maisha yako then ajifunze.

  <p>
  </p>
  <p>&nbsp;</p>
   
 13. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #13
  Mar 15, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,242
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Kosa siyo lake,Mfumo wetu wa elimu ndo chanzo cha hili janga.
  Tunasoma sana ili kupata Vyeti/Digiriiiii,na matokeo ya hizo digiriiiiiiiiii ni kuishia kuajiriwa,kwani mfumo hautupi nafasi ya kuwa self confidence kufanya kitu inje ya uliyoyasoma.
   
 14. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #14
  Mar 21, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo na siongelei tu uvivu wa huyu kijana.

  Fikiri. Mtoto unakua wazazi wana kuambiaje? Soma upate kazi nzuri. Walimu darasani wana kuambia soma ili? Upate kazi nzuri. Tokea utotoni tuna kuwa encouraged kuja kuwa watafuta ajira na si watengeneza ajira na ndiyo maana ukiangalia Tanzania wengi wa wafanyabiashara wakubwa si wasomi wakubwa kwani wange soma sana na wao wange kuwa watu wa kutafuta ajira tu.

  Ila hili tatizo si la Tanzania tu. SOmeni kitabu kinaitwa Rich Dad, Poor Dad mtajua hata Marekani wana tatizo hili. Hatufubdishwi creativity wala independence. Tusha lishwa ile tabia ya mtu kutaka kuja kuwa dokta, engineer au lawyer. Mazoea ni kama sheria.

  Kwa hyo kila kitu ni mindset tu mkuu. Watanzania wengi tuna mindset ya kiutegemezi na huo ndiyo ukweli.
   
 15. Smarter

  Smarter JF-Expert Member

  #15
  Apr 5, 2011
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 455
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mimi nahisi kijana anamatatizo mengine zaidi yaliyojificha. Kwasababu graduates wengi sana wanaanza/wanafanya kazi tofauti na professionals zao. Vijana wa UD Bcom wengi tu wako mitaani wanafanya biashara KKoo.

  Tatizo hapo sio degree, ni studies za maisha na Malezi yanayopelekea mitazamo fulani fulani.........Kama anachembe chembe za Ushorabaro...Anaona noma kuonekana KKoo wakati wenzie wanafanya kazi kule anakofikiri ndio kuna ajira ( BOT, TRA, TPDC, EWURA) wakati kkimsingi angefanya hilo la KKoo angeweza kupaata Pesa zaidi.....MAOMBI YANAHITAJIKA......Ukimuacha aone Maisha with its true colors atatafuta vizuri hiyo ya KKoo, bt kama hana upeo ndio utampoteza kabisaaa
   
 16. BABA JUNJO

  BABA JUNJO JF-Expert Member

  #16
  Apr 9, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Huyo anamatatizo ya ufahamu na anahitaji msaada. Mimi nia masters nimeajiriwa niko kazini mwak wa saba sasa natafuta kwa bidii sana oppoturnity ya kujiajiri siipati sipendi mno kuajiriwa nashangaa mtu mwenye kadigrii kamoja hapendi kujiajiri ana pnda kuajiriwa/ Wonderful!!!!
   
 17. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #17
  Apr 9, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  Hakuna 1st class hapo, biashara udsm? Kama ni hivyo aje udbs kufundisha
   
Loading...