Hivi mtu akifa na hela zake ziko benki na Mpesa, tukiwa na cheti cha kifo tunaweza fuatilia?

Fuateni taratibu zote za kuteua msimamizi wa mirathi. Ikiwemo pia kwenda mahakamani.

Mahakama ikishatoa nyaraka za kumteua msimamizi wa mirathi, huyo ndiye atakayefuatilia kwa bank na kampuni ya simu ili kupata pesa.

Kumbuka kuwa jukumu la msimamizi wa mirathi ni kutambua na kukusanya mali na madeni yote ya marehemu. Jukumu la pili ni kugawa mali kwa warithi halali kisheria.

Hivyo, Msimamizi wa mirathi atakayeteuliwa ndiye atakayefuatilia na kupewa hizo pesa. Naye atazigawa kwa warithi halali kwa mujibu wa sheria.

Kwa suala lako, ingependeza huyo mke ndio apewe usimamizi wa mirathi.
 
Fuateni taratibu zote za kuteua msimamizi wa mirathi. Ikiwemo pia kwenda mahakamani .

Sheria ya mirathi kwa upande wa wajane kina mama inatakiwa kuangaliwa upya
 
Hio dealth certificate huwa hawaipokei bank wala mpesa, wanapokea death certificate tu. Sijui hata kwanini!

Warudishie RITA hio dealth certificate, halafu waambie wakupe death certificate. Halafu nenda mahakama ya mwanzo fungua shauri la kuomba kufungua mirathi ya huyo marehemu, mahakama watawapa barua ya usimamizi wa mirathi ndio mwende bank au huko mpesa mkazitoe hela, kama kuna nyumba au kiwanja kaacha mtauza. NA KAMA MAREHEMU AMEACHA MADENI, MTALIPA!

Usipo fanya hivo, jiandae na kesi ya uhujumu uchumi kwa kujipatia pesa kutumia njia ya udanganyifu (Hata kama hela ni Sh 2,000/=, uhujumu uchumi haina dhamana).
 
Upya kwa sababu gani? Ina mapungufu gani?
FRESHMAN wewe kama mwanaume umetafuta mali na mke wako kipenzi lakini ukitangulia kuondoka hizo mali zinauzwa warithi wanagawana. Sasa kama una nyumba moja wakishagawana yeye utu uzima ushawadia, kukimbizana hawezi tena, unafikiri yeye ataenda wapi.

Nawaza nimpoteze babachanja wangu halafu nyumba yangu nilivyoisotea Mimi na yeye iuzwe ili warithi wapate chao halafu Mimi nikaanze kutafuta makazi.

Maumivu juu ya maumivu
 
Hio dealth certificate huwa hawaipokei bank wala mpesa, wanapokea death certificate tu (Ikiambatana na barua ya usimamizi wa mirathi ya marehemu).

Warudishie RITA hio dealth certificate, halafu waambie wakupe death certificate.
Sijakuelewa hapo mzee umesema kwamba awarudishie RITA death certificate then wampe death certificate tena hapo hujaeleweka vizuri labda missspells
 
Mimi nilishaufanya mchakato huo nikiwa msimamiz wa mirathi. Death Certificate ni ka document kamoja tu, unapoenda huko M pesa au Bank kufatilia pesa unapaswa uwe na Document ya Kikao cha Familia kilichokuteua kuwa msimamiz wa mirathi, Uwe na nakala Za hukumu ya Mahakaman nk.

Hapo kama kaacha Mke inabidi ndio afatilie. Wewe kama aliyefariki ni kaka yako tambua kuwa huna sifa ya kuwa mrithi kabisa kisheria.Warithi halali hapo ni Mke na Watoto na Wazazi wa Marehem.
 
FRESHMAN wewe kama mwanaume umetafuta mali na mke wako kipenzi lakini ukitangulia kuondoka hizo mali zinauzwa warithi wanagawana. Sasa kama una nyumba moja wakishagawana yeye utu uzima ushawadia, kukimbizana hawezi tena, unafikiri yeye ataenda wapi

Nawaza nimpoteze babachanja wangu halafu nyumba yangu nilivyoisotea Mimi na yeye iuzwe ili warithi wapate chao halafu Mimi nikaanze kutafuta makazi
Maumivu juu ya maumivu
Sasa inauzwaje kama mama ndo kabaki kichwa cha familia atakaeuza ni nani? mana tayari mama yupo muuze ili iweje tatizo ndo linakujaga hapo kukosa busara kwa baadhi ya Wana ndugu shida Sana
 
Kuna mtu alifariki January mwaka jana taratibu zote zikafuatwa na msimamizi wa Marathi na pesa katika bank accounts zote zikapatikana lakini cha ajabu pamoja na kukamilisha kila kitu pesa bado hajapewa mkewe. Anaambiwa zipo hazina hajui tena afanye nini kishajichokea.
Fuateni taratibu zote za kuteua msimamizi wa mirathi. Ikiwemo pia kwenda mahakamani .

Mahakama ikishatoa nyaraka za kumteua msimamizi wa mirathi, huyo ndiye atakayefuatilia kwa bank na kampuni ya simu ili kupata pesa.

Kumbuka kuwa jukumu la msimamizi wa mirathi ni kutambua na kukusanya mali na madeni yote ya marehemu. Jukumu la pili ni kugawa mali kwa warithi halali kisheria.

Hivyo, Msimamizi wa mirathi atakayeteuliwa ndiye atakayefuatilia na kupewa hizo pesa. Naye atazigawa kwa warithi halali kwa mujibu wa sheria.

Kwa suala lako, ingependeza huyo mke ndio apewe usimamizi wa mirathi.
 
Huwa inakuwa kubwa Sana kama kuna watoto wa pande mbili tofauti na walikuwa hawapendani kingine kwamba na suala la elimu nalo tatizo kubwa Sana aisee ukikosa elimu sometimes huwa tatizo tena
Sheria hii ni mbovu
 
Kuna mtu alifariki January mwaka jana taratibu zote zikafuatwa na msimamizi wa Marathi na pesa katika bank accounts zote zikapatikana lakini cha ajabu pamoja na kukamilisha kila kitu pesa bado hajapewa mkewe. Anaambiwa zipo hazina hajui tena afanye nini kishajichokea.
Sina hakika hapo issue ni nini.

Ila ninadhani hii inatokana na kuwa siku hizi wakati mwingine unakuta kuna yale masuala ya pesa kutumwa bank kuu au akaunti ya mahakama.

Sasa kama baada ya uteuzi wa msimamizi wa mirathi, barua ya mahakama inasema pesa ziwekwe bank kuu au akaunti ya mahakama, basi taasisi husika inalazimika kulipa pesa huko. Sasa si unajua taratibu za serikali zinavyokuwa?

Ni jukumu la msimamizi wa mirathi kufuatilia. Ndio kazi yake hiyo.

Ila nina uhakika kuna baadhi ya kamoubi za simu zinalipa moja kwa moja kwa wasimamizi wa mirathi. Hili nimelishuhudia binafsi kwa ndugu zangu
 
Back
Top Bottom