Hivi mtoto wa kike kama haolewi anapaswa kuendelea kuishi na wazazi mpaka umri gani?

Hapana. Hajanituma nimtafutie mchumba. Mada hii ni ya mimi kungwi kutaka kujielimisha namna nzuri ya kutoa ushauri juu ya umri sahihi wa mtoto wa kike kuondoka nyumbani hata kama hajaolewa.
Hatakiwi kuondoka nyumba bila kuolewa, lakini inawezeka akaondoka kwasababu ya ajira mfano kapata kazi Serikali kapangiwa Mwanza na yeye kwao ni Tabora, au kazalishwa bila kuolewa ili la kuzalishwa bila kuolewa itategemea na tabia yake na mienendo yake.
 
Anatukanwa na majirani?? Au anahisi Tu?
Tanzania ya Leo kuna jirani wa kwenda kutukana mtoto wa mtu kisa hajaolewa?...muwe mnataja na vitongoji mnavyotoa hivi vituko twende tukatembee tuone vituko uswahilini
Majirani wenyewe watoto wao hawaja olewa wanaishi nao
 
Kwa mila na tamaduni zilizokuwa zimezoeleka huko nyuma ilikuwa kwamba mtoto wa kike ataondoka kwa wazazi wake kwa kuolewa.

Kwa miaka ya karibuni mifumo na taratibu za maisha zimegeuka kabisa. Idadi kubwa ya watoto wa kike hawaolewi kwasababu mbalimbali.

Kufuatia mabadiliko haya ndiyo sababu ninakuja kwenu wanaJF na maswali yangu haya:-

1. Kwakuwa kuolewa ni nadra sana siku hizi, je, mtoto wa kike azeekee kwa wazazi wake?

2. Kama jibu la swali la kwanza hapo juu ni HAPANA, je, ni umri upi sahihi wa mtoto wa kike (asiyeolewa) kuondoka kwa wazazi wake na kwenda kujitegemea?

Kwanini nimeleta uzi huu?

Kuna mdada mmoja kaja kuniomba ushauri mimi Sexless, kungwi la kitaifa.

Anasema ana miaka 32 (msomi wa chuko kikuu) hajabahatika kuolewa wala hajapata kazi. Bado yupo kwa wazazi lakini hivi sasa anatukanwa na majirani, makaka na mashangazi. Wazazi wake hawana shida naye kabisaaa, wako peace kabisa.

Tutoe ushauri utakaosaidia wadada wote nchini wenye changamoto kama ya huyu mteja wangu.
Huyo ni wewe usimsingizie dada wa watu ila si mbaya tangazo tumelielewa,njoo pm tuyajenge
 
Kimsingi masimanho yao yamejikita kwenye umri. Wanasema umri wote huo (miaka 32 ) bado unapishana na babako bafuni? Wanamuambia bora akapange chumba chake mtaani aondoke nyumbani
Binti hana kazi ya kumuingizia kipata halafu aende akajitegemee, Je akajitegemee kwa kujiuza ?
 
Kwahiyo mkuu kuhusu umri sahihi wa mtoto wa kike kuondoka kwao? Hujasema chochote
Mtoto wakike anaondoka kwao kwa kuolewa au kupata kazi mbali na kwao na uko alipo pata kazi kama kuna ndugu zake mfano Kaka, Dada, Mjomba, Shangazi, Baba zake atachagua pakwenda kuishi.
 
Je bikra anayo?
kama ana bikra ruksa kukaa kwa wazazi wake hata Miaka 100

maana zama hizi Kupata Mwanaume Kama hauna bikra ni ngumu Sana labda uende kuombewa kwa kuhani Mussa Mbezi
 
Kimsingi mwanamke ni kuchungwa nyakati zote za maisha yake.....mwanamke hana ukomo wa kukaa nyumbani........ wazazi Wana wajibu wa kumuhudumia mpaka atakapoolewa na kama Hana mume na wazee hawana uwezo basi kaka zao wanawajibika kumuhudumia dada yao mpaka apate mume
Mkuu apo kwa kaka inategemea na tabia ya Dada yao kama dada yao ana tabia njema atasaidiwa
 
Kanda ya ziwa kubwa mkuu. Mkoa gani specifically? Maana kwa mkoa wa Mara ndoa siyo ya watu 2.

Makubaliano ni ya watu 2 lkn ng'ombe (.mahari) zikishatolewa mke anakuwa wa ukoo. Atakatwa mpk mkono lkn haondoki.
Umeanza vizur lkn naona km una haribu ss.
Acha kutuchafua watu wa kutoka Mara. Mara kuna makabila mengi ebu kuwa specific ni watu gan wanafny ivo. Usipende kutumia generalization
 
Hatakiwi kuondoka nyumba bila kuolewa, lakini inawezeka akaondoka kwasababu ya ajira mfano kapata kazi Serikali kapangiwa Mwanza na yeye kwao ni Tabora,
Sababu au lengo la kufanya hivi ni nini kwa mtu anayeitafuta miaka 40?
 
Kwa mila na tamaduni zilizokuwa zimezoeleka huko nyuma ilikuwa kwamba mtoto wa kike ataondoka kwa wazazi wake kwa kuolewa.

Kwa miaka ya karibuni mifumo na taratibu za maisha zimegeuka kabisa. Idadi kubwa ya watoto wa kike hawaolewi kwasababu mbalimbali.

Kufuatia mabadiliko haya ndiyo sababu ninakuja kwenu wanaJF na maswali yangu haya:-

1. Kwakuwa kuolewa ni nadra sana siku hizi, je, mtoto wa kike azeekee kwa wazazi wake?

2. Kama jibu la swali la kwanza hapo juu ni HAPANA, je, ni umri upi sahihi wa mtoto wa kike (asiyeolewa) kuondoka kwa wazazi wake na kwenda kujitegemea?

Kwanini nimeleta uzi huu?

Kuna mdada mmoja kaja kuniomba ushauri mimi Sexless, kungwi la kitaifa.

Anasema ana miaka 32 (msomi wa chuko kikuu) hajabahatika kuolewa wala hajapata kazi. Bado yupo kwa wazazi lakini hivi sasa anatukanwa na majirani, makaka na mashangazi. Wazazi wake hawana shida naye kabisaaa, wako peace kabisa.

Tutoe ushauri utakaosaidia wadada wote nchini wenye changamoto kama ya huyu mteja wangu.
Je ana mtoto au hana? Je Kuna mtu anampakua ? Je ana nundu aka kichuguu? Je ameshawahi kupewa mafunzo ya unyago au ndo mpaka kitchen party? Je ameshajua jamaa kwanini jamaa wanamkimbiaga? Je anaomba hela au kulia milio ya hela ndani ya muda gani wa mahusiano?
 
Mkuu apo kwa kaka inategemea na tabia ya Dada yao kama dada yao ana tabia njema atasaidiwa
Kaka kumuhudumia dada yake sio msaada ni wajibu....kuhusu tabia njema pia ni wajibu wenu kumrekebisha na kumuweka sawa....ndio maana nyinyi mkawa wasimamizi wake...... mwanamke ni kiumbe dhaifu ambaye anapaswa kuchungwa.....na wachungi ni baba, mume au kaka.....

Ndio maana kwenye mirathi kaka anachukua ziada kwa ajili ya dada yake endapo atatoka kwa mumewe........
 
Kwa mila na tamaduni zilizokuwa zimezoeleka huko nyuma ilikuwa kwamba mtoto wa kike ataondoka kwa wazazi wake kwa kuolewa.

Kwa miaka ya karibuni mifumo na taratibu za maisha zimegeuka kabisa. Idadi kubwa ya watoto wa kike hawaolewi kwasababu mbalimbali.

Kufuatia mabadiliko haya ndiyo sababu ninakuja kwenu wanaJF na maswali yangu haya:-

1. Kwakuwa kuolewa ni nadra sana siku hizi, je, mtoto wa kike azeekee kwa wazazi wake?

2. Kama jibu la swali la kwanza hapo juu ni HAPANA, je, ni umri upi sahihi wa mtoto wa kike (asiyeolewa) kuondoka kwa wazazi wake na kwenda kujitegemea?

Kwanini nimeleta uzi huu?

Kuna mdada mmoja kaja kuniomba ushauri mimi Sexless, kungwi la kitaifa.

Anasema ana miaka 32 (msomi wa chuko kikuu) hajabahatika kuolewa wala hajapata kazi. Bado yupo kwa wazazi lakini hivi sasa anatukanwa na majirani, makaka na mashangazi. Wazazi wake hawana shida naye kabisaaa, wako peace kabisa.

Tutoe ushauri utakaosaidia wadada wote nchini wenye changamoto kama ya huyu mteja wangu.

Mimi nilianza kazi na 24 years japo ilikua late kidogo nikataka niondoke nyumbani ili nimpunguzie mama angu majukumu maana mimi ndo first born na nlikua na kiherehere kweli cha kum support bi mkubwa.

Siku hiyo tuko kwenye mizunguko yetu nikamwambia, Mama, mimi nataka nikapange nyumba maeneo ya nnakofanyia kazi au hata karibu na ofisi kama ni msasani au mikocheni maana huku ni mbali. Alichonijibu tena baada ya dakika kumi za ukimya,” sijawahi ona mtoto wa kike anaondoka nyumbani” akaendelea “ huwa haileti picha nzuri hata wakwe wakija kukuchumbia wakaskia umepanga nje huwa inaleta picha mbaya sana kwamba huko nje unatabia za tofauti na unavyoishi ukiwa nyumbani”

Nashukuru nilielewa maneno yake nilikaa nyumbani hadi nakuja kuolewa after some few years nilielewa maana wakwe walikua wanauliza anaishi na wazazi? Ndio. Basi kidogo wanapunguza hofu.

Ushauri wangu; USITOKE NYUMBANI, huko nje utapata vishawishi vingi sana. Labda utafute kazi mkoani that’s the only excuse ya wewe kusema unakaa kwako. Na usiwaskilize ndugu hao wana midomo siku zote. Ya kwao tu yanawaelemea. Na Kuhusu ndoa usijali utaipata tu. Ila kama wazazi waliokuzaa hawaoni shida usiwafurahishe wa nje. Na hata mchumba akija akijua unakaa nje mwenyewe hatokua na amani kwamba huleti wanaume wengine or that’s how they believe.

Kikubwa jishughulishe. Tafuta hata mtu akufundishe kutengeneza sabuni za miche uza, kushona au kufanya make up. Mzazi akuone productive.
 
Alichonijibu tena baada ya dakika kumi za ukimya,” sijawahi ona mtoto wa kike anaondoka nyumbani” akaendelea “ huwa haileti picha nzuri hata wakwe wakija kukuchumbia wakaskia umepanga nje huwa inaleta picha mbaya
Ushauri wa mamako hauna maana kwa zama hizi ambapo ndoa siyo Jambo la kutumainiwa ama kutegemewa na mtoto wa kike.

Yaani mtu anaitafuta 40 ashindwe kupambania maisha yake kwa kusubiria kitu asichokuwa na hakika nacho?
 
Back
Top Bottom