Hivi mtanzania anayeishi Marekani, Ujerumani au Uingereza anajua shida za masela wa Pandachigiza?

Hivi wafadhili wetu, kama world Bank, IMF, ujerumani, Marekani, USAID, SIDA, uingereza, n.k " WAnajua shida za masela wa Pandachigiza?"

Na bado ndio hao wanaotoa pesa kusaidia maji vijijini kule
Pandachigiza. Huku serikali ya ccm inaowajua ikiwatekeleza.

Kumbe mtoto wako anaweza kutunzwa vizuri sana na jirani yako pale mwenyewe ukimtekeleza bila kujua mimba iliingiaje.

 
Lkn ndugu umenena!?hebu itizame tarafa ya nindo nzima.tizama pia kata ya pandagichiza (kanyageni vizuri)kwa lugha ya kiswahili. Au kata ya isela magazi.au lyabukande.au lyamidati.hizi ni baadhi ya kata zilizopo ktk tarafa ya nindo.wananchi wake ni wakulima na wafugaji.lkn leo atokee mtu hapa houston marekani;awaamulishe wasukuma wafugaji wa LYABUJIJE AU WA ILAMBOLYABUSALU waandamane.kisa magufuli eti ni dikteta.!!!??
 
Kwani mtanzania anayeishi masaki anazijua? Mi mwenyewe hicho kijiji maskini ndo nimekisikia leo
 
Ni nani asiyejua kwamba hizo nchi ulizotaja ndio zinazoisaidia TZ kuanzia kula, kulala na matibabu!? Matangazo mengi kwa radio ni msaada wa watu wa marekani... Sasa kama wanatoa msaada wanashindwaje kujua hali zenu?tunakukaribisha tarehe 26-04-2018 jitokeze kupaza sauti dhidi ya ukandamizaji
 
Ni nani asiyejua kwamba hizo nchi ulizotaja ndio zinazoisaidia TZ kuanzia kula, kulala na matibabu!? Matangazo mengi kwa radio ni msaada wa watu wa marekani... Sasa kama wanatoa msaada wanashindwaje kujua hali zenu?tunakukaribisha tarehe 26-04-2018 jitokeze kupaza sauti dhidi ya ukandamizaji
leo ni tarehe 27-04-2018
 
Kuishi nje ya nchi hakufanyi nisiwe na uchungu na nchi yangu maana kabla ya yote ni mtanzania na nina ndugu na marafiki ambao bado wanapata shida: kwa mfano tu huko kijijini kwetu hamna maji (watu wanakunywa maji ya mtoni), huduma za afya ni lazima wasafiri si chini ya km 10( hii dispensery yenyewe ni ya kanisa, thanks to the catholic sisters) achilia mbali umeme, sasa naachaje kuwa na uchungu kama haya niliyoyapitia mimi bado ndugu zangu na wanakijii wanayapitia.

Na ukiwa na uchungu. Unaamini katika Process za kufikia waliko wenzetu. Umesoma historia wamefikaje. Tz mission town nyingi. Leo mnawekewa mazingira mnaanza maneno. Najiuliza hapa Ujerumani ni lini niliokota Hela ya bure sikumbuki. Kazi. Kazi. Na ujue mabepari bado wanatunyonya. Ukitaka Korosho wapange wao. Kesho wanasema Pamba yako. Hatununui. Nk. Freiheit ya kuwajibika ya Sisi kama Nchi ipo wapi.
 
Pandagichiza ni moja ya kata iliyopo shinyanga vijijini ambayo hata ukigoogle unaweza usiipate !
Hivi tukitumia frontal lobes za brain zetu ...mtu anayeishi los angels au edinburgh au philadelphia au munich anaweza kujua updates za changamoto zinazowakabili wasiojulikana wanaoishi kata ya Pandagichiza na vijiji vyake?

Hivi hawa matapeli na wachumia tumbo wanajua hata ni watoto wachanga wangapi hufariki huko [HASHTAG]#Pandagichiza[/HASHTAG]?

Hebu watanzania tuachage mizaha na tutumie wakati wetu vizuri ili tujikwamue na effects za kuwa nyuma ya wakati.

Tuachane na midomo ya kimbea ya watoto wa kishua ambao hawajawahi kung'atwa na mbu au kuathirika na maji yanayowasha ya mashamba ya mpunga.

Tujitahidi kuwa busy kujikwamua katika umasikini na tutumie elimu zetu kwa wale tuliobahatika kutoboa ili tuwasaidie walalahoi wanaoishi ibinzamata au lokisale.

Muheshimiwa Rais unalindwa na katiba katika kuwanyoosha vilivyo wanaotaka kutuondoa kwenye mada ya msingi ya kuhakikisha masikini wa kutupwa wanafanikiwa kimaisha baada ya miaka mingi ya kuteseka.

Mheshimiwa Rais una haki ya kikatiba ya kumfanyia lolote kwa yoyote bila kujali kelele za mafisadi wachache ambao wanataka kukwamisha zeal ya kuuletea umma masikini wa watanzania maendeleo.

TUACHE VICHEKESHO NA TUWE SERIOUS ...NA PIA TUTAMBUE NYAKATI ZIMEBADILIKA...TUPO KWENYE ERA YA BUSINESS UNUSUAL!

Tutake au tusitake ni lazima tunyookee njia moja tu... yaani njia nzuri na iliyokubaliwa na watanzania ....kwa gharama yoyote ile!!
Acha ushamba wako toka kolomije na chato, kwani shida za hao huko vijijini shinyanga zimetatuliwa na ununuzi ndege, kukomboa ndege, kujenga uwanja wa ndege chato kwa kuchukua Trillion 1.5 kienyeji Hazina ( BOT) ? Mtanzania wa Ulaya hajui shida ya wa vijijini shinyanga kivipi? Watanzania kote Duniani wanajua pesa zote za maendeleo wanakula kifisadi wasukuma wawili washamba toka kolomije na chato,miladi yote Nchini wana 10% zao humo ni mafisadi kuliko awamu zote tokea Nchi ipate Uhuru, vichekesho uache wewe kilaza kuwa serous dai Trillion 1.5 , mdai Mtukufu pesa za kivuko feki bilion 8 , mdai zile bilion 252 zilipotea wizara ya ujenzi kwa kuwalipa makandarasi hewa,’mdai Zile nyumba za serikali alizojinunulia kibao tena kienyeji akagawa kwa mdogo wake na hawala ambao hawakuwa watumishi Umma,kama ulikuwa hujui sasa kaa ujue mafisadi ni hao na kinara wa Ufisadi ni Mtukufu malaika toka chato.
 
VIVA JPM VIVA JPM VIVA JPM...hapa kazi tu
Hapa kazi tu ni kula Trillion.1.5 ? Kula bilion 8 za kivuko feki cha mwaka 1978? Kufuja bilion 252 wizara ya ujenzi kwa kuwalipa makandarasi hewa? Kununua ndege kwa bei kubwa mara dufu kwa cash ili wale 10%? Kukomboa ndege Canada kwa cash wakala 10% hizo ndizo kazi tu?
 
tulikuwa pamoja shule na huyo wa Pandachiziga lakini akaamua ku drop out, leo hii mimi I am a tad bit better off na nina ma stress yangu ya ku maintain middle class life standard, huyo wa Pandachiziga is not a special citizen, na yeye apambane na hali yake

isitoshe yeye tayari anapata special dispensation, LUKU yake bei tofauti, kodi halipi, shule anasomesha bure au za cheap poor standards vijijini, hana cha fuel bill wala kodi au ujenzi, screw him!
 
Back
Top Bottom