Leo nilipokuwa napitia blog ya Issamichuzi nilikutana na habari za Mkuu wetu wa nchi kuwa mgeni rasmi kula Marekani kwenye ufunguzi wa mkutano mkuu wa tatu wa chama cha watanzania waishio huko kwa jina la DICOTA. Mhe. Kikwete alitoa hotuba yake kwenye mkutano huo. Pamoja naye, alikuwepo pia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ndg. Membe.
Kilichonishangaza mimi na zaidi kunichangana hadi kufika niweke thread hii hapa ni kauli ya Membe aliyoitoa alipokuwa akifafanua suala la mchakato wa kupata uraia wa nchi mbili. Nanukuu kipande cha habari hiyo "Akisisitiza jitihada za Serikali na za Rais Kikwete katika kuhalakisha suala la uraia pacha, ambalo ni mojawapo ya kilio kikubwa cha watanzania waishio ughaibuni, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa alisema, ingawa ni suala la kikatiba, lakini serikali inategemea kuwa ndani ya kipindi hiki ambapo katiba inapitiwa na kufanyiwa mabadiliko ndiyo wakati muafaka wa suala hili kujadiliwa kwa kina ili likamilishwe na kuingia kwenye Katiba Mpya" mwisho wa kunukuu.
Nukuu hiyo hapo juu inamkariri Waziri huyo akiongelea Katiwa kupitiwa na kufanyiwa mabadiliko. Swali ni je, hivi tunapitia Katiba yetu ama tunaandika katiba mpya? Waziri huyo anamalizia na kutaja jina la Katiba Mpya. Je, hivi tunapopitia katiba na kufanya marekebisho tutapata Katiba Mpya ama ni Katiba ya mwaka 1977 iliyofanyiwa marekebisho mwaka itakaokamilika? Binafsi najua kwamba, Serikali inatambua hitaji letu wananchi kwamba, Katiba Mpya ni kipa umbele na wala siyo kupitia Katiba ya sasa. Mbona Serikali hiyo hiyo viongozi wake waandamizi hawana kauli moja kuhusiana na jambo moja hilo hilo? Je, tuamini kauli ya Membe ni kauli ya boss wake pia? Nini tufanye sasa hivi sisi wananchi ili mazingira hayo ya katiba kupitiwa badala ya kuandikwa mpya yasitokee?