Genekai
R I P
- Feb 9, 2010
- 12,517
- 4,985
Habari za leo wanajamvi? Nilikuwa natoka town traffic ikawa kali sana kwa "jam" ndo nkakumbuka huko nyumbani Bongo. Kuna mradi wa mabasi yaendayo kasi na makubwa ambayo serikali ilikuwa na mpango wa kuyaanzisha hasa Dar kwenye high ways kama Nyerere road, Mandera na Ali Hassan Mwinyi na kufanya vipanya vifanye kazi kwenye feeder roads kama Shekilango, Yombo na nyingine nyingi bongo, naomba nielezwe huo mradi umefikia wapi au ulishaanza? Pia kuna wakati Mh. Pombe Magufuri akiwa waziri wa Ujenzi walianzisha mchakato wa kujenga daraja la kuunganisha City center na Kigamboni na kuna wakati tuliambiwa kuwa NSSF ndo walipewa kazi ya mchanganuo. Sasa jamani wanajamvi, hii mipango imefikia wapi? Ni hayo tu ila kuna mwanasocioligia mmoja alisema "the more we know the stupider we become untill we reach the point of knowing everything about nothing"