Hivi mpenzi wako akikublock namba yako ndio inamaanisha nini?

tang'ana

JF-Expert Member
Apr 3, 2015
11,877
15,444
Habari za leo wapendwa?

Kuna jamaa yangu ana galfriend wake anasoma Mzumbe ya Mbeya. Walikua wako poa tu kimahusiano na kimawasliano. Huyu jamaa makazi yake ni hapa Arusha na gal kwao ni Dar.

Sasa kama week tatu zilizopita huyu manzi alianza kupunguza mawasiliano na jamaa, then jamaa akatumia busara kidogo akamuuliza kulikoni au kama kuna kitu kamkosea amwambie. Manzi akasema hamna kitu ni vile tu yuko bize anajiandaa na final exams.

Well mawasiliano yakawa hivyo hivyo tu ya kusuasua ikafika siku jamaa akampigia manzi akamwambia amwambie lini atakua free ili ndo awe anamtafuta maana kwa wakati ule ilikua kama usumbufu vile na pia alitaka kumpa muda wa kukonsetreti na shule. Manzi akasema tarehe 11 july atakua kamaliza paper.

Wakakaa bila kuwasliana toka 22 june mpaka juzi tarehe 11 ndo jamaa kamtafuta manzi. Wameongea fresh ila manzi akaanza kumlalamikia jamaa angu kwamba hayuko fair coz kipindi kile yeye anamwambia yuko bize akadhani anamdanganya inaonyesha ni jinsi gani hamuamini.

Kukawa na malumbano kidogo hapo mwishowe binti kakasirika na kumblock jamaa number yake, akimpgia anaambiwa number bize. Sasa wakuu,hii kesi imeletwa mbele yangu niitolee maamuzi. Nimemhoji jamaa kama bado anampenda manzi kasema yes na kamfanyia intelijensia kagundua hana mtu yeyote.

Nyie watanzania wenzangu mnaweza kumpa mbinu gani kijana wenu ili aweze kumrejesha msichana wake?
 
kupuuziwa na mwenza inaumaaa!!!!! jaman kama mnasoma huko chuO muwage mnawafeel wenzenu kuw wanaitaj UPENDO wa mahaba sio mawasiliano yanakuwa yakusuasua mda wote upo BUSY,,, kwanin muwatese wenzenu kisa wanaume / wanawake huko chuo ni wengi Pia matata na wazuri kwa sent za wazazi /mikopo ,,, jaribu kusikia kilio cha anaekuwazia kama ni bize hata yey anaweza kuwa bize mbona.
 
Angekuwa kiivyo si angezima simu kabisa ili asiwe hewani kabisa ila huo ubusy wa mtu mmoja tu ni uongo
 
Kama ni wewe au jamaa yako unatakiwa uelewe nukuu hii, "actions speak louder than words". asingoje aambiwe kuwa love expiry date yake imefika-matendo anayofanyiwa yanatosha. Kwa mimi nijuavyo hata kama angekuwa anasoma Yale, Harvard university au Massachusetts Institute of Technology bado angepata muda wa kuchati na mpenzi wake kwa mfano kumtakia usiku mwema, nice day. Ila kukosa hata "morning my love" kunamaanisha kinda aliyesajiliwa huko chuoni anacheza vizuri kiasi kwamba hakuna haja ya mkongwe kuwekwa moyoni tena. Mwambie afanye yake tu maana wanawake hawa tunaoishi nao hawa sijui kichwani wana nini na wanapenda nini zaid kwa mpenzi au mme!
 
Habari za leo wapendwa?

Kuna jamaa yangu ana galfriend wake anasoma Mzumbe ya Mbeya. Walikua wako poa tu kimahusiano na kimawasliano. Huyu jamaa makazi yake ni hapa Arusha na gal kwao ni Dar.

Sasa kama week tatu zilizopita huyu manzi alianza kupunguza mawasiliano na jamaa, then jamaa akatumia busara kidogo akamuuliza kulikoni au kama kuna kitu kamkosea amwambie. Manzi akasema hamna kitu ni vile tu yuko bize anajiandaa na final exams.

Well mawasiliano yakawa hivyo hivyo tu ya kusuasua ikafika siku jamaa akampigia manzi akamwambia amwambie lini atakua free ili ndo awe anamtafuta maana kwa wakati ule ilikua kama usumbufu vile na pia alitaka kumpa muda wa kukonsetreti na shule. Manzi akasema tarehe 11 july atakua kamaliza paper.

Wakakaa bila kuwasliana toka 22 june mpaka juzi tarehe 11 ndo jamaa kamtafuta manzi. Wameongea fresh ila manzi akaanza kumlalamikia jamaa angu kwamba hayuko fair coz kipindi kile yeye anamwambia yuko bize akadhani anamdanganya inaonyesha ni jinsi gani hamuamini.

Kukawa na malumbano kidogo hapo mwishowe binti kakasirika na kumblock jamaa number yake, akimpgia anaambiwa number bize. Sasa wakuu,hii kesi imeletwa mbele yangu niitolee maamuzi. Nimemhoji jamaa kama bado anampenda manzi kasema yes na kamfanyia intelijensia kagundua hana mtu yeyote.

Nyie watanzania wenzangu mnaweza kumpa mbinu gani kijana wenu ili aweze kumrejesha msichana wake?
Huyo demu tayari kamchoka rafiki yako.
 
Huyo ni wewe lakini isiwe shida ngoja nikupe maujanja. Cha kufanya hapo wewe mpotezee tu,huu sio usawa wa kulazimishia mapenzi. Mabinti warembo wapo kibao kwa nini ung'ang'anie usikopendwa. Angekua unamfukuzia huyo manzi ningemuambia ukaze buti ila kwa sababu ni demu wako mpotezee mazima. Mitihani haina uhusiano na mawasiliano,hapo manzi anaona kama unamzingua tu hana ishu na wewe tena. Mpotezee mdau kuwa na moyo wa kiume sio wa kivulana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom