Hivi mpaka nijue kiingereza ndo niajiriwe?

Kaduguda

JF-Expert Member
Aug 1, 2008
724
641
Watanzania wenzangu, nimekuwa nikjiuliza sana bila majibu ya uhakika. Hivi kwa nini ili nipate kazi ndani ya nchi yangu ambayo tumejihalalishia kwamba Kiswahili ni lugha yetu ya Taifa mpaka niandike barua ya kuomba kazi kwa lugha ya kiingereza? Halafu ukienda kwenye usaili haohao waliokwambia uandike barua bado hata kiingereza chenyewe kinawasumbua na matokeo ni usaili huo kufanyika kwa Kiswahili. Ilikuwa na maana gani basi kuandika hiyo barua kwa kiingereza, kwa nini isiwe Kiswahili tu? Kwani kuandika kiingereza ndo kigezo cha kupat kazi?

Naomba tusaidiane hapa kama kuna umuhimu wa kung’ang’anizana kutumia kiingereza hata kwa kazi ambazo hiyo lugha haitumiki kabisa. Mfano, mimi Afisa wa kutoza kodi chini ya halmashauri fulani, kila siku niko minadani na huko ni Kiswahili na lugha za wenyeji wangu ndo zinatumika kwa sana lakini wakati wa kutafuta kazi naambiwa niandike barua kwa kiingereza sasa huu sio utumwa ndugu zangu? Matokeo yake nilichokiona kwa ndugu zangu wengi ni kila barua kuwa na mfanano wa namna fulani yaani utakuta tofauti ni jina tu lakini asilimia kubwa ya maneno ni yaleyale kwa kila barua ya mwombaji. Tufanye nini ili kuondokana na jinamizi hili la utumwa wa lugha?

Nimeona kwenye nchi za wenzetu, kujua kiingereza sio tija sana. Na hata waombapo kazi hiyo lugha sio ya lazima na haswa kama hiyo kazi haitahusisha mawasiliano ya kimataifa. Kwangu naona kung’ang’ania ni kuendeleza utumwa usiokuwa na sababu kwa vijana wetu wa kitanzania.

Nawakilisha!
 
Kwani hujui Kiingereza? Kama unajua, si uandike tu hiyo barua kwa kiingereza ili upate kazi (iwapo hicho ni kigezo)? Katika ulimwengu huu wa utandawazi huwezi kukwepa kiingereza kama focus yako ni zaidi ya kazi za uswahilini. Hivi kwani ukitumia kiingereza, utasahau kiswahili? Mimi huwa nawashangaa sana watu wanaoona matumizi ya Kiingereza ni udhalilishaji wa Kiswahili !!! Kuna nchi nyingi sana ambazo hazina historia ya kuwa na kiingereza, lakini sasa zinalazimika kuwafunza raia wake kiingereza. Kwa mfano Mauritius, masomo yanafundishwa kwa kiingereza licha ya kuwa walitawaliwa na Ufaransa. Huko Maldives, ili mwanafunzi ahesabike amefaulu kustahili cheti, lazima afaulu Kiingereza. Mfano, akipata division I haitasaidia kitu kama hakufaulu Kiingereza. Yote hayo ni kufocus dunia ya sasa inakoelekea. Tusibeze kiingereza eti kwa kuwa lugha ya Taifa ni kiswahili !!
 
Mkuu kama requirement ni kingereza na kazi unaitaka, we kubali tu yaishe, si unajua nchi hii kila kitu kipo upsidedown?
 
Kaduguda pole sana kwa yaliyokukuta. Huu mkanganyiko ni vigumu sana kuuondoa hasa unapokuwa na viongozi wasiowajibika ( akina Mr and Mrs Business as usual) Inasikitisha sana, tuungane sote kwa pamoja kulisemea jambo hili labda mmojawao atasikia na kufanyia kazi
 
Tusibeze kiingereza eti kwa kuwa lugha ya Taifa ni kiswahili !!

Hakuna anayebeza kiingereza, bali ni namna watu wanavyotuchanganya. Kwa nini wakuombe uandike barua kwa kiingereza halafu interview inafanywa kwa kiswahili (logic iko wapi)? Jamani tukipe kiswahili nafasi yake. kama tuliamua iwe lugha ya Taifa basi na iwe hivyo. La sivyo tuwatangazie watanzania kuwa kiingereza kitakuwa lugha ya Taifa. Wamarekani wengi wanajifunza kiswahili lakini hawaambiwi waandike barua za kazi kwa kiswahili. China, vijana wanaanza kusoma kiingereza toka darasa la 4 kama somo mpaka chuo kikuu, lakini kichina ndio hutumika kama lugha ya mawasiliano kasoro kwa kazi zinazohitaji umahili wa kiingereza ndizo wanaweza kukufanyishwa interview ya kiingereza. Brazil wanafanya hivyo hivyo. Sisi wadanganyika tuna matatizo gani?
 
... Kwa nini wakuombe uandike barua kwa kiingereza halafu interview inafanywa kwa kiswahili (logic iko wapi)?

Hapo ni sawa na kuuliza kwa nini wakuambie uandike barua kwa mkono halafu wenyewe wanakujibu kwa barua iliyokuwa typed & printed !!! Lazima ujue kuwa wewe ndiye interviewee, wao hawajipimi ila wanakupima wewe, may be wanataka wajue fluence yako ktk lugha mbili, au nature ya kazi ni kuandika zaidi kuliko kuongea (tukubaliane kuwa kuna watu ni wazuri wa kuandika kuliko kuongea hayo hayo waliyoandika, and may also be vice-versa!!).
 
Hapo ni sawa na kuuliza kwa nini wakuambie uandike barua kwa mkono halafu wenyewe wanakujibu kwa barua iliyokuwa typed & printed !!! Lazima ujue kuwa wewe ndiye interviewee, wao hawajipimi ila wanakupima wewe, may be wanataka wajue fluence yako ktk lugha mbili, au nature ya kazi ni kuandika zaidi kuliko kuongea (tukubaliane kuwa kuna watu ni wazuri wa kuandika kuliko kuongea hayo hayo waliyoandika, and may also be vice-versa!!).


Umahili wa lugha hujulikana kwa kuandika au kwa kuzungumza? Hebu niambie, ni njia gani ambao pasipo na shaka utamjua mtu kuwa yu mahili kwa lugha husika, kwa kuandika au kuzungumza? Kuandika hakusaidii chochote kama hayo maandishi hatoyaandika wakati wewe ukiwa unamsimamia maana mtu anaweza akaandika barua ya mtu mwingine kwa mkono wake. Lakini kwenye usahili, kama ni John anatakiwa kujibu maswali tunauhakika kuwa ndiye na si Peter. Hivyo kama tunataka kujua kuwa John ni mahili wa lugha ya kiingereza lazima tumshoot maswali ya kiingereza otherwise itakuwa ni kubabaisha tu
 
Hapo ni sawa na kuuliza kwa nini wakuambie uandike barua kwa mkono halafu wenyewe wanakujibu kwa barua iliyokuwa typed & printed !!! Lazima ujue kuwa wewe ndiye interviewee, wao hawajipimi ila wanakupima wewe, may be wanataka wajue fluence yako ktk lugha mbili, au nature ya kazi ni kuandika zaidi kuliko kuongea (tukubaliane kuwa kuna watu ni wazuri wa kuandika kuliko kuongea hayo hayo waliyoandika, and may also be vice-versa!!).

Ndugu Sinkala! Eneo la kazi wilaya mojawapo TZ, mwajiri Mtanzania/serikali ya Tanzania, ninaotarajia kuwatumikia Wa-TZ, lugha ya mawasiliano kuanzia kwa wafanyikazi wenzangu mpaka raia ni Kiswahili. Maombi niandike kwa kiingereza sioni mantiki hapa. Na kumbuka pia katika jukumu langu la kazi sina hata sehemu ambayo nalazimika kutumia kiingereza, kwa nini wanishurutishe?

Haya barua yenyewe ni kama tumeigirishiana mimi, A, B, na C karibu kila kitu twafanana. Huu kwangu ni ulimbukeni kwani hii haioneshi kwamba najua hiyo lugha bali ni kutimiza matakwa yao tu. Na pia hata hao wasaili wangu wenyewe kiingereza chao unaweza cheka au uka-JOB HUNDRED- "Ukazimia"
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom