Hivi mnaweza kutabiri matokeo, iwapo utafiti kama huu utafanyika hapa nchini..............?

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,393
Watafiti wa chuo kikuu cha Colorado na Texas walifanya utafiti kuhusiana na wanawake kutoka nje ya ndoa zao. Katika utafiti huo wataalamu hao waliwahoji wanawake 4,884 walioolewa kwa mtindo wa mahojiano ya uso kwa uso na mtindo wa mahojiano ya siri kwa kutumia njia ya maswali katika kompyuta.

Katika njia ya kwanza ya maswali ya uso kwa uso ni asilimia 1 tu ya wanawake hao walikiri kuzisaliti ndoa zao miaka ya nyuma na katika njia ya pili ya kujibu maswali kwa njia ya Kompyuta wenyewe wanaita questionnaire ilipatikana asilimia 6 ya wanawake hao waliokiri kuzisaliti ndoa zao. Utafiti huo umeripotiwa katika Chapisho moja la hivi karibuni la The Journal of Family Psychology la nchini Marekani.

Lakini hata hivyo chapisho hilo limetoa habari za kushangaza kuhusiana na wanandoa kutoka nje ya ndoa zao hususan kwa wanandoa vijana pamoja na wanandoa wazee wenye umri wa miaka zaidi ya 60. Kwa mfano Watafiti wa Chuo Kikuu cha Washington nchini Marekani wamebaini kwamba usaliti kwenye ndoa kwa wanaume wenye umri zaidi ya miaka 60 umeongezeka hadi kufikia asilimia 28, mwaka 2006 ukilinganisha na mwaka 1991 ambapo ilikuwa ni asilimia 20. Kwa wanawake walio na zaidi ya miaka 60, wao usaliti katika ndoa zao umeongezeka hadi kufikia asilimia 15 mwaka 2006 tofauti na mwaka mwaka 1991 ambapo usaliti kwa vikongwe hao ilikuwa ni asilimia 5 tu………….. Duh hii ni kasheshe kubwa!

Hata hivyo kwa wanandoa vijana mambo bado ni kizungumkuti, wanaume wanaofikia asilimia 20 na wanawake wanaofikia asilimia 15 walio na chini ya umri wa miaka 35 walikiri kuzisaliti ndoa zao.

Watafiti hao walizitaja sababu za wanandoa vikongwe kuingia katika kizungumkuti hicho cha kuzisaliti ndoa zao, sababu zilizotajwa ni ujio au uwepo wa tiba za kitabibu na dawa za kuongeza nguvu za kiume, kwa mfano Viagra kwa wanaume na kwa wanawake tiba za kitabibu za uboreshaji wa maumbile yao hususan mahipsi, matiti na via vya uzazi zimewaongezea ashki na hivyo kutaka kujikumbusha enzi za ujana wao.

Kwa wanandoa vijana sababu zilizotajwa ni uwepo huria wa filamu za ngono, pamoja na upatikanaji wa video za ngono katika mitandao ya intenet kumepelekea wanandoa vijana kusaliti ndoa zao kutokana na tamaa yan kutaka kujaribu aina mpya ya kufanya mapenzi na hiyo huwapelekea kuzisaliti ndoa zao.
 
Ngoja hizo mashine za kunyanyua matiti zilizopo duka fulani huko Sinza zisambae nchi nzima, hapo ndipo tutapata matokeo mazuri ya utafiti wetu!
 
Ngoja hizo mashine za kunyanyua matiti zilizopo duka fulani huko Sinza zisambae nchi nzima, hapo ndipo tutapata matokeo mazuri ya utafiti wetu!

hivi tunafanya utafiti wa nini tena....?.....nimesahau.....

 

Lakini hata hivyo chapisho hilo limetoa habari za kushangaza kuhusiana na wanandoa kutoka nje ya ndoa zao hususan kwa wanandoa vijana pamoja na
wanandoa wazee wenye umri wa miaka zaidi ya 60. Kwa mfano Watafiti wa Chuo Kikuu cha Washington nchini Marekani wamebaini kwamba usaliti kwenye ndoa kwa wanaume wenye umri zaidi ya miaka 60 umeongezeka hadi kufikia asilimia 28, mwaka 2006 ukilinganisha na mwaka 1991 ambapo ilikuwa ni asilimia 20. Kwa wanawake walio na zaidi ya miaka 60, wao usaliti katika ndoa zao umeongezeka hadi kufikia asilimia 15 mwaka 2006 tofauti na mwaka mwaka 1991 ambapo usaliti kwa vikongwe hao ilikuwa ni asilimia 5 tu………….. Duh hii ni kasheshe kubwa!
Dah!! Si mchezo vikongwe wanapiga infidelity kweli kweli....
 
Watafiti wa chuo kikuu cha Corolodo na Texas sijui waliwapata wapi hao wanawake vizee wa miaka 60, mpaa wakaja na result hizo.
 
mbona kwa umri less than 35 years hawajaonyesha kama kuna ongezeko la kucheat au la kama walivyofanya kwenye umri mkubwa?
ila 20% ni nyingi jamani yaani mwanaume mmoja kati ya watano,ana cheat.....mnh na magonjwa haya,now i understand kuolewa ni moja ya very risky game,lol...i wont trade my life like that.....siolewi ng'o nisije nikafa mapema...nitakufa na natural causes sio binadamu mwenzangu anipeleke kaburini ...NO kwa kweli lol
 
mbona kwa umri less than 35 years hawajaonyesha kama kuna ongezeko la kucheat au la kama walivyofanya kwenye umri mkubwa?
ila 20% ni nyingi jamani yaani mwanaume mmoja kati ya watano,ana cheat.....mnh na magonjwa haya,now i understand kuolewa ni moja ya very risky game,lol...i wont trade my life like that.....siolewi ng'o nisije nikafa mapema...nitakufa na natural causes sio binadamu mwenzangu anipeleke kaburini ...NO kwa kweli lol
Kila kitu kina pande mbili, na bila hizo changamoto za ku-cheat katika mahusiano, maisha yangekosa ladha kabisa ..............
 
Back
Top Bottom