Hivi mnawachukuliaje watu wanaopiga picha katika ajali mbalimbali?

TRUTH gasper

Member
Mar 27, 2017
64
82
Habari wana JF,

Hivi mnakubaliana na hili swala la watu kuposti au kupiga picha za ajali na kuweka katika mitandao? Hebu jiweke kwenye position ya undugu wa aliepoteza maisha alafu kumbuka picha zitakaa miaka yote tuone unajisikiaje.
 
Hili swala tumeshalipigia sana kelele lakini wapi.. Siku hizi kila mwenye simu amegeuka muandishi wa habari.. Mtu akiona ajali cha kwanza anachofikiria ni kutoa simu apige picha apost kwenye mitandao.
 
Mimi binafsi hata kama sio ndugu yangu kupiga picha au kurekodi cwez...Siku hizi watu wanapata matatizo wengi wetu tunageuka wapiga picha
 
Kuna wengine hawana aibu kabisa,wakati wa kuaga mwili anakua na simu ili ampige picha marehemu
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Sasa hivi hata madaktari kitu cha kwanza ni kumpiga mgonjwa picha (hata kama yu uchi) na kuzitupia mtandaoni
 
Bila ya hizi picha hatutajifunza chochote,chonde chonde ndugu zangu watanzania ukiona tukio la ajali mauwaji uonevu manyanyaso pigeni picha ili ili tushikamane kwenye kupinga watanzania tuko wengi.
 
Kinacholeta shida ni utitiri wa wapiga picha wasio na mafunzo ya uandishi wa habari. Kama kazi hiyo wangeachiwa waandishi sio mbaya maana wao wana maadili na wanajua ni picha gani za kuonywsha umma na ni zipi hazifai. Utakuta picha kwenye gazeti imefunikwa kivuli maeneo fulani ya mwili kwa kuwa hayafai kuonyeshwa au unaangalia BBC News wanaripoti tukio fulani la kikatili halafu wanaomba radhi kuwa picha hazitaonyeshwa kwa kuwa zinatisha mno. Halafu kazi ya kupiga picha wakiachiwa professionals wengine tutasaidia walioumia badala ya kila mtu kung'ang'ania kupiga picha.
 
Kwa upande wao ni sawa...
Usitake watu wafanane mtazamo.
VIEWS ARE ASSHOLES AND EVERYONE GOT ONE.... Kwa hiyo kama wao wanaona kupiga picha ni sawa wewe kausha.
 
Mijitu imekuwa mijinga kweli.

Mtu anaacha kusaidia watu waliopata ajali wanakimbilia kupiga picha.

Picha nyingine sio nzuri lakini jitu na akiili zake linaziweka mtanaoni.
 
Mleta mada na wanaokusapoti acheni unafiki...humu jf Uzi ukija bila picha utasikia tukuaminije "weka picha"

Kwani kupiga picha kuna madhara gani? Kunabadilisha uhalisia kua walokufa wamekufa? Usipopiga ajali picha utarejesha roho za marehemu?

Jengo linaungua ncpopiga picha litaacha? Tuacheni unafiki na tukubaliane na wakati uloopo
 
Acha uoga.[/QUOi acha akae na uoga natamani akamatwe mmoja wamfanyie MF.. MTU amechinjwa jitu linapost et type amen amen ya mavi...huko fb ndio hakufai kabisa kwanza picha za maiti ni confidancial wakae nazo ndugu wa karibu na mamlaka husika kama police na hospital..ifike mahal watu tujitambue na tujue.utu ni nini..
 
Mijitu imekuwa mijinga kweli.

Mtu anaacha kusaidia watu waliopata ajali wanakimbilia kupiga picha.

Picha nyingine sio nzuri lakini jitu na akiili zake linaziweka mtanaoni.

Hakuna picha mbaya.. aliekufa kafa tu no way
 
Back
Top Bottom