Hivi mnaujua wimbo wa Taifa wa Zanzibar?

yani hakunaga mwenye kufahamu maneno yaliyoko kwenye wimbo wa Jamhuri ya Zanzibar?
Maneno ya Wimbo la Taifa la (Zanzibar) Unguja na Pemba ni haya:
Mungu ametubarikia, Unguja na Pemba yote.
Sote tunashangillia, Jamhuri kutuletea.
Mungu ametubarikia, Jamhuri kutuletea.

Wimbo huu ulianza kutumia mara tu baada ya mapinduzi ya 1964 na kuwacha wimbo huu
iliokuwa unatumika tangu 1911-1964.​
 
Last edited by a moderator:
Zanzibar ikijitenga, watapata msukosuko kidogo, watagundua kumbe sisi ni Waunguja na wao Wapemba.
Hapo ndio utamu uliko, Pemba wimbo wao wa Taifa utakuwa na mahadhi ya Kibao Kata, na Unguja wimbo wao utakuwa na mahadhi ya Hamada Amelewaaa

Bujibuji mbavu zangu
 
Waaacheeeee waimbe wanavyojua, hii ndoa ya Tanganyika na Zanzibar ingekuwa inafuata misingi kama ile ya ndoa halisi za Kiislam tungeshakuwa tumeachana.
halafu wazenji si %98 waislam?
 
Maneno ya Wimbo la Taifa la (Zanzibar) Unguja na Pemba ni haya:
Mungu ametubarikia, Unguja na Pemba yote.
Sote tunashangillia, Jamhuri kutuletea.
Mungu ametubarikia, Jamhuri kutuletea.

Wimbo huu ulianza kutumia mara tu baada ya mapinduzi ya 1964 na kuwacha wimbo huu
iliokuwa unatumika tangu 1911-1964.​

mkuu nimekasikia kamelodi. ni kazuri by the way
 
Last edited by a moderator:
Yap! kamelodi kake katamu, lkn kumbuka kuwa haka kamelodi haka ni kale ka wimbo wa mkoloni. Wa Zanzibar wa sasa uko chapwa sana.

ok kumbe sio huu niiliosikia juzi pale stadium? Halaf hiyo chapwa umetuacha wengi
 
Nimeona kupitia TBC1 hapa mpambano kati ya Burundi na Zanzibari. Nyimbo zao za Taifa zimepigwa, nikasikia melody ya wimbo wa Zanzibar. Hauna mfanano wowote na wimbo wetu wa tanganyika. Inakuwaje mataifa kama Zimbabwe, Afrika ya Kusini wana melody inayofanana na Tanganyika wakati Zanzibar ambayo tumeungana nayo hakuna mfanano wowote? Kadhalika naombakama kuna mtu mwenye maneno yaliyo kwenye wimbo wa Taifa wa Zanzibar atuwekee humu

Inshalla! Mashallah!!! Allah!! Allah!! Allah!! Mashallah!!!!!!!!!!!!!!!! Bila shaka hayo yamo.

jamani kumbe zanzibar nao wana wimbo wa taifa. sasa swali hapa wa bara tuanapoimba....MUNGU IBARIKI TANZANIA INAKUWAJE HAPO?
 
wana rais, wana ngao ya rais, wana wiwbo wa taifa, wana mahakama kasoro ya rufaa na pia wana kadhi courts, wana bunge what else do u want to bcam a state? zanzibar ni nchi ambayo ni kama iko utumwani as some powers ziwekuwa withheld. YES for three or one gvt kwenye muungano na sio 2 gvts kama sasa Nyerere kiboko
 
Zanzibar ikijitenga, watapata msukosuko kidogo, watagundua kumbe sisi ni Waunguja na wao Wapemba.
Hapo ndio utamu uliko, Pemba wimbo wao wa Taifa utakuwa na mahadhi ya Kibao Kata, na Unguja wimbo wao utakuwa na mahadhi ya Hamada Amelewaaa

ahsanteeee!sikuwahi kufikiri na huku siasani naweza kushikilia mbavu zangu kama hivi !lol!
 
Nikikurekebisha kidogo ndugu mtoa mada, Tanganyika haina wimbo wake kwa sasa. Wimbo huu wa Mungu ibariki Tanzania kama unavyojieleza ni Wa Tanzania ikiwemo pia Znz ndani yake. Ndio maana Taifa stars inayohusisha pia wachezaji toka Znz ikiwa inacheza na timu nyingine ya nje hupiga wimbo huohuo wa Tanzania sawa sawa pia na ikisimama yenyewe kama Tanganyika.
 
Mkae mkijua Zanzibar ni nchi kamili, ni "Tanganyika" tu ndiyo inayoumwa "Identity crisis"
 
Zanzibar ikijitenga, watapata msukosuko kidogo, watagundua kumbe sisi ni Waunguja na wao Wapemba.
Hapo ndio utamu uliko, Pemba wimbo wao wa Taifa utakuwa na mahadhi ya Kibao Kata, na Unguja wimbo wao utakuwa na mahadhi ya Hamada Amelewaaa

Mkuu Bujibuji umemake my day dah! Umeniacha hoi sana dah!!
 
Back
Top Bottom