Hivi mnaposema Simba inajiendesha kwa hasara mnafikiria nini?

Cashman

JF-Expert Member
Jun 8, 2018
2,293
3,962
Naomba nipate ufafanuzi.Iwapo Simba inapata hasara kwa uwekezaji wa Bilioni 20 +25 tunazoambiwa,je huyu Azam media angepata faida gani kuwekeza bilioni 48 kwa Simba?

Je, Simba ikiamua kutangaza biashara yoyote,mfano ya bia n.k,wanaweza kulipwa kiasi gani kwa mwaka?

Je, Simba hii, hii, ukichukua idadi ya wanachama ilio nao,kila mmoja akanunua kadi ya uanachama kwa shilingi elfu 20,itaingiza kiasi gani?

Je, viingilio katika mechi,vinamchango wa shilingi ngapi kwa mwaka?

Je, mauzo ya jezi na Bidhaa nyingine za Simba,vinaingiza shilingi ngapi?

Iwapo kampuni au kiwanda kimoja tu cha dawa,kinatumia zaidi ya bilioni 20kutangaza bidhaa zake,je wakitokea wawekezaji wawili tu,waamue kutoa bilioni 5 kila mmoja kwa mwaka kudhamini Simba,hiyo pesa haitoshi kujiendesha kwa mwaka mmoja?

Ifike mahali tuache kuidhoofisha timu kwa kutaka kupata umaarufu binafsi tu.

Ninachokiona ,kama Simba inaendeshwa kwa hasara,basi ni uzembe wa mwekezaji katika kuitumia Simba kufanya biashara.

Leo nasema huyu mwekezaji ana bidhaa zake zinaidhamini Simba,lakini hatumii watu wenye akili kumtangazia biashara zake kupitia Simba.

Azam wako vizuri kimkakati na ndio maana bidhaa zao zinapendwa sana.

Sasa hivi kwa kanda ya ziwa kuna kampuni ya Jambo wanakuja juu sana katika biashara ya vinywaji baridi,

Mo anatumia watu cheap,au anatumia vyeti vya watu badala ya kutumia akili za watu wafanye ubunifu kwa kuanzia logo hadi muonekano wa bidhaa zake.

Mabidhaa yake ninayoyajua,wametumia basic colors kuyapamba utadhani nyumba za vijijini zinavyopambwa na rangi za kukoleza. Hajui kuwa anahitaji wataalamu wanaoweza kukuwekea rangi kwenye bidhaa,ikamvutia mnunuzi kutumia bidhaa yako.

Aende Kenya kuwauliza sunlight wanatengenezaje sabuni zao za unga hadi zinatafutwa sana madukani na hazionekani.Sio unatutengenezea misabuni ya kufulia maturubai pekee.Huwezi kutoa na zile za kufulia nguo za maana zikiwa na franrance za maana?

Simba ni timu kubwa kamwe haiwezi kuleta hasara,isipokuwa mikakati ya kimenejerial ndiyo mibovu.Mfano ni ni pale kupata kadi ya Simba ni kama vile unaomba Visa ya Marekani.Hakuna matangazo ya wazi ni wapi zinauzwa,kwa bei gani.Hata jezi tu huku mikoani hazipo,na watu wako tayari hata kununua kwa sh. Elfu 50 mradi ziwe za vuwango.

Ukitaka kushusha kiwango ili watu wengi wanunue hii nayo ni mikakati ya kizembe. Hao utopolo kuna watu walitoka huku mikoani kwenda kununua jezi za yanga kuna walionunua kwa sh. Elfu 80 jezi moja.Ninawafahamu ni askari wa jeshi.

Leo mtu mmoja ana kaa mahali anatuaminisha eti Simba ina hasara?Kivipi?
 
Naomba nipate ufafanuzi.Iwapo Simba inapata hasara kwa uwekezaji wa Bilioni 20 +25 tunazoambiwa,je huyu Azam media angepata faida gani kuwekeza bilioni 48 kwa Simba?

Je Simba ikiamua kutangaza biashara yoyote,mfano ya bia n.k,wanaweza kulipwa kiasi gani kwa mwaka?

Je Simba hii,hii,ukichukua idadi ya wanachama ilio nao,kila mmoja akanunua kadi ya uanachama kwa shilingi elfu 20,itaingiza kiasi gani?

Je viingilio katika mechi,vinamchango wa shilingi ngapi kwa mwaka?

Je mauzo ya jezi na Bidhaa nyingine za Simba,vinaingiza shilingi ngapi?

Iwapo kampuni au kiwanda kimoja tu cha dawa,kinatumia zaidi ya bilioni 20kutangaza bidhaa zake,je wakitokea wawekezaji wawili tu,waamue kutoa bilioni 5 kila mmoja kwa mwaka kudhamini Simba,hiyo pesa haitoshi kujiendesha kwa mwaka mmoja?

Ifike mahali tuache kuidhoofisha timu kwa kutaka kupata umaarufu binafsi tu.

Ninachokiona ,kama Simba inaendeshwa kwa hasara,basi ni uzembe wa mwekezaji katika kuitumia Simba kufanya biashara.

Leo nasema huyu mwekezaji ana bidhaa zake zinaidhamini Simba,lakini hatumii watu wenye akili kumtangazia biashara zake kupitia Simba.

Azam wako vizuri kimkakati na ndio maana bidhaa zao zinapendwa sana.
Sasa hivi kwa kanda ya ziwa kuna kampuni ya Jambo wanakuja juu sana katika biashara ya vinywaji baridi,

Mo anatumia watu cheap,au anatumia vyeti vya watu badala ya kutumia akili za watu wafanye ubunifu kwa kuanzia logo hadi muonekano wa bidhaa zake.

Mabidhaa yake ninayoyajua,wametumia basic colors kuyapamba utadhani nyumba za vijijini zinavyopambwa na rangi za kukoleza. Hajui kuwa anahitaji wataalamu wanaoweza kukuwekea rangi kwenye bidhaa,ikamvutia mnunuzi kutumia bidhaa yako.

Aende Kenya kuwauliza sunlight wanatengenezaje sabuni zao za unga hadi zinatafutwa sana madukani na hazionekani.Sio unatutengenezea misabuni ya kufulia maturubai pekee.Huwezi kutoa na zile za kufulia nguo za maana zikiwa na franrance za maana?

Simba ni timu kubwa kamwe haiwezi kuleta hasara,isipokuwa mikakati ya kimenejerial ndiyo mibovu.Mfano ni ni pale kupata kadi ya Simba ni kama vile unaomba Visa ya Marekani.Hakuna matangazo ya wazi ni wapi zinauzwa,kwa bei gani.Hata jezi tu huku mikoani hazipo,na watu wako tayari hata kununua kwa sh. Elfu 50 mradi ziwe za vuwango.
Ukitaka kushusha kiwango ili watu wengi wanunue hii nayo ni mikakati ya kizembe.
Hao utopolo kuna watu walitoka huku mikoani kwenda kununua jezi za yanga kuna walionunua kwa sh. Elfu 80 jezi moja.Ninawafahamu ni askari wa jeshi.
Leo mtu mmoja ana kaa mahali anatuaminisha eti Simba ina hasara?Kivipi?
25 + 20 = 85

Makolo wamepigwa na kitu kizito hapa
 
Attachments

  • hajismanara_1644433070950722.mp4
    3.2 MB
Mkuu ni rahisi sana kuongea kuliko kuweka vitu kwenye uhalisia, hakuna mtu yeyote au kampuni anaweza kuipa simba bilioni 5 kwa mwaka. Pili ni wanachama wachache mno wa kuweza kutoa 20k ya uanachama
Watanzania tutaendelea kuwa na mawazo mgando Hadi lini lakini? Yaani full kukatishana tamaa kwamba hatuwezi na hapo ndiyo wajanja wachache Kama Mo wanatake advantage. Tutanyonywa Hadi tukome tusipobadilika.
 
Jezi 35000 na bado watu hawanunui
Viingilio 7000
Zawadi ya ubingwa kidogo
Hela ya mdhamini mkuu sport pesa kidogo
 
Wawekezaji walitakiwa wasipungue 3 mo akafanya kila mbinu awe peke yake, ukienda mnazi mmoja kuna khanga zinauzwa za chapa ya simba zimetengenezwa na kiwanda chake bila simba kupata chochote.
Mauzo ya wachezaji alifanya siri kiasi walichouzwa, kama bilioni 20 ipo wanashindwa kwenda benki kuomba mkopo wa kujenga kiwanja
 
Utopolo akili huna, hizo kanga mama yako alishawai nunua
Unaulizia mauzo kwanini usiulizie mishahara? Ukitoa chama na luis ni mchezaji gani mwingine ameuzwa mpaka useme kuwa kunamapato yanatokana na uuzaji wa wachezaji
 
Watanzania tutaendelea kuwa na mawazo mgando Hadi lini lakini? Yaani full kukatishana tamaa kwamba hatuwezi na hapo ndiyo wajanja wachache Kama Mo wanatake advantage. Tutanyonywa Hadi tukome tusipobadilika.
Peleka hizo 5b uone kama simba watakataa
 
Ni ngumu mashabiki kunua jezi original na kulipia kadi sh elfu 20..
Nirahisi kuongea kuliko kutenda..
 
Utopolo akili huna, hizo kanga mama yako alishawai nunua
Unaulizia mauzo kwanini usiulizie mishahara? Ukitoa chama na luis ni mchezaji gani mwingine ameuzwa mpaka useme kuwa kunamapato yanatokana na uuzaji wa wachezaji
Haya ni matusi ya Waarabu, bila shaka wewe ni Mwarabu.
 
Back
Top Bottom