Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 9,335
- 13,293
Kuna viroja kila siku watu wanaandika humu! Eti kuna madudu, mara wizi, mara ufisadi nk., CAG kaibua baada ya kufanya ukaguzi wake! Lakini hata siku moja hujasikia kuna watu wametuhumiwa, wamekamatwa, wameshtakiwa wala kufungwa kutokana na ukaguzi huo!!
Ukweli ni kuwa hakuna madudu wala ufisadi wo wote unakuwa umetendeka, bali ni hoja za ufafanuzi ambazo CAG anaomba apewe na mara anapopewa ufafanuzi huzifuta hoja hizo mara moja!!
Sasa baadhi ya magazeti wakiwemo wanaJF wamekosa uelewa wa namna CAG anavyotoa hoja zake na hivyo kutaka kuwaaminisha wasomaji kuwa katika idara za serikali na mashirika yake hakuna uaminifu wala weledi katika utendaji wa kazi!!
Huu ni upotoshaji wa hali ya juu na unapaswa kukemewa na kukomeshwa mara moja kwa kuwa unawakatisha na kuwavunja moyo watumishi wa umma ambao usiku na mchana hawalali ili kulinda na kuwaletea wananchi maendeleo.