LE GAGNANT
JF-Expert Member
- Jan 20, 2011
- 1,241
- 251
Usimba na uyanga unachangia sana kuua soka la tz
Usimba na uyanga unachangia sana kuua soka la tz
Tanzania hatuwezi fika mbali kisoka sababu 10% na undungunaizeshe wa TFF, tulikuwa na kikosi kizuri kile cha copa coca cola kile kikosi kisingevunjwa tungekuwa zaidi ya chipolopolo.
Pili tujue ni jinsigani ya kuiandaa timu ya taifa, kipindi kile 1993 baada ya wachezaji wote kupoteza maisha wakati huo KK aliunda timu ya vijana akawapeleka brazili, akajitoa kwenye mashindano yote ya kimataifa akaisuka timu taratibu bila haraka ndipo wakapata hiki kikosi walianza kufundishwa zamani wakiwa bado kinda sasa wamekomaa kazi yao imeonekana wazi.
Tukitaka kufika walipo Zambia inabidi tutafute makinda tuwape mafunzo ya uhakika taratibu bila haraka nasi tutafikia walipo Zambia ama hata zaidi ya Zambia, tuache ubabaishaji na undugunaizesheni, ushkaji na mambo ya 10% tutafika mbali.
Wachezaji ndiyo wa kulaumiwa na siyo kocha. Tujiulize mara ya mwisho kushiriki AFCON hadi leo ni makocha wangapi tumekuwa nao na hakuna lolote la maana, je wote hao hawana mbinu za ufundishaji? Ni muda muafaka kuiweka hii timu ya wazee pembeni na kuishirikisha timu ya chipukizi.
Hapo umemchukulia Herve Renard kama ndio siri pekee ya mafanikio ya Zambia, kwamba angepewa kikosi chochote hata kama dhaifu kama hiki chetu basi angeweza tu kushinda CAN 2012! Si kweli bana...uwepo wa wachezaji wenye kiwango kikubwa ni moja ya sababu ilizoifanya Zambia ishinde, hatuna sisi wachezaje kama wale wa Zambia. Labda Paulsen angekuwa na mafanikio zaidi ya Renard kama angepata kikosi kama cha Zambia...nobody knows!
Wachezaji wa Tanzania hawana malengo, wanalewa sifa za kijinga, wanasahau kinachofanya wawe pale, ni mambumbumbu.
Viongozi wa soka Tanzania, hawana vision, hawashauriki, wapo pale kwa interest zao
Ni ndto tanzania kushiriki mashindano yoyote ya kimataifa, hata tukienda ni ndoto kufika hata robo final achilia mbali kuchukua kombe
Chibingo, tatizo la Watanzania wanaoongoza soka katika TFF na katika vilabu vyetu wengi wao huwa ni wanasiasa tuu. Hugombania nafasi hizo ili wajulikane na baadaye utawasikia wanagombea UBUNGE.Katika kumtafuta mrithi wa Marcio Maximo Kocha wa Zambia Herve Renard aliomba kuifundisha Taifa Stars lakini TFF wakasema hakidhi vigezo (hana qualification), ikabidi wamuajiri Poulsen. Tujiulize, je huyu Poulsen katufikisha wapi na huyu Herve Renard "the chosen one" au Mourinho wa Africa amewafikisha wapi Chipolopolo? Nawasilisha.
Tatizo laTanzania sio kocha bali mfumo tulio nao sio wakutengeneza teaminayoweza kuleta ushindani kokote mfumo wetu unaruhusu wahuni kuingia katika team kubwa na hatimae taifa sasa leo Bongo hata akija Mourinho bado tutakuwa kichwa cha mwendawazimu