HIVI MNAIKUMBUKA HABARI HII??Uhasama wa CCM, CHADEMA Arusha wahamia serikalini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

HIVI MNAIKUMBUKA HABARI HII??Uhasama wa CCM, CHADEMA Arusha wahamia serikalini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by AMARIDONG, Jun 8, 2011.

 1. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  Uhasama wa CCM, CHADEMA Arusha wahamia serikalini

  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]Mbunge Lema asusiwa hafla na vigogo watendaji

  [​IMG]Awezesha wanafunzi 400 wa shule za kata kusoma bure

  UHASAMA wa kisiasa baina ya watendaji wa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika wilaya ya Arusha Mjini na viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) umezidi kukua baada ya watendaji wa serikali walioalikwa katika uzinduzi wa mpango wa kuwasomesha bure wanafunzi kutoka familia masikini ambao ulibuniwa na CHADEMA, kususuiwa na watendaji hao.
  Miongoni mwa viongozi wa Serikali walioalikwa katika uzinduzi huo, lakini hawakuhudhuria, ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Isdori Shirima, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Raymond Mushi na Mkurugenzi wa Manispaa ya Arusha, Estomih Chang’a.
  Sherehe hizo zilifanyika Jumapili iliyopita katika uwanja uliopo nje ya ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Arusha na kuhudhuriwa na walezi na wazazi wa wanafunzi 400 waliopata udhamini wa masomo ya sekondari kutoka kwa Taasisi ya Maendeleo ya Jimbo la Arusha (ArDF).
  Pamoja na kupata ufadhili huo wa masomo, wanafunzi hao pia watapata fursa ya kutibiwa bure katika vituo vya afya vinavyomilikiwa na Shirika la Green Hope la Canada lenye matawi yake Mjini Arusha, na watatumia kadi maalumu kama zile za Mfuko wa bima ya Afya.
  Taasisi hiyo ya (ArDF) ilibuniwa na wenzake, kama chombo cha kuchochea maendeleo ya jimbo hilo; huku wakilenga katika sekta za elimu, afya, maji na miundo mbinu na ilizinduliwa Desemba mwaka jana.
  Taasisi hiyo ambayo malengo yake si ya kisiasa ilianzishwa ili kusimamia miradi ya maendeleo katika maeneo kadhaa ambayo si rahisi kufikiwa na bajeti ya serikali, na imekuwa ikitumia fedha zinazochangwa na wananchi wa Arusha pamoja na wafadhili wa nje.
  Eneo la kwanza ambalo taasisi hiyo ilijitokeza kusadia ni katika sekta ya elimu ambapo itawalipia ada na mahitaji mengine muhimu wanafunzi wa shule za sekondari za serikali za kata kutoka familia masikini za jimbo la Arusha Mjini ambazo hazina uwezo. Mpango huo ulizinduliwa Jumapili katika hafla ambayo, hata hivyo, ilisusiwa na viongozi wa serikali ya CCM waliopewa mwaliko.
  Taarifa kuwa viongozi wote wa juu wa serikali mkoani Arusha walipewa mwaliko zilithibitishwa na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Elfuraha Paul Mtowe, wakati wa uzinduzi alipozungumza na Raia Mwema.
  “Ni kweli tulikuwa tumewaalika viongozi wote wa juu; yaani Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa Halmashauri na maafisa wengine, lakini kama unavyoona hawakutokea, na kibaya zaidi hawakutuma hata wawakilishi wao”, alisema Mwenyekiti huyo wa ArDF.
  Mtowe aliongeza kuwa iwapo viongozi hao wangehudhuria, wangepata fursa nzuri ya kufahamu baadhi ya changamoto ambazo taasisi yake inakabiliana nazo ambazo wao kama viongozi wa serikali wako katika nafasi nzuri ya kutoa ushauri, na pia kutafuta suluhisho la changamoto hizo.
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Isdori Shirima hakupatikana kuelezea sababu zilizofanya washindwe kuhudhuria uzinduzi huo; kwani kila alipopigiwa simu juzi simu yake ilikuwa inaita bila kujibiwa, lakini taarifa zilizopatikana kutoka kwa baadhi ya maafisa wa serikali zilidai kuwa viongozi hao walichukulia tukio hilo kama la kisiasa kwa mradi huo uliobuniwa na viongozi wa CHADEMA.
  “Waliobuni mpango huo ambao umepokelewa kwa mwamko wa aina yake na wananchi wa Jimbo la Arusha, ni viongozi wa CHADEMA, na kutokana na uhasama uliopo kwa sasa baina ya CHADEMA na CCM ambayo ndiyo yenye serikali, viongozi wa serikali walichukulia tukio hilo kuwa la kisiasa hivyo walilipuuza”, alisema Ofisa mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina gazetini.
  Ofisa huyo aliongeza kuwa viongozi wa serikali wanaona kuwa hatua ya kuhudhuria uzinduzi huo ni sawa na kumpa “ujiko” mbele ya wananchi Mbunge huyo wa Arusha Mjini ambaye alikuwa anaadhimisha siku 100 tangu achaguliwe kuwa mbunge, na tayari wananchi wengi wanaanza kupata imani kuwa anaweza kuondoa kero zao za msingi tofauti na wabunge waliomtangulia.
  Uhasama kati ya vyama hivyo katika jimbo hilo ulianza tangu wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu, na kuendelea hadi wakati wa uchaguzi wa Meya wa Manispaa ya Arusha ambapo uchaguzi huo ulilalamikiwa na CHADEMA ambao waliitisha maandamano kupinga matokeo yake na kusababisha watu watatu kupoteza maisha baada ya kupigwa risasi na polisi.
  Akizungumza katika uzinduzi huo, Mbunge Lema ambaye pamoja na kueleza kusikitishwa kwa na hatua ya viongozi hao kususuia uzinduzi alisema hatua hiyo inatokana na Watanzania kuwa na fikra hasi katika mambo ya msingi.
  “Hatua ya viongozi wa serikali ni mwendelezo wa kuwepo kwa fikra mgando katika jamii ya Watanzania katika mambo ya msingi, na hali hii imekuwa tatizo katika utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo kwa nchi”, alisema.
  “Kama Watanzania tungekuwa na fikra chanya tunaweza kuwa si tu Taifa lenye maendeleo ya kuwa na barabara, shule na hospitali nzuri; bali Taifa la wazalendo wanaopenda nchi yao na vitendo viovu kama ufisadi visingekuwa na nafasi”, alisema.
  ……..”Sehemu kubwa ya ardhi ya Taifa dogo la Israel ni jangwa na ardhi yake haifai kwa kilimo, lakini Taifa hilo ni moja ya nchi zinazozalisha matunda kwa wingi duniani, na pia wamefanikiwa katika maeneo mengi hasa ya teknolojia ya utengenezaji wa silaha za kisasa”, alisema Mbunge huyo.
  Alisema wakati Israel imeweza kukabiliana na changamoto ya kuwa na ardhi isiyofaa kwa kilimo (jangwa), vijiji katika mikoa ya Tanzania inayozunguka Ziwa Victoria ambalo ni kubwa kuliko yote barani Afrika, havina maji na wananchi wa vijiji hivyo wanateseka kwa ukosefu wa maji salama na ya uhakika.
  “Hapa ninachomaanisha ni kwamba si kwamba vitu vingi haviwezekani; bali ni suala la mitazamo yetu na vipaumbele vyetu kama Taifa na kuwepo kwa fikra hasi miongoni mwa wananchi wenyewe na viongozi”, alisema.
  Akitoa mfano, Lema alieleza kuwa katika mji wa Arusha pekee kwa siku moja wakazi wanakunywa pombe (bia) za Sh. milioni 242, kwa mujibu wa takwimu za kampuni za bia nchini. Aidha, kati ya mwaka 2005-2010 vikao vya harusi, kipaimara na ubarikio viligharimu mabilioni ya fedha ambazo zingeweza kujenga hata chuo kikuu.
  “Kwa hiyo, ukichunguza kwa makini utagundua kuwa tatizo la Watanzania si fedha bali vipaumbele, na fikra chanya za kutaka kuleta mabadiliko katika jamii yetu. Tatizo la msingi linaanzia kwa wananchi wenyewe kabla kuwafikia viongozi wa serikali”, alisema Lema; huku akishangiliwa na watu.
  “Fedha zinazotumika kwa starehe hapa nchini katika siku za mwisho wa juma ni nyingi sana na asilimia 10 tu ya fedha hizo zingeelekezwa katika matumizi ya msingi ya binadamu, basi, kusingelikuwa na watoto wanaoshindwa kwenda shule kutokana na ukosefu wa ada na mambo mengne madogo madogo…..hapa simaanishi watu wasifanye starehe zao, lakini ila tuwakumbuke makundi yenye mahitaji katika jamii yetu”, alisema.
  Mbunge huyo alisema kazi ya kwanza ya taasisi hiyo ya ArDf ni kutafsiri kwa vitendo na kubadilisha mtazamo wa wananchi wa Arusha kuwa chanya katika mambo ya msingi ya maendeleo yao kwa kuwaunganisha na kuwashirikisha katika mipango ya maendeleo.
  Alisema baada ya kufanikiwa kuanzisha mradi huo wa kuwasomesha bure watoto 400 kutoka familia ambazo hazina uwezo kifedha, sasa taasisi hiyo itaelekeza nguvu zake katika ujenzi wa hospitali ya watoto wadogo na wanawake wajawazito na wanachosubiri ni kupata eneo la ekari tano kutoka kwa mmoja wa wafadhili ili ujenzi huo uanze.
  “Tayari tumepata wafadhili watakaotusadia fedha na utaalamu kujenga hospitali ya kisasa kwa ajili ya watoto na wajawazito tu, lakini pia wananchi wa Arusha watapaswa kuchangia na utaratibu utakaotumika ni sawa na huu tuliotumia kupata fedha za kuwasomesha wanafunzi hawa”, alisema.
  “Mimi kama Mbunge nitasismamia utekelezaji wa miradi yote niliyoahidi wakati nawaomba kura wananchi wa jimbo la Arusha, na kwa pamoja tutabadilisha sura ya mji wetu huu ili uwe mji wa mfano hapa nchini kwa kubadilisha miundombinu yake”, alisema Lema.
  Mbunge huyo alitoa wito kwa wananchi wenye nia nje kuendelea kutoa misaada ya hali na mali kwa taasisi hiyo ambayo haina malengo ya kisiasa na kuongeza kuwa viongozi wa serikali wanapaswa kutenda haki kwa kutenganisha siasa na kazi za serikali ili kutatua matatizo ya wananchi.
  Awali Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya ArDF, Elfuraha Mtowe, alieleza kuwa mpango wa kuwasomesha wanafunzi hao ulibuniwa na kufanikiwa baada ya taasisi yake kufanya harambee maalumu ya kuchangisha fedha ili kufanikisha mpango wa elimu kwa wanafunzi hao 400.
  “Lengo letu ilikuwa ni kuwasadia watoto 1000 lakini tulisambaza fomu kupitia watendaji wa serikali katika kata za Manispaa ya Arusha na fomu zilizorudishwa ni 417 tu kati ya fomu 1000….na hao tumewafanyia utafiti wa kutosha na ni watoto kutoka familia maskini zisizo na uwezo na watasoma bure kwa kulipiwa gharama zote za masomo yao katika shule 22 za kata ambako wanasoma”, alisema.
  Mtowe alisema msaada huo utakuwa ni wa ada za shule kiasi cha Shilingi 40,000 kwa mwaka na michango ya shule isiyozidi Shilingi 110,000 kwa mwaka na fedha hizo zitalipwa moja kwa moja katika shule hizo na ArDF ili wanafunzi hao waendelee na masomo yao.
  “Kwa makadirio, jumla gharama zote hizo kwa mwaka kwa idadi ya wanafunzi tulionao sasa ni Shilingi milioni 60 . Fedha hizo zinatokana na michango ya hiari kutoka kwa wafanyabiashara, taasisi na makampuni ya watu binafsi yaliyopo jimbo la Arusha Mjini”, alisema Mwenyekiti huyo.
  “Sisi ArDF tutafuatilia kwa makini maendeleo ya wanafunzi hao katika shule zote hizo wanazosoma lakini mipango iko mbioni kupata waalimu wa kujitolea kutoka nchi za Canada na Uingereza ambao tutawatawanya katika shule hizo kutokana shule nyingi za kata kukosa waalimu wa kutosha”, alisema.
  Naye Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Amani Golugwa, alisema ili michango hiyo ya kuendesha taasisi hiyo iwe endelevu, wamebuni masanduku maalumu ambayo yatawekwa katika maeneo mbalimbali ya burudani na huduma za kijamii kama baa maarufu, mahoteli makubwa, na maeneo ya michezo ili watu wachangie kiasi kidogo cha fedha kinachobaki katika matumizi yao. “Tunakadiria kupata kiasi cha Shilingi milioni 20 kila mwezi kutoka katika makusanyo ya masunduku hayo na fedha hizo ndizo zitakazotumika kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo ya jamii yetu tukijumuisha na fedha za wafadhili wa ndani na nje”, alisema Golugwa.
  Mmoja wa wazazi aliyepata fursa ya kuzungumza na Raia Mwema katika hafla hiyo, ni Mwanaidi Hussein - mkazi wa Sombetini ambaye mtoto wake, Hussein Juma, anayesoma kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Lemara amepata ufadhili wa masomo wa taasisi hiyo.
  Mama huyo alieleza kuwa hana mume na ana watoto watano wanaomtegemea ambao watatu bado wako shule ya msingi na amekuwa akipata taabu kukamilisha mahitaji ya mtoto wake anayesoma kidato cha tatu kwa muda wote. Alisema kuna kuna wakati hulazimika kuacha shule kutokana na kushindwa kulipa michango wanayodaiwa shuleni.
  “Nashukuru nimepata msaada huu, na sasa nina imani kuwa mwanangu atamaliza kidato cha nne lakini kwa muda mrefu nimehangaika naye sana. Kuna wakati alikuwa anakaa nyumbani bila shule kwa zaidi ya mwezi mmoja kutokana na mimi kushindwa kupata fedha za kulipia michango anayodaiwa shuleni”, alisema mama huyo.
  Wachunguzi wa mambo wanaeleza kuwa pamoja na mipango mizuri ya maendeleo inayobuniwa na Mbunge Lema na wenzake, mipango hiyo inaweza kushindwa kuleta tija kutokana na uhasama uliopo baina ya CHADEMA na CCM hali ambayo iliwahi pia kumkuta aliyekuwa Mbunge wa Karatu, Dk.Wilbroad Slaa ambaye pia mipango yake mingi ya maendeleo ilikwamishwa na watendaji wa serikali ya CCM.
  [​IMG]
   
 2. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  yataka moyo kusoma hapo
   
 3. M

  Marytina JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  acha uvivu mh speaker
   
 4. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Join Date : 7th June 2011
  Posts : 8
  Thanks: 0Thanked 0 Times in 0 Posts

  Rep Power : 0
   
 5. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  hapo vipi,nipe record sasa
   
 6. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #6
  Jun 8, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  nimekugongea thanks na wewe nipe record
   
 7. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #7
  Jun 8, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Nakuunga mkono. Tunatakiwa tuwe tuna summarize ili wengi wasome. Likiwa reeeefu namna hii linatia uvivu. Huenda kuna hoja ndani yake lakini nami nimepata uvivu kulisoma
   
 8. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #8
  Jun 8, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Jana!!! Sijasoma labda ni vijana wetu toka Chamani
   
 9. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #9
  Jun 8, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0

  Posible,ila watch out
   
 10. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #10
  Jun 8, 2011
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mie nimeitolea uvivu mikaisoma. Inasikitisha viongozi wa serikali kuwa na mawazo mgando kiasi hicho! Tena nilitegemea huyo RC angekuwa mbele kwenye suala kama hilo maana ni msomi (kama bado ana elimu na si vyeti).
  BRAVO HON. LEMA!
   
Loading...