Hivi mnafahamu kwamba ardhi ya Tanzania kwenye kilimo inatumika kwa asilimia 15 tu? Tunakwenda wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi mnafahamu kwamba ardhi ya Tanzania kwenye kilimo inatumika kwa asilimia 15 tu? Tunakwenda wapi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Aki The Great, Aug 31, 2012.

 1. A

  Aki The Great Member

  #1
  Aug 31, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wadau nimeona nipost thread yangu hii ili tuweze kuwa na uwanja mpana zaidi wa kujadili mambo kadhaa ya nchi yetu hasa suala la Kilimo na uchumi wa nchi yetu. Ninapata shida sana baada ya kubaini kwamba tumekuwa na matumizi hafifu sana ya ardhi yetu kwanye uzalishaji wa chakula hasa mahindi na mpungu.

  Ni aslimia 15 ya ardhi ndiyo imekuwa ikitumika katika uzalishaji wa mazao yote ya chakula na biashara. Katika asilimia hiyo 15 ni asilimia 3-5 tu ya kilimo hapa nchini ndiyo inatumia kilimo cha umwagiliaji.

  Je kama taifa tunao usalama wa kutosha wa chakula kwa taifa? Pamoja na kuzalisha kwenye eneo dogo hivyo kilimo kimechangia asilimia 24-26 ya GDP. Jadili
   
 2. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #2
  Aug 31, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  wamekuja wawekezaji kutoka brazili watu wanalalamika
  sasa sijui hayo mashamba yaliokaa bila kilimo yana faida gani
  wawekezaji wawe wa ndani au nje watasaidia sana kupunguza tatizo la chakula
  na pia viwanda vya ndani kama bakhresa na azania wataaha kuagiza nfaka nje
  hata TBL pia waulize wanatoa nhano wapi.
   
 3. k

  kijereshi JF-Expert Member

  #3
  Aug 31, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 257
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Lowasa alishasema elimu kwanza ndio kilimo kifuate ranch zote tulishauza vyuo vya utafiti na kilimo viko hoi bin taaban
   
 4. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #4
  Aug 31, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,262
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  tuna ardhi ya kutosha na kilimo cha mashamba makubwa ndiyo yatakayoinua uchumi wetu.
   
 5. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #5
  Aug 31, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,849
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  Niko pamoja na LOWASSA, huwezi kuanzisha kilimo cha kisasa bila kutoa elimu na namna ya kutunza mazao na kutumia mbegu bora.elimu unaitoa kupitia mikutano, makongamano na vipeperushi baada ya hapo ndiyo kilimo.
  Lakini mimi nasema unaweza kuanza kutoa elimu huku ukiandaa mazingira mazuri kama vile serikali kuanza kuchimba mabwawa kwa ajili ya umwagiliaji.Kilimo cha kutegemea mvua unaweza kulima ekari 1000 na ukavuna gunia 500 tu kwa maana nyingine unavuna nusu gunia kwa ekari hii usishangae kwani mvua zisiponyesha mazao hayakui na kutoa mazao kwa kiwango.hongera lowassa achana na kina lipumba wasio jua kilimo eti Prof.!!!!!!!!!!!!!
   
 6. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #6
  Aug 31, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Serikali ccm ilitumia nafasi ya slogan Yao ya uwongo "kilimo kwanza" kununulia v8 Kama wanavyotumia sensa kupitishia hela zao
   
 7. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #7
  Aug 31, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  -ardhi kubwa ni hifadhi ya taifa
  -kilimo cha umwagiliaji ni porojo za kisiasa, ukijaribu kuweka irrigation system watakukalia kooni kwa kigezo cha uharibifu wa mazingira/vyanzo vya maji

  - taifa lenye akili linaangalia future ya vizazi vijavyo, leo hii tz tupo kama 45m na ajira ni mbinde kwa vijana na kwa hali hii kufikia 2020 swala ajira litakuwa kama nigeria (hakuna ajira hata kama una phd), ! kwahiyo hawa vijana watalzimika tu kwenda kulima watake wasitake! au vinginevyo tuuze ardhi tuongeze idadi ya vibaka wasomi, mahousegirl/boy nchi za kiarabu na vyangudoa ndani na nje ya nchi kama ilivyo kenya, nigeria, ethiopia, phillipines, india etc.

  imagine population yetu ikifikia watu milioni 70 na ardhi kubwa ipo chini ya mwekezaji kwa miaka 99!
  Ubinafsishaji wa ardhi hapana.
   
 8. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #8
  Sep 1, 2012
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Tunatatizo la "haraka bila sababu" hivi kwani hiyo ardhi ikikaa mpaka watanzania wenyewe waipatie matumizi kuna tatizo gani? Tunataka kuishi kama vile mwisho wa maisha ya watanzania wote ni kesho, hii sio sahihi.

  Uwekezaji wowote mkubwa ufanywe na serikali na sio wawekezaji wa nje kwani kwa kufanya hivyo ikitokea kwamba wananchi hawana ardhi wakati serikali inafanya miradi mbalimbali ni rahisi ku review sera na kuangalia jinsi ya kuwasaidia wananchi. Tofauti na ikitokea kwamba ardhi kubwa inamilikiwa na wageni (wawekezaji uchwara) mwisho wa siku tutakuwa tunazungumzia vita na si vinginevyo kwani huo utakuwa ni wakati ambao bubu atake asitake ataongea!

  Badala ya kushabikia uwekezaji tujiulize kwa % kwamba uwekezaji ambao tayari kama nchi tumeishaingia tumefaidika kwa kiasi gani? Kwetu sasa sio wakati wa kukurupuka.

  Tumegenisha hadi nyumba za serikali ambazo walikuwa wanakaa watumishi mbalimbali wa serikali wakiwemo majaji na watumishi wengine, tujiulize sasa serikali inaingia gharama kiasi gani kuwahifadhi watumishi hawa hasa wanapohama vituo vyao vya kazi vya awali, wizi mtupu!
   
 9. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #9
  Sep 1, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,112
  Likes Received: 1,499
  Trophy Points: 280
  sioni tatizo kwa kuwa na ardhi kubwa ambayo haijatumika kwani tunaweza kurudia makosa kama ambayo tulifanya ya kukimbilia kuchoimba madini wakati tulikuwa hatujaandaa sera wala wataalamu matokeo yake tunakuza uchunmi wa nchi nyingine na kuendelea kuporwa rasilimali.Tuna vyuo vya kilimo vya kutosha ambavyo vingi vilianzishwa na serikali ya awamu ya kwanza lakini tuna tatizo la kushindwa kupanga mipango ya matumizi sahihi ya ardhi kwani tumekuwa tukishuhudia mapigano ya wakulima na wafugaji kugombea ardhi.Inabidi tujue ni ardhi gani itengwe kwa kilimo na ipi kwa ufugaji.
  Pia bado tunaendelea kuongezeka lazima tuwe na ardhi ya kutosheleza kwa kizazi kinachokuja tusiwe tunajifikiria sisi tuliopo matokeo yake tutazua matatizo makubwa kwa kizazi kinachokuja.Tutafanya kizazi hicho kiwe watumwa katika nchi yao.
   
 10. Ipan

  Ipan Member

  #10
  Sep 1, 2012
  Joined: Aug 15, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kabisa....mimi niko USA na watanzania wenzangu tulioko huku tumeona jinsi gani wamarekani wenzetu wanavyojari kilimo. Saa hizi mazungumzo mengi na wenzangu huwa tunafikiria ni jinsi gani tuweze kurudi nyumbani na kuingia katika suala la kilimo. Natafuta shamba zaidi ya heka 10 ambalo nitanunua ili nianze kufanya kilimo cha umwagiliaji huko maeneo ya Lake Manyara.
  Tuna ardhi safi yenye rutuba nyingi.....naomba kama una information yoyote ile changia tafadhari na tuwasiliane.
   
 11. murugalama

  murugalama JF-Expert Member

  #11
  Sep 2, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 228
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Haraka hii tuliyonayo ni ya nini? Kwa sasa watanzania hatuhitaji wawekezaji kwy sekta ya kilimo, km tukipata ewezeshaji tutatoa ziada ya kutosha.
   
 12. m

  mzeelapa JF-Expert Member

  #12
  Sep 3, 2012
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 1,034
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Mawazo yote yaliyotolewa naafikiana nayo, kinachoniuma zaidi kwa nini ardhi ambayo wakulima wadogowadogo wanaitumia kwa kilimo badala ya kupewa mbinu za kisasa za kilimo bora, wananyang"anywa na Serikali na kupewa wawekezaji (uchwara) wakati ardhi kubwa ipo tu! Kulikuwa na sababu gani kuwahamisha wakulima wa Rufiji wakati ardhi imejaa. Wakati wa ukoloni wakulima walowezi walikuja kufyeka mapori (virgin land) na ndio mashamba haya tunayoyaona ya Tumbaku, mkonge nk. lakini hawa matapeli wanaokuja sasa wananyang"anya maeneo yaliyokuwa tayari mashamba. Serikali iwe macho kwa kuangalia mfano wa Zimbabwe.
   
 13. Mwanahisa

  Mwanahisa JF-Expert Member

  #13
  Sep 3, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 1,397
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hivi tuna sheria ya Aridhi Tanzania? Je ni ya mwaka gani kama ipo, na imeandikwa kwa lugha gani? Nisaidiwe hapa jamani.
   
Loading...