Hivi Mmiliki Wa WhatsApp, Instagram na Facebook anapataje Fedha Mimi nikitumia Mitandao yake?

Usibishe Mkuu bundle unazotumia kuna certain percentage ambayo wale host Kama Voda Au telia au tigo au Du wanazifidia kwa namna fulan kwa either blog au web unayo blowse but siyo kubwa! Hawa wanategemea sana matangazo n kupakua app zao
Hakuna ukweli juu ya hili ni uongo kabisa.
 
Kuna watu wanalipia ili kutangaza kazi zao Harafu wewe unakua kama targeted one.
Pia vipakuliwa huko katika duka la Google nako wanafaidi sana.
Kiswahili kigumu jamani! Imenibidi niipeleke kwenda kiingereza hiyo sentensi yako ya mwisho ndio nimeelewa.
 
Kiswahili kigumu jamani! Imenibidi niipeleke kwenda kiingereza hiyo sentensi yako ya mwisho ndio nimeelewa.
Dah Harafu hicho ni kiswahili rahisi sana sasa hata mimi huku kuna viswahili wanabonga hata sivielewi
 
View attachment 1963390
Ukiona neno “sponsored” facebook . Ujue hilo ni tangazo na limelipiwa.
Wanapata fwedha kupitia matangazo ndiyo maana wana huduma zao za matangazo hasa Facebook & Instagram, Na hata WhatsApp wameipenyeza.

Wanachokifanya Facebook kujipatia kipato hakina tofauti sana na wanachokifanya Google kupitia ads program zake za Google Adsense na Admob. Hii mitandao unapoweka apps zao kwenye kifaa chako inasoma system infos muhimu kama contact, calls, location history, imei namba na IP address ndiyo maana unashangaa unatembelea Facebook ila unaletewa matangazo ya Vodacom Tanzania, Pepsi au Coca-Cola za makampuni ya TZ ilihali hizi kampuni ziko worldwide, au unaona tangazo la TCRA kuhusu usajili wa alama za vidole, Simple tu apps zao wamewapa location ya target ndiyo maana unaletewa matangazo ambayo yanakuhusu kwa namna 1 ama nyingine na ya lugha yako kabisa.


Kwa kukuongezea tu, Unapotumia mtandao wa Facebook bure kupitia mtoa huduma flani hapa nchini au nchini nyingine basi huyo mtoa huduma analipwa na Facebook naye, Kitaalamu Facebook inawekwa katika mfumo wa CDN (Content Delivery Network) kwa wale wataalamu wa internet hii kwetu tunaita ni Bug Host (Yaani unaweza ku configurate na kutumia free internet kupitia huu udhaifu wa facebook kutumika kama host ) ilkua zamani lakini asaiv hakuna haya mambo tena yashagazimwa. Yaani hizi kampuni zina ecosystem yake zinajiendesha kwa kutegemeana sana ili kila mmoja afaidike kwa namna moja ama nyingine.
 
Wakuu Kazi Iendelee

Naomba kujua kwamba Huyu Mmiliki Wa WhatsApp, Instagram na Facebook Wanapataje fedha Mimi nikitumia Ku-access Hyo Mitandao Yao?

Naomba Kujifunza Wakuu Kwa anaejua
Kwa kawaida bidhaa yoyote ukipewa bure jua bidhaa ni wewe si hiyo bidhaa
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom