Hivi mmejiuliza Sababu za Kutenguliwa DC wa Sumbawanga Jane Nyamsenda? Inachekesha sana!

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,562
217,903
Wengi tumesikia na kusoma taarifa za Dada Jane Nyamsenda Kuondolewa kwenye Cheo cha Ukuu wa Wilaya, Taarifa hiyo imetolewa na Ikulu ambayo ndio Mamlaka yake ya Uteuzi, na baadaye tukaridhika tu kwamba ndugu Jane Nyamsenda ametumbuliwa, tukaona ni kawaida kama zilivyo kawaida zingine, tukanyamaza!

Bali mimi nikajiongeza kidogo ili kufahamu kiundani, kisa cha dada huyo mrembo kutumbuliwa haraka na ghafla namna hiyo, niliyoyaona yamenistaajabisha na kunichekesha sana!

Siku ya Wanawake ya Dunia, DC aliandaa kama igizo hivi, sijui ni la utayari wa vyombo vya dola au sijui ni kuonyesha uwezo wa Wanawake, haieleweki hasa lengo la jambo lile, basi bhana Wananchi wakiwa wamekusanyika uwanjani msafara wa Mkuu wa Wilaya ambaye bila shaka alikuwa ndio Mgeni Rasmi Ukaingia uwanjani, ukiwa umesheheni askari kibao wenye Mabunduki ya kivita, wakashuka kikakamavu wakaizunguka gari ya DC, mpambe akaja akafungua mlango, DC akatoka akiwa nadhifu huku akitilia kilemba cha kichwa kama kile anachovaa Mh Rais.

Msafara wake ukaanza kusogea kwa miguu akiwa katikati lundo la Maaskari wenye mitutu mizito, sasa baadaye mara askari wake wakaanza kurusha risasi kuelekea mbele yao huku DC akinyakuliwa na kurejeshwa ndani ya gari kwa Style ya kuokoa viongozi dhidi ya maadui na hatimaye gari kuondoka kwa kasi kubwa!

Baada ya kuona jambo hili nimegundua kwamba DC Jane Nyamsenda ni mkuu wa Wilaya wa aina ya Makonda, Sabaya na Jerry Muro, anaonekana anapenda kujimwambafy kupita maelezo! Yaani kwake Ukuu wa Wilaya ni kama Ukuu wa Nchi, Tukio aliloliandaa halikuwa na uhusiano wowote na siku ya Wanawake, Sijui ni nani alimdanganya? Ni Aibu sana kwake, kwa Wazazi wake na kwa waliomteua.

Natoa wito kwa mamlaka ya Uteuzi kwamba, pamoja na ukweli kwamba majukumu ya Mkuu wa Wilaya ya Kufungua Makongamano ya UKIMWI, Kupokea Viongozi wa Kotaifa, Kusimamia Mbio za Mwenge na Kusaidia CCM kwenye Uchaguzi ni mepesi kuliko hata majukumu ya mmachinga au mama lishe, lakini bado kuna haja ya kuteua watu sahihi wanaostahili, haya mambo ya kuokota watu UVCCM, watoto, wajomba, mashemeji wa viongozi, walioshindwa ubunge na Chawa wa viongozi yataliaibisha Taifa, tuwe na mfumo ulio wazi wa kuchagua hawa watu au Tufute hivi vyeo ili kuiheshimisha nchi.

 
Wengi tumesikia na kusoma taarifa za Dada Jane Nyamsenda Kuondolewa kwenye Cheo cha Ukuu wa Wilaya, Taarifa hiyo imetolewa na Ikulu ambayo ndio Mamlaka yake ya Uteuzi na baadaye tukaridhika tu kwamba ndugu Jane Nyamsenda ametumbuliwa, tukaona ni kawaida kama zilivyo kawaida zingine, tukanyamaza!

Bali mimi nikajiongeza kidogo ili kufahamu kiundani , kisa cha dada huyo mrembo kutumbuliwa haraka na ghafla namna hiyo, niliyoyaona yamenistaajabisha na kunichekesha sana!

Siku ya Wanawake ya Dunia , Mh DC aliandaa kama igizo hivi , sijui ni la utayari wa vyombo vya dola au sijui ni kuonyesha uwezo wa Wanawake , haieleweki hasa lengo la jambo lile , basi bhana Wananchi wakiwa wamekusanyika uwanjani msafara wa Mkuu wa Wilaya ambaye bila shaka alikuwa ndio Mgeni Rasmi Ukaingia uwanjani, ukiwa umesheheni askari kibao wenye Mabunduki ya kivita , wakashuka kikakamavu wakaizunguka gari ya DC , mpambe akaja akafungua mlango , DC akatoka akiwa nadhifu huku akitilia kilemba cha kichwa kama kile anachovaa Mh Rais.

Msafara wake ukaanza kusogea kwa miguu akiwa katikati lundo la Maaskari wenye mitutu mizito , sasa baadaye mara askari wake wakaanza kurusha risasi kuelekea mbele yao huku DC akinyakuliwa na kurejeshwa ndani ya gari kwa Style ya kuokoa viongozi dhidi ya maadui na hatimaye gari kuondoka kwa kasi kubwa !

Baada ya kuona jambo hili nimegundua kwamba DC Jane Nyamsenda ni mkuu wa Wilaya wa aina ya Makonda , Sabaya na Jerry Muro , anaonekana anapenda kujimwambafy kupita maelezo ! yaani kwake Ukuu wa Wilaya ni kama Ukuu wa Nchi , Tulkio aliloliandaa halikuwa na uhusiano wowote na siku ya Wanawake , Sijui ni nani alimdanganya? ni Aibu sana kwake, kwa Wazazi wake na kwa waliomteua.
Labda ni maono yake.
 
Duuh, Haikua poa kuandaa igizo la kuonyesha Kiongozi Mwanamke anafanyiwa jaribio la kupigwa.

Ni mchezo mbaya sana kwani unaweza ukawapa watu ujasiri Fulani Kwa kuona kuwa mbona walinzi wale walikua dhaifu hata mtu akiwa na upanga anaweza akawafyeka wote na kufanya misheni yake?

Kwa nchi hizi zenye wapigania madaraka michezo kama Ile haifai.

Inaweza ikatoa mwanya Kwa Wahalifu kufanya maandalizi ya kukabiliana na kikosi hicho Cha wamama waigizaj!!
 
Jane Chacha, amechacha! Any ways, siwezi kumzungumzia vibaya. Sikuwahi kuuona ubaya wake tangu alikuwa room mate wa class mate wangu pale UD.
Nilifahamiana naye kwa kuwa 'ilikuwa haipiti siku' bila mimi kwenda room kwao kwa vile room mate wake alikuwa best angu.
Baada ya kupotezana naye, nilikutana naye pale Ubungo akaniambia kuwa anasoma PhD.
Mara ya mwisho kuonana naye, nilienda kumsalimia kule Tabata Kimanga. Alinipokea stendi kwa heshima na akanipokea kihand bag changu kwa heshima.
Huwa nasema, heshima niliyoipata kwa huyu mwanamke sijawahi kuopata kwa mwanamke mwingine yoyote hapa Duniani. Ni mwanamke machachari kama mnavyowafahamu watu wa mkoa wa Mara ila naamini ni ujana utakuwa umemponza.
Magu aliwahi kusema kuwa atakuwa anateua vijana na kwa vile vijana damu bado zinachemka basi tuwavumilie... pale wanapochemsha.
 
Wengi tumesikia na kusoma taarifa za Dada Jane Nyamsenda Kuondolewa kwenye Cheo cha Ukuu wa Wilaya , Taarifa hiyo imetolewa na Ikulu ambayo ndio Mamlaka yake ya Uteuzi , na baadaye tukaridhika tu kwamba ndugu Jane Nyamsenda ametumbuliwa , tukaona ni kawaida kama zilivyo kawaida zingine , tukanyamaza !

Bali mimi nikajiongeza kidogo ili kufahamu kiundani , kisa cha dada huyo mrembo kutumbuliwa haraka na ghafla namna hiyo , niliyoyaona yamenistaajabisha na kunichekesha sana !

Siku ya Wanawake ya Dunia , Mh DC aliandaa kama igizo hivi , sijui ni la utayari wa vyombo vya dola au sijui ni kuonyesha uwezo wa Wanawake , haieleweki hasa lengo la jambo lile , basi bhana Wananchi wakiwa wamekusanyika uwanjani msafara wa Mkuu wa Wilaya ambaye bila shaka alikuwa ndio Mgeni Rasmi Ukaingia uwanjani , ukiwa umesheheni askari kibao wenye Mabunduki ya kivita , wakashuka kikakamavu wakaizunguka gari ya DC , mpambe akaja akafungua mlango , DC akatoka akiwa nadhifu huku akitilia kilemba cha kichwa kama kile anachovaa Mh Rais .

Msafara wake ukaanza kusogea kwa miguu akiwa katikati lundo la Maaskari wenye mitutu mizito , sasa baadaye mara askari wake wakaanza kurusha risasi kuelekea mbele yao huku DC akinyakuliwa na kurejeshwa ndani ya gari kwa Style ya kuokoa viongozi dhidi ya maadui na hatimaye gari kuondoka kwa kasi kubwa !

Baada ya kuona jambo hili nimegundua kwamba DC Jane Nyamsenda ni mkuu wa Wilaya wa aina ya Makonda , Sabaya na Jerry Muro , anaonekana anapenda kujimwambafy kupita maelezo ! yaani kwake Ukuu wa Wilaya ni kama Ukuu wa Nchi , Tukio aliloliandaa halikuwa na uhusiano wowote na siku ya Wanawake , Sijui ni nani alimdanganya ? ni Aibu sana kwake , kwa Wazazi wake na kwa waliomteua .

Natoa wito kwa mamlaka ya Uteuzi kwamba Pamoja na ukweli kwamba majukumu ya Mkuu wa Wilaya ya KUFUNGUA MAKONGAMANO YA UKIMWI , KUPOKEA VIONGOZI WA KITAIFA , KUSIMAMIA MBIO ZA MWENGE NA KUSAIDIA CCM KWENYE UCHAGUZI ni mepesi kuliko hata majukumu ya mmachinga au mama lishe , lakini bado kuna haja ya kuteua watu sahihi wanaostahili , haya mambo ya kuokota watu UVCCM , watoto , wajomba , mashemeji wa viongozi , walioshindwa ubunge na Chawa wa viongozi yataliaibisha Taifa , tuwe na mfumo ulio wazi wa kuchagua hawa watu au Tufute hivi vyeo ili kuiheshimisha nchi .
Si kweli, ile video imekuwa edited na waliokuwapo uwanjani wanasema hayo hayakutokea. Kutakuwapo na sababu nyingine tu, lakini kinachoonekana kwenye ile video hakikuwepo kabisa uwanjani
 
Back
Top Bottom