Hivi mimba ni kweli zinachagua vyakula au ni kujifanyisha?

manSniper

JF-Expert Member
Sep 9, 2015
814
679
Nashangaa sana kusumbuliwa eti mimba leo inataka chips kuku, mara baga, mara Malta yaani inakua kero sana.Mwanamke akiwa katika hali hii mara hataki uende kazini daa! Mara inataka kila saa ugegede tu yaani daa! Hivi ni kweli au ni kujifanyisha tuu? Mbona mimba isipende ugali maharagwe?
 
Mkuuu in kweli bora wako anachangua chakula mm wng alikuwa anataka niwe napika chakula mm bila kupika mm hawezi kula kabs
 
Naunga mkono hoja. Wanawake wa ulaya wao huwa wanataka nini wakiwa wajawazito maana hayo machipsi si wanakulaga siku za kawaida?
 
Kanunue read bull za bei ya jumla mkuu na karanga gunia weka ndani, huyo atakua anajitoa ufahamu mara kwa mara so akiona hivo ufahamu utakua standby
 
Mama yangu uwaanasema "kama mimba ni ugonjwa wagumba wasingekuwa wanaenda kwa daktari ili washike mimba" soo mwanamke akishika mimba then aniletee hizo swagauwa namuacha tuone mwisho wake.
 
Heheheheeee ni mimba ya mchepuko? Polee dawa ni kuikubali hali na kuendana nayo kadri na jinsi inavyokupelekesha.

Akishazaliwa bado mtoto atasingiziwa mengi tuu hehehehee
 
Laiti kungekua na uwezekano wa kuwahamishia japo kwa siku1 tu mshinde nayo
isingekuwa shida nimewauliza wanawake wengi wenye mimba huwa wanasema wapo kawaida tu wala hawaoni uzito! izo nyingine mbwembwe tu tena chunguza wengi wanaodai misos mikubwa ndo wale wakina fatuma mkude wa uswahilini
 
Naunga mkono hoja. Wanawake wa ulaya wao huwa wanataka nini wakiwa wajawazito maana hayo machipsi si wanakulaga siku za kawaida?
Mara nyingi mkate wa kuoka (toast) tena bila siagi wala jam kavu kavu.
 
Ni changes of hormone, lakini wale wanaopata mimba bado wako nyumbani hawajaolewa au wako shule, wanatwanga kila kitu. Ugali maharage twende, ugali dagaa mwao, wazazi wakishtuka mtoto ana mimba ni miezi mitano hukooo. Ni maajabu ya Muumba mwenyewe.
 
Mimba zinasumbua sana miez minne ya mwanzo kwa walio wengi. si vyakula tu bali hata tabia. Ni vema umvumilie mkeo maana ukimchanganya utakuwa umemtwika mizigo miwili. Msongo wa mawazo nao sio mzur kwa mjamzito.
 
Back
Top Bottom