Hivi mikutano ya kisiasa.

kinguo

JF-Expert Member
May 27, 2016
440
318
Wanajamvi naomba kuleta mada tuijadili kwa kina. Hivi Naibu waziri ww Nishati na madini Mendrad, Mbunge wa Gairo Shabiby. Hivi hii mikutano yanayofanya si ya kisiasa kweli au mikutano ni ile inayohusisha Wapinzani kama kina Lema , Mbowe, Mbatia , Zitto tu ndio ya kisiasa naomba nijulishwe ili nisiwe na munkari wa kuuliza. Maana tunako kwenda sio kuzuri kama watu wanavyofikiria. Maana haiwezekani wengine wafanye mikutano wengine wanyimwe. Jeshi letu la Polisi naliomba lisijishushie heshima kwa upendeleo wanao uonyesha. Matusi toka Lumumba buku saba yanaruhusiwa. Nawasilisha tujadili kwa kuisaidia Tanzania sio kwa ajili yetu ni kwa vizazi vijavyo.
 
Back
Top Bottom