Hivi Michuzi ni Mtumwa wa CCM??

Jadi

JF-Expert Member
Aug 2, 2011
1,494
860
Jamani hapa JF naomba kujua nisije kosea, nimekuwa naingia kwenye blog ya Michuzi na kukuta mapicha kibao ya CCM, mara kurudisha kadi za upinzani, mara kampeni za Nape, Makala n.k, au CCM ndo wafadhili wake??yani ukikosea kufungua page yake ujue data kibao zimepotea.

Tusaidieni sie wenye uchungu na hawa wanaoshabikia mambo ya hovyo, muda ule kuna mgomo mkali wa madr, yeye anatuletea mara makamu wa raisi afungua tawi, mara waziri mkuu anaongoza maandamano ya wanaCCM, kweli I wish nisifungue kabisa huko, ingawa kuna habari chache twasoma huko, namshauri abalance matukio, upinzani vs magamba
 
yule ni mpiga picha wa jk kwa hyo automatic lazima awe anauccm ndani yake...
 
Ni yakwake, ana uhuru ya kufanya/kupost vile apendavyo.
 
Mkuu pole sana yaani bado unapoteza muda wako kuangalia blog ya michuzi? Walau Blog ya michuzi ilikuwa blog ya jamii kabla ya 2010. Lakini toka hapo na baada ya uchaguzi imekuwa ni blog ya CCM sio ya jamii. Kama unataka kupata habari za Magamba basi huko ndiko kwenyewe lakini kama unataka kupata habari zenye tija kwa taarifa huko siko. Wengine tulishaacha siku nyingi kuiangalia hiyo blog ya Magamba! Jamaa anapendelea mpaka anakera!! Shame on him!!
 
Jamani hapa JF naomba kujua nisije kosea, nimekuwa naingia kwenye blog ya Michuzi na kukuta mapicha kibao ya CCM, mara kurudisha kadi za upinzani, mara kampeni za Nape, Makala n.k, au CCM ndo wafadhili wake??yani ukikosea kufungua page yake ujue data kibao zimepotea. Tusaidieni sie wenye uchungu na hawa wanaoshabikia mambo ya hovyo, muda ule kuna mgomo mkali wa madr, yeye anatuletea mara makamu wa raisi afungua tawi, mara waziri mkuu anaongoza maandamano ya wanaCCM, kweli I wish nisifungue kabisa huko, ingawa kuna habari chache twasoma huko, namshauri abalance matukio, upinzani vs magamba

Michuzi ni mchumia tumbo, kazi ni kujikomba kwa watu
 
ni mpiga picha wa raisi huyo so raisi ni ccm naye bila shaka ili aendelee na kibarua lazima awe hivyo me nilishangaa ule msiba wa regia rambirambi ya jk aliiweka na ile ya chadema hakuiweka mpaka mwisho
 
CCM Ndio Kula yake.
NB: Kila anayejihusisha na CCM yuko pale kwa maslahi yake binafsi.
 
Watu washamjulia M.kwere..........angalia hapa:

1) Salva aliwajeruhi wapinzani wa Kikwete mwaka 2005, wakina Salim A. Salim,.........Mtanzania na Rai
2) Clouds wakawa wanampa shavu, wanamsifia, wakamfanyia birthday kama mtoto
3) Michuzi akajikita kwenye kwenye mapicha, akaweka mapicha ya Kikwete, ya CCM...mazuri mazuri, kama ni ya upinzani, basi itakuwa ya kuaibisha hivi or something like that!!!

Wote wamekula shavu la M.kwere.
Ukimjulia Mswahili, unampamba na misifa tu!!
 
mtu mwenye akili usifungue kabisa Bigrita kamaliza yote hata juzi chadema walipoenda ikulu kwa swala la katiba Dk slaa alimwambia JK nimekuja watu wanasema ninakukimbia,jamaaJK AKABWAGIZA AAAH SI KINA MICHUZI HAWA BWANA,kwa hiyo kajama kanajipendekeza kweli,huoni hata akaazeeki mpaka akili
 
Jamani hapa JF naomba kujua nisije kosea, nimekuwa naingia kwenye blog ya Michuzi na kukuta mapicha kibao ya CCM, mara kurudisha kadi za upinzani, mara kampeni za Nape, Makala n.k, au CCM ndo wafadhili wake??yani ukikosea kufungua page yake ujue data kibao zimepotea. Tusaidieni sie wenye uchungu na hawa wanaoshabikia mambo ya hovyo, muda ule kuna mgomo mkali wa madr, yeye anatuletea mara makamu wa raisi afungua tawi, mara waziri mkuu anaongoza maandamano ya wanaCCM, kweli I wish nisifungue kabisa huko, ingawa kuna habari chache twasoma huko, namshauri abalance matukio, upinzani vs magamba

Naungana na wewe asilimia 200, mimi nilikuwa ni mmoja wa wanachama wazuri wa blog ya michuzi. Lakini ilipofika wakati wa uchaguzi wa mwaka jana aliegemea sana kwenye habari za CCM. Sasa kwa kuwa mimi ni mtu asikuwa na mrengo wa kisiasa bali mtu wa kufuata fikra pevu nikaamua tangu siku zile kuachana na blog ya michuzi.

Anyway, inaelekewa jamaa anapata kula yake kutoka kwa wakuu wa CCM. Hivyo analinda ugali na mboga yake. Ni miongoni mwa wachumia tumbo tulikuwa nao hapa Tanzania. Hata kama 2+2=4 lakini yuko tayari kusema 2+2=6 ilimradi tu wakubwa wanamhakikishia ugali na mboga wanataka aseme hivyo.

True kabisa michuzi blog b4 2010 ilikuwa nzuri sana wakati wa kampeni na baada ya uchaguzi blog ikawa total ya ccm! Ukipost chochote against ccm michuzi anapotezea. Anyway ndiyo anakopatia kula yake no way.
 
kweli yanibidi nisticky huku huku JF, anaboa sana, anaweka mapicha mpaka kero, sasa nimejua, asanteni sana wadu
 
Hawezi kukwepa huo mfumo, Michuzi alikuwa choka. Sasa kama hao jamaa wanamtoa, kwanini asijipendekeze kwao? Nani anataka uzalendo wa kina Mandela, ule maharage wakati wenzio wanapeta uraiani? Endelea Michuzi, hao mabwana zako ikitokea wameshindwa utatuambia kuwa "Jamani samahani nilikuwa naganga njaa tu, mimi na nyie damu damu". Utapokelewa kama mwana mpotefu uendelee na mapicha yako.
 
Tumpe uhuru ile ni blog yake kama hutaki usiende kuchungulia nani kakutuma kwake kama mnapishana mtazamo?
 
Lini uliona Tanzania Daima ikiandika habari nzuri za CCM au Mwanahalisi? Ni mtazamo wao na Michuzi ni mtazamo wake na ndio demokrasia tunasema kila siku kwamba CCM inatunyima na sisi tunafanya hayo hayo.
 
Mh! Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni. Unacheki lakini matangangazo ktk blog ya Michuzi bwana! kapiga bao blogs zote na hata jf hatuoni ndani. Hivi ni kwa nini watangazaji wote wanakimbilia kule? Jibu ni kwamba wanafuiata blog yenye kusomwa na watu wengi zaidi ya zote. Je watangazaji Nao ni CCM? Tujiulize kabla ya kulaumu. Pia habari njema za CCM humu jf hazioni ndani. Ni kwa nini? The bottom line ni kwamba yeye amna uhuru wa kupenda anachotaka kama ambavyo jf ina uhuru wa kuchukia asichotaka. Mpo hapo wakubwa?
 
Back
Top Bottom