Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,480
- 30,152
Tunashuhudia "figisu figisu" nyingi sana zikiendelea katika kesi ya akina Mbowe ikifanyiwa "delaying tactics" huku kiongozi huyo Mkuu wa Chama kikuu cha upinzani nchini cha Chadema, pamoja na mbunge mwenzake Esther Matiko, wakiendelea kusota gerezani Segerea kwa kile kilichoitwa kuidharau mahakama ya Kisutu, tokea mwezi Novemba mwaka Jana, ukiwa huu ni mwezi wa pili wako mahabusu!
Tunafahamu pia kuwa mawakili wa Mbowe walipeleka hati ya dharura mahakama kuu kupinga kufutiwa dhamana kwa wateja wao, baada ya mahakama ya Kisutu kufuta dhamana ya watuhumiwa hao wawili
Tunafahamu kuwa mtu hawezi kupewa adhabu ya kifungo hapa nchini hadi mahakama itakapothibitisha pasipo shaka yoyote kuwa mtu huyo ametenda kosa la jinai
Hivi hiki kitendo cha watuhumiwa hao wawili kukaa gerezani kwa mwezi wa pili sasa tutakiitaje kama siyo kuhukumiwa "indirect" kufungwa gerezani??
Sasa inakuwaje hawa akina Mbowe "wanakomolewa" kwa kukaa mahabusu ikiwa ni mwezi wa pili sasa, wakati mahakama haijawahukumu kuwa wametenda kosa la jinai kwa tuhuma walizofunguliwa nazo mashitaka??
Au tuseme mhimili huo wa mahakama nao "umetekwa" na mhimili wa Executive, kwa kuwa tuliwahi kumsikia Mheshimiwa Rais Magufuli akitoa onyo hadharani kuwa viongozi wa Chadema wataozea jela??
Ni vyema mhimili wa mahakama ukajiosha katika kutenda haki na ukajitoa katika "kufikirika" kuwa unatumika na mhimili wa Executive katika maagizo yake
Kwani ni mhimili huo pekee ndiyo unaotambulika kuwa ndiyo unaotenda haki hapa nchini na ndiyo kimbilio la wanyonge wa nchi hii
Tunafahamu kuwa mhimili mwingine wa Bunge tayari "ushatekwa" na mhimili wa Executive na unatekeleza yale inayoagizwa.....
Itakapotokea wananchi wakakosa Imani na mhimili wa mahakama, basi ujue kama nchi tutakuwa tumefikia hatua mbaya sana na tunaomba mhimili huo wa mahakama utende haki
Mungu ibariki Tanzania