Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,480
- 30,152
Katika nchi yetu kila mwaka huwa tunakuwa na wiki moja ambayo huwa tunaiita ni wiki ya sheria nchini, ambapo tumeianza rasmi tarehe 24/1/2021 na kilele chake kitakuwa tarehe 1/2/2021.
Ninajua kumekuwa na juhudi kubwa sana toka kwenye mhimili mmoja ambao ni serikali "kuulazimisha" mhimili mwingine wa mahakama, ili waweke kipaumbele chao kwa kutafsiri sheria za nchi na kuwa katika lugha ya Kiswahili.
Ninavyojua Mimi katika utawala bora wa sheria, ni lazima kuwepo na "power separation" miongoni ya mihimili mitatu ya dola, ambayo ni "Executive, Legislature and Judiciary'
Ninashoshangaa ni kwa hapa nchini kwetu kwa mkuu mmoja wa Mhimili, ambao ni "Executive" ambapo ni Rais wa nchi, kuagiza mhimili mwingine ambao ni "Judiciary" kuwa ni "lazima" wazitafsiri sheria za mahakama zao kutoka lugha yao rasmi, ambayo ni Kiingereza na kuwa Kiswahili, kwa kile alichokiita wananchi wake wananyimwa haki zao, kwa mhimili huo kutumia lugha ya Kiingereza, ambapo kwa madai yake ni kuwa wananchi wake walio wengi, hawana ufahamu mkubwa wa lugha hiyo, hivyo wananyimwa fursa ya kupata haki yao kwenye mhimili huo wa mahakama.
Hebu tujiulize, hivi ni kwanini mhimili huo hautoi kipaumbele katika mambo ya kisheria, ambayo ndiyo kilio na kipaumbele cha wananchi wengi kwa hivi sasa?
Hebu nitoe mifano ya vipaumbele hivyo:-
1.N i kwanini nchi yetu haitoi kipaumbele kubadilisha sheria ya kutopingwa mahakamani, matokeo ya Urais, mara tu yatangazwapo na Tume ya uchaguzi wa Taifa, tukiwa ndiyo nchi pekee tunaonyima fursa hiyo ya kupeleka mahakamani malalamiko hayo katika kipande hiki cha Bara hili la Afrika?
2. Ni kwanini mahakama zetu kipindi hiki zimetumika kisiasa zaidi, kwa kuendesha kesi nyingi za "kubambika" zinazohusu uhujumu uchumi na utakatishaji pesa, kuliko wakati wowote katika serikali za awamu zilizopita?
3. Ni kwanini DPP amepewa mamlaka makubwa mno ya kuamua nani akae ndani na nani atoke awe huru, katika kile kinachoitwa "plea bargaining" katika kesi zao za "kubambika" katika utawala huu wa awamu hii ya uongozi?
Mimi nadhani hayo ndiyo ya kuyapa kipaumbele katika ubadilishaji wa sheria za mahakama zetu, kuliko hilo la kubadilisha lugha, kwa kuwa hiyo lugha ya Kiingereza ndiyo lugha rasmi ya kimahakama, na siyo kero na kilio cha wananchi wengi hapa nchini kwa hivi sasa, katika kunyimwa haki za kisheria nchini.