Hivi Mheshimiwa Chiligati anadhani Watanzania bado mabwege? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Mheshimiwa Chiligati anadhani Watanzania bado mabwege?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanahakij, Aug 19, 2009.

 1. Mwanahakij

  Mwanahakij Senior Member

  #1
  Aug 19, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu Mheshimiwa sana, kanukuliwa mambo akisema mambo mengi, yamkini, gazeti la Mwananchi la leo limenukuu kama ifuatavyo kuhusu tuhuma za ufisadi zinazomsonga Mkapa.

  “Hayo yote ni mambo mazuri, lakini bado Watanzania wanaona kuwa alichokifanya Mkapa kilikuwa ni kazi bure, jamani sisi ni watu gani tusiokuwa na shukrani yaani kila jambo kwetu ni baya, tukumbuke kuwa nchi hii ilikuwa katika hali ya kuwa mufilisi; ilikuwa haikopesheki lakini sasa tunakopesheka,” alisema Chiligati.

  Swali kwa huyu Mheshimiwa Chiligati, ni je nani aliifilisi hii nchi? Kwa maneno mengine ni kuwa nani aliifikisha hii nchi hadi ikafikia katika hali ya kuwa mufilisi; [ikawa] haikopesheki? Swali la nyongeza ni je, tumfanyeje huyo aliyeifanya Tanzania yetu ikawa mufilisi kabla ya kumuenzi Mkapa kwa kuinusuru kuwa mufilisi?
   
 2. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  hizoo ni tuhuma za kifisadii ambazoo huwa hatupendi kuzijadilii au hatuna uelewaa nazoo na tumebakia na HIZI ZA MZEE MKAPA..

  Chiligati amefunua shutuma mpya kwamba nchi ilikuwa muflisi na MKAPA akarekebishaa...hongera MKAPA ila hebu pia tufuatiliee huoo umufilisi nani aliufikishaa hapooo..
   
 3. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #3
  Aug 19, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...ama kweli kuna ka-uvivu wa kufikiri.
   
 4. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #4
  Aug 19, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Swali jingine kwa Chiligati ni kwamba je nani hajawahi kuifanyia nchi hii mazuri? Kwa sababu hiyo yeye Chiligati hajaifanyia nchi hii mema? mbona mie nimeifanyia mema mengi tu? Au kuifanyia nchi mema lazima uwe rais?
  Na je kila aliyeifanyia nchi mazuri ruksa kuiba?
  Ni wangapi wamefanyia nchi mazuri wakakosea na wako magerezani?
  Je kufanyia nchi mazuri maana yake kuvunja sheria za nchi?
  Tutamshukuru kwa mazuri na tutamtuhumu kwa mabaya. Aje mwenyewe Mkapa na kuomba radhi kwa watanzania, tutamsamehe.
   
 5. Jiwe Linaloishi

  Jiwe Linaloishi JF-Expert Member

  #5
  Aug 19, 2009
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 3,736
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Tutamsamehe iwapo mizani itabance lakini kwa ninavyoona mabaya ni mengi kuliko mazuri. tumfilisi tu then tumwache apumzike nafikiri hiyo ndio busara. otherwase tumzombe.........
   
 6. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #6
  Aug 19, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Sioni kama ni busara kumfilisi mtu kama Mkapa. Ameiweka Tanzania kwenye mzani jamani siyo kama huyu kaboka mchizi wa sasa hivi.

  Tusiige tabia za nchi nyingine sisi hatuna historia ya kufanya huo ubwege. Nafikiri wafanye tathmini ya vitu alivyonavyo wakimfilisi hiyo hela itafanya nini? Kama bado elimu tuo chini, watoto wanakaa chini, je hiyo hela itakuja kufanya hizo kazi?

  Mwacheni Ben wa watu apumzike mazuri alifanya tuwe na shukrani sometimes.
   
 7. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #7
  Aug 19, 2009
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  mzee mkapa ana nguvu za kufanya kazi na ameshiba napendekeza kwa ufisadi aliofanya tumpe adhabu ya kusomba tofali za ujenzi wa madarasa ya shule za msingi tanzania kwa mikono yake mwenyewe na chenge,lowasa,karamagi,rostam wao wabebe zege na maji kwa mikono yao pia ufisadi utakoma tu.
   
 8. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #8
  Aug 19, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hivi ukimkuta binti njiani hana pa kwenda na mwenye njaa, hana mavazi mazuri ukafanya usamaria wema, ukamchukua nyumbani kwako. Pale nyumbani ukampatia mahali pazuri pa kulala, ukampatia chakula na mavazi na ukampeleka shule kwa gharama yako na wakati huyo binti ameanza kupendeza mara ukamgeuka ukamshika kwa nguvu na kumnajisi (rape her) billa idhini yake na kumpa mimba yule binti atakufikiriaje?

  Hayo ndio ya Mzee Mkapa na Tanzania kutokana na maelezo ya Bwana Chiligati. Eti Mzee Mkapa amekuta nchi katika hali mbaya, haikopesheki akaifufua mpaka Tanzania (binti) ikawa ya neema tele na nchi ikafikia mahala pa kukopesheka. Ilipofika hapo nchi ikabakwa na huyo msamaria mwema na kupata uja uzito na matokeo yake ni mapacha "haramu" kina Meremeta, EPA, Deep Green. Tangold, Kiwira na watoto wengine bado hawajitokeza mpaka labda baba yao hatakapo toweka hapa duniani!

  Rais Mkapa alifanya mazuri ndio lakini akaharibu mwishoni na yeye kama msomi mzuri anajua fika ile riwaya ya Shakespear isemayo kwamba " Matendo mazuri ya mtu akifa nayo ufa naye, lakini yale mabaya ukaa kwenye mifupa yake uko kuzimu".

  Hivi Bwana Chiligati anataka kutuambia kwamba watanzania bado ni wavivu wa kufikri?
   
 9. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #9
  Aug 19, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Wale wazi wa kuku ama samaki huwa wanafungwa miaka kadhaa , je huwa hawana historia ya mambo katika jamii wanayo ishi siku zote ? Sheria inasemaje lakini kwa mtu mwenye tuhuma na hata wizi wa kiwango cha Mkapa , Chenge ......................................endeleza list.Ukimfunga Mkapa means Chenge next na hilo CCM imesema iko tayari kuua watu wote kuliko wana CCM kuguswa
   
 10. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #10
  Aug 19, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  CV yake iko wapi?
   
 11. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #11
  Aug 19, 2009
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,508
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280
  Mzee hivi unauliza swali au ndiyo jibu lenyewe. Kwa taarifa yako CCM washatuona waTZ ni mabwege na wavivu wa kufikiria na ndiyo maana kila kukicha wanatuchezea mazingaombwe (inanikumbusha nilipokuwa primary school wakati maprofesa wa kizaire walipokuwa wanatukoga na mazingaombwe yao) na sisi tunachekelea na kesho yake tumesahau. Kama kweli sisi siyo mabwege na wavivu wa kufikiria mbona hatujafanya kitu??

  Kwa ujumla waTZ hatuamini kama TZ itakuwepo bila CCM kama vile tulivyodhani kuwa hakuna mtu yeyote zaidi ya Nyerere anaweza kuwa rais. Propaganda za CCM zishapandikizwa vichwani mwetu mpaka inatia huruma. Na hii inatia huruma tu kwa wachache wanaoona.
   
 12. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #12
  Aug 19, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,607
  Trophy Points: 280
  Huyu Chiligati huyu na kuropoka kwake...sijui ametumwa au ametunga yeye...katika mawaziri pumba wamu hiii wa kwanza Chilly Boy,jamaa ana Pumba live hadi namuonea huruma kama huu uwaziri ungekuwa kwa interview jamani sijui kama hata udiwani angepata...........jamaa kilaza hasaa
   
 13. M

  Magezi JF-Expert Member

  #13
  Aug 19, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  nawewe unastahiri kutahiriwa bila ganzi!!
   
 14. M

  Magezi JF-Expert Member

  #14
  Aug 19, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Assume sasa huyu chilli ndo mdingi wako.... imekaaje hiyo!!
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  Aug 19, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,780
  Likes Received: 83,133
  Trophy Points: 280
  Inaelekea mwenzetu huyajui aliyofanya Mkapa hadi kuitwa fisadi. Kwa kukumbusha tu alihusika katika ununuzi wa Rada ya kifisadi, uuzwaji wa nyumba holela ambao umeisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 200, kusaini mikataba ya uchimbaji wa madini ambayo haina manufaa kwa Tanzania na pia kujiuzia mgodi kiwizi.
   
 16. Kimori

  Kimori JF-Expert Member

  #16
  Aug 19, 2009
  Joined: May 26, 2008
  Messages: 217
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu Chiligati anatuona Watanzania wote wajinga?, sasa HATUDANGANYIKI!!!
   
 17. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #17
  Aug 20, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  there is no doubt kuwa Mkapa was the best President we had. Kuna mengi yanayothibitisha hayo. Aliichukua nchi ikiwa hovyo na kuifikisha mahali pazuri. Na aliweka mikakati mingi ya kuendeleza uchumi ingawa sasa inaonekana kuwa haitekelezwi. Alituanzishia TRA, aliereform foreign policy, aliweka mkukuta,mmem, memkwa and so on and so on.
  Lakini hii sio kinga ya ujinga alioufanya akiwa ikulu, lazima tuwe honest kama mtu alisimamia ufisadi BOT, kesi ya rada, kagoda etc hakuna anayeweza kusema kuwa ni Mr clean. Au hatuwezi kudanganywa kuwa mkuu wa nchi alikuwa hajui.

  Hata hivyo ni kichekesho kwa Mh Chiligati kumsifu mtu aliyetufany tuweze kukopa, jambo la maana zaidi ni kuwa kama angetufanya tuwe self reliant ingekuwa bora na kumsifu sana. Sijui ana maana gani kuwa nchi ilikuwa haikopesheki.
   
 18. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #18
  Aug 20, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Mkapa alichukua uongozi toka kwa Mwinyi, sasa chilihati anaposema kuwa Mkapa aliikuuta nchi imefilisika anamaana ya kuwa Alhaji ndio ameifilisi nchi hii? GT mambo ndio hayo sasa kibao kiko kwenu!
   
 19. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #19
  Aug 20, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Huo ni upumbavu mtupu kwa sababu huyo Mkapa pamoja na kufanya ufisadi huo bado atakula PENSHENI ya Milele kwa migongo ya walipa Kodi. Alijitahidi kufanya kila aliloweza kuifikisha nchi ilipokuwa lakini rekodi zinaonyesha kuwa alivunja sheria na kushiriki kwenye ufisadi kwa njia moja au nyingine. Is FISADI period, NO QUESTION.
   
 20. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #20
  Aug 20, 2009
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Labda chiligati hajui hata ku-define maana ya neno mazuri... labda alimaanisha mazuri ya mkapa anayotuhumiwa kwa ufisadi....

  Tumpongeze pia Chiligati kwa kuwa mkweli kwamba Mafisadi waliifanya au kuifikisha nchi ikawa hata haikopesheki... Muflisi... Labda tena wanataka tena tuelekee hukohuko kwenye muflisi...

  Washauri wa chiligati inafaa wamchauri asafishe tongotongo machini kwa changa la maji chumvi ili ajue walala hoi wanavyojisikia jinsi mafisadi wanavyoipelekesha nchi hadi kufikia muflisi.
   
Loading...