Hivi mfungwa akifanya tena kosa kubwa akiwa magereza hukumu yake inakuwaje tena

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
24,685
26,779
Yaani kwa mfano mfungwa ambae kashahukumiwa kifungo labda cha miaka kadhaa akiwa huku huko gerezani labda akafanya kosa kubwa tena zaidi ya lililomfunga je hukumu yake inaongezwa akiwa huko huko gerezani au anatolewa anapelekwa tena mahakamani anahukumiwa tena au anahamishwa tena gereza?
 
Anashitakiwa tena kwa mujibu wa sheria za nchi.

Kwa mfano kama ni mfungwa kwa kosa la wizi, akiua mwenzake atapelekwa mahakamani kwa murder case na taratibu zingine zitafuata, kama atabainika na hatia atahukumiwa kunyongwa kama kawaida

Magereza hawahukumu mtu, wao huweza kutoa adhabu endapo umetenda kosa la kinidhamu kwa mujibu wa sheria zao.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na Kama Ni kosa la kukimbia na akakamatwa au mengineyo..pale jela kunakua na mwanasheria wa jela hivo adhabu hutokana na kosa husika..either ile 1ya tatu ya kifungo chake kilichopunguzwa kufutwa na kutumikia full kifungo chake..au kupigwa rungu mpaka ana piga bao...mamaae...jelaaa ...na makosa mengine hupelekea mtu kupelekwa mahakamani na kuwa na kesi ya pili huku Ni mfungwa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom