Hivi methali kama hizi zinaweza kufanyiwa marekebisho?

Nyaka-One

JF-Expert Member
Oct 27, 2013
4,625
6,560
Natambua wahenga wetu walituachia hazina kubwa ya methali na nahau ambazo tumekuwa tukizitumia kwa namna mbalimbali katika maisha yetu.

Hata hivyo kuna baadhi ya methali ambazo pengine kimaadili zingeweza kufanyiwa marekebisho na hivyo kusomeka kivingine. Mfano wa methali hizo ni hizi hapa chini:

1. Maskini akiokota MATAKO hulia mbwata.
2. Cha kuazima hakisitiri MATAKO.
3. Mficha UCHI hazai.

Na kadhalika.
 
Masikini akiokota Makalio hulia Mbwata
Cha kuanzima hakisitiri Makalio
Mficha Sehemu za siri hazai
Na nyingine
Nyani haoni Sehemu za Siri za Nyuma

Zitakosa ladha

Kwny Kiswahili huwa tunasema 'Ashakum si Matusi' then unakuwa na immunity ya kutukana au kutaka maeneo hayo ya Siri kwa majina halisi.
 
Sio hiyo tu mkuu, kuna methali nyingine naona kama hazina tija tena katika ulimwengu huu wa kibepari, mfano aliye huu mngoje chini.
Kwa nini usimfwate huko huko alipo
 
Natambua wahenga wetu walituachia hazina kubwa ya methali na nahau ambazo tumekuwa tukizitumia kwa namna mbalimbali katika maisha yetu.

Hata hivyo kuna baadhi ya methali ambazo pengine kimaadili zingeweza kufanyiwa marekebisho na hivyo kusomeka kivingine. Mfano wa methali hizo ni hizi hapa chini:

1. Maskini akiokota MATAKO hulia mbwata.
2. Cha kuazima hakisitiri MATAKO.
3. Mficha UCHI hazai.

Na kadhalika.
Zeruzeru- albinism!
Kiziwi- asiyesikia!
Kipofu-asiyeona!
matako-makalio!
Hivi huu ujinga wa kupotosha lugha ya kiswahili mchana kweupe ni nani karuhusu!
Hivi BAKITA nao wako wapi kukemea uharamia huu wa lugha sanifu ya kiswahili?
Kinachokera, maneno wanayoona wao hayawapendezi, wanakimbilia kuyafasili badala ya kuyatohoa kama wanaweza!
Lugha yetu tunaipeleka wapi?
Mwishowe sasa kila neno la kiswahili litafasiriwa.
 
Kwa kweli sasa hivi wanakosea sana , maana wanabadirisha maneno ya kiswahili na kuwa sentesi

Sasa Zeruzeru wanasema mtu mwenye ulemavu wa ngozi, ulemavu wa ngozi uko wa aina nyingi, hata ukoma ni ulemavu wa Ngozi

Kipovu wanasema mtu wmenye ulemavu wa Macho, sasa ulemavu wa macho upo wa aina nyingi, hata chongo, makengeza ni ulemavu wa macho
 
Tutengeneze za kwetu zenye mapungufu kibao
Lakini hizi za WAHENGA tuziache kama zilivyo.
Maana zinajitosheleza na zenye kuvutia kuliko za kwetu.
"Shule ya vidudu"
 
Back
Top Bottom