Hivi Membe na Lowassa nani katendwa haswa?

Jiwe alibomoa jengo la tanesco ubungo kwa kudanganywa eti ni la Lowasa.Akabomoa bilcanas kwa kudanganywa eti ni jengo la Mbowe kumbe NHC.Akawabomolea kimara kwa hisia eti walichagua chadema,akawafukuza watu Kazi Ili kumpooza machungu bashite dhidi ya sindano za Gwajiboy,akawanyanyasa watumishi kwa hisia eti walimpigia kura Lowasa.

Chuki ni mbaya sana umuumiza zaidi mwenye chuki.

Hapo pa kubomoa majengo kwa “kudanganywa” umeongopa.Kwamba Rais wa Nchi asijue Billicanas lilikuwa ni jengo la NHC?
 
Sasa kama sio ukichaa ni kitu gani. Ungefunga biashara ukaacha jengo likafanya shughuli nyingine. Akili za kisukuma zinakutuma kwamba jengo ndo lilikuwa linafanya biashara ya ngada?
Ndio maana gari ikukutwa na nyara za serikali hutaifishwa,hali kadhalika mali zitokanazo na biashara haramu hutaifishwa pia,ni mtazamo tu
 
Nimesoma mahojiano ya Membe na gazeti la Jamuhuri ,Membe kamlaumu sana hayati Magufuli,akijua marehemu hawezi jitetea.

Hii kwa wenye utimamu wa akili ni rubbish kabisa.

Kwangu mimi Membe ni muoga sana,na maisha yake mpaka sasa pamoja na umri wake anapenda sana mbereko ,hasifii bure, bali ni mlenga fursa ,watu kama hawa Magufuli aliwatia adabu,mama Samia awe makini sana .

Kwangu mimi Lowassa ndio shujaa wangu, pamoja na rafiki yake kumtenda ndivyo sivyo, mzee wa watu kajikalia kimya kama vile hakuna udhalimu uliofanyika dhidi yake ,huko ndio kupevuka kisiasa na kiongozi.

Ifahamike jamii nzima ya wafuatiliaji wa mambo wanajua alichotendwa.

Membe jifunze kwa Lowassa ,your about 70yrs old now.
No research ni comment bro,haya mambo tuyatizame tu,undani wake hatuujui

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom