Hivi Membe na Lowassa nani katendwa haswa?

Kila mtu ana kiwango chake cha uvumilifu. Ndiyo maana yule ni Membe na yule ni Lowasa. Unazungumziaje visasi vya Hayati ambaye alikuwa anaweka visasi mpaka dhidi ya majengo? Msipangie watu hisia zao. Wewe sifia yeye akandie. Ni mgaanyo wa majukumu tu. Mimi Magu hakuwahi kunitendea personally lakini nachukizwa alivyotendea wengine.

Kikubwa tujifunze kutendea haki watu,tusiangalie matokeo angalia sababu.
Meko alikuwa na kinyongo mpaka na majengo ya Bilicanas na la TANESCO pale Ubungo. Moja la biashara ya Mbowe na jingine akidhani ni la Lowassa...
 
Ingekuwa ni nchi inayojitambua hasa Kisheria na Maadili, kwa Kiapo cha Kazi Nyeti aliyokuwa nayo Bernard Camillius Membe na Kauli zake alizozitoa kwa aliyekuwa Boss wake Mkuu Kimedani na Kiitifaki Hayati Rais Dkt. John Pombe Magufuli hivi sasa alitakiwa awe ameshakamatwa kwa Mahojiano zaidi na Kubwa zaidi hata Maisha yake kufikia Ukomo Kiidara / Kimafia.
Gentamycin popoma
 
Meko alikuwa na kinyongo mpaka na majengo ya Bilicanas na la TANESCO pale Ubungo. Moja la biashara ya Mbowe na jingine akidhani ni la Lowassa...
Billicanas ilikuwepo kimakosa na ilitumika kama kituo cha kuuzia ngada , kiongozi yoyote hawezi achia upuuzi huo uendelee.
Kuhusu Lowassa hajawahi kuwa na uadui na Magufuli,labda ulilishwa matango pori
 
Mhh mkuu nakumbuka JF ilivyokuwa inamshambulia Lowassa tokea alipoacha kazi ya Uwaziri Mkuu hadi Uchaguzi mkuu.
Lowassa aliandamwa na repeated or related issues .
Na ilikuwa kila siku kulikuwa na topic mmoja au zaidi za kumuangamiza Edward Lowassa.
Kuna wakati baadhi ya wadau walipouliza hivi bila kumkashifu Lowassa JF itakuwa imekufa.
Sio kweli kwamba JF ilikuwa upande wa Lowassa.
Kama umesoma na kuelewa maelezo kuna tofauti kubwa kati ya KUJUA na KUSUPPORT hebu tumia akili yako kidogo tu
 
laiti lowasa angekua na akili za kimembe nadhani angemshambulia sana kikwete bt mwamba katulia utadhani hakufanyiwa umafia wowote.
Kikwete tena, dah huyu mwamba ana kazi ngumu sana!
Mijitu hata haijui chochote tayari hiyo inaibuka na kumshambulia kikwete bila kuelewa undani.......kikwete anatabasamu tu
 
Jiwe alibomoa jengo la tanesco ubungo kwa kudanganywa eti ni la Lowasa.Akabomoa bilcanas kwa kudanganywa eti ni jengo la Mbowe kumbe NHC.Akawabomolea kimara kwa hisia eti walichagua chadema,akawafukuza watu Kazi Ili kumpooza machungu bashite dhidi ya sindano za Gwajiboy,akawanyanyasa watumishi kwa hisia eti walimpigia kura Lowasa.

Chuki ni mbaya sana umuumiza zaidi mwenye chuki.
 
Kikwete tena, dah huyu mwamba ana kazi ngumu sana!
Mijitu hata haijui chochote tayari hiyo inaibuka na kumshambulia kikwete bila kuelewa undani.......kikwete anatabasamu tu
.
naona umejicomentia tu bila kujua kinachoendelea
 
Mi nadhani angetumia muda huu kumshukuru Mungu kufikisha miaka 70,maana ni umri wa bahati nasibu kuufikia
 
Nimesoma mahojiano ya Membe na gazeti la Jamuhuri ,Membe kamlaumu sana hayati Magufuli,akijua marehemu hawezi jitetea,
Hii kwa wenye utimamu wa akili ni rubbish kabisa ,
Kwangu mimi Membe ni muoga sana,na maisha yake mpaka sasa pamoja na umri wake anapenda sana mbereko ,hasifii bure ,bali ni mlenga fursa ,watu kama hawa Magufuli aliwatia adabu,mama Samia awe makini sana .
Kwangu mimi Lowassa ndio shujaa wangu ,pamoja na rafiki yake kumtenda ndivyo sivyo, mzee wa watu kajikalia kimya kama vile hakuna udhalimu uliofanyika dhidi yake ,huko ndio kupevuka kisiasa na kiongozi.
Ifahamike jamii nzima ya wafuatiliaji wa mambo wanajua alichotendwa

Membe jifunze kwa Lowassa ,your about 70yrs old now
Matatizo mengi ambayo yako CCM leo yamesababishwa na Membe. Membe ni mfitini mkubwa, ni mvurugaji alijaribu fitina kwa Magufuli akagonga muamba mikubwa ya Mwanza safari yake ya fitina ikafa kifo cha mende. Isingekua tamaa zake za uongozi na mbinu chafu za kumfitini Lowassa pengine leo tusingekuwa tunayaongea ya Magufuli na mambo mengi ambayo ni ya kweli au uongo aliyoyasema Membe kuhusu Magufuli.

Ukimya wa Lowassa unatufundisha kuwa shujaa mara nyingi hasemi bali hunyamaza kimya, lakini, matendo ya kishujaa yana sauti kuliko maneno. Membe ni muoga na mpenda vurugu. Shujaa hapambani na marehemu, marehemu hasemwi vibaya, hasikii haoni hawezi kujitetea hana jukwa la kujitetea. Membe ni muoga huwezi kupambana na wafu ukawa shujaa.

Wasingeshiriki kuiharibu CCM yeye na shemeji yake hao watu anaodai wameuwawa na maiti za kutupwa baharini kama wapo kweli isingetokea kama asingemfini Lowassa yeye na shemeji yake na kundi lake la waoga.

Magufuli ni shujaa kwa muda mfupi aliyohudumu kama rais wa Tanzania ameibadilisha maisha ya watanzania. Ametuthibitishia kwamba Tanzania bila rushwa na ujanjajanja inawezekana. Tuwapuuze waoga wanao ogopa na kutishwa na vivuli vya marehemu kwa jina lao sahihi ni waoga na siyo mashujaa. Membe siyo shujaa ni muoga. Lowassa ni shujaa amenyamaza kimya kwa maslahi mapana ya Taifa. Hajamsema Polepole wala Bashiru yeye ameonesha kuwa ana ngozi ngumu ya kisiasa anao moyo mkuu wakuvumilia. Amekubali kuwa Tanzania ni kubwa kuliko Lowassa akanyamaza kimya na kutoa nafasi kwa wengine kuongoza bila kuwa vuruga. Lowassa ni Shujaa. Magufuli ni shujaa. Tuna nashukuru kwa mtumishi wake uliotukuka na wa uzalendo. Mungu amurehemu. Amin.
 
Membe amejionea kuliko aje apigwe na parinkson disease kisa ma stress ya kusifiwa eti ana ngozi ngumu Bora ajiropokee zake tu Moyo wake upoe.

Ujinga wa kusema marehemu hasemwi nadhani Sasa utaenda kuisha maana watu watakua wanajua Kama ulifanya ukuda hata ukichomoka utasemwa Kama kawaida tu na familia yako itayasikia machungu yaleyale uliyosababisha kwa watu wengine wkt ukiwa hai.

Na Ukweli Ni kwamba Magu alikua na roho mbya kichizi yaani Ile kishenzi lkn Membe nae hua Ni empty brain miaka yote ninayomfahamu.
 
Billicanas ilikuwepo kimakosa na ilitumika kama kituo cha kuuzia ngada , kiongozi yoyote hawezi achia upuuzi huo uendelee.
Kuhusu Lowassa hajawahi kuwa na uadui na Magufuli,labda ulilishwa matango pori
Sasa kama sio ukichaa ni kitu gani. Ungefunga biashara ukaacha jengo likafanya shughuli nyingine. Akili za kisukuma zinakutuma kwamba jengo ndo lilikuwa linafanya biashara ya ngada?
 
Mhh mkuu nakumbuka JF ilivyokuwa inamshambulia Lowassa tokea alipoacha kazi ya Uwaziri Mkuu hadi Uchaguzi mkuu.
Lowassa aliandamwa na repeated or related issues .
Na ilikuwa kila siku kulikuwa na topic mmoja au zaidi za kumuangamiza Edward Lowassa.
Kuna wakati baadhi ya wadau walipouliza hivi bila kumkashifu Lowassa JF itakuwa imekufa.
Sio kweli kwamba JF ilikuwa upande wa Lowassa.

Yeye anaongelea upande wa uvumilivu kama nimemwelewa.Hayo unayoyasema hapa yanadhihirisha kiwango cha juu sana cha ukomavu na uvumilivu wa kisiasa wa Lowassa.Nakumbuka 2007-2008 JF lilikuwa inabamba na hot topics za Richmond zilizopelekea EL kuresign.Kinara wa mashambulizi alikuwa Mzee Mwanakijiji.I miss JF ya enzi hizo.
 
Back
Top Bottom