Wickama
JF-Expert Member
- Mar 8, 2009
- 1,466
- 1,195
Wadau,
Mbwa ni wanyama wanaotumika sana na majeshi yote duniani ili ama kupambana na uhalifu, kuokoa watu kwenye majanga, kugundua yalipo mabomu ya kuchimbia na hata kwenye viwanja vya ndege kutambua mizigo iliyobeba bidhaa hatarishi kama madawa ya kulevya, nyara za serikali na kadhalika.
Ukiachilia miaka ya nyuma sana sikumbuki kuliona jeshi letu la polisi likitumia mbwa hawa kuwasaidia kusaka walikotorokea wahalifu kama wezi wa mifugo na wengine wengi. Nadiriki kusema mbwa hawa wanatumika zaidi kudhibiti mikusanyiko ya kiraia. Yaani kwa sasa ndio kama jukumu lao la msingi. Nilishawahi kuona uwanjani Entebbe mbwa hawa wakikagua kwa kunusa mizigo ya abiria wanaoondoka na hata kuingia nchi hiyo. Sijawahi kuona kitu kama hicho hapa kwetu. Ni kawaida wenzetu nchi za nje kuwatumia hata kugundua alipozikwa mtu baada ya kufanyiwa jinai. Bongo sijui.
Kwa kweli zile "images" za askari polisi zamani wakihaha na mbwa hawa kufuata nyayo na harufu za walikopita wahalifu siku hizi SAHAU. Pia, ni kawaida sana kwa viongozi wa jeshi la polisi kutoa takwimu za ajali au uhalifu kupanda au kushuka, sijawahi kusikia taarifa zinazobainisha mchango wa kiweledi wa wanyama hawa na matukio husika katika mwaka wowote. Maafande, nitashukuru kukosolewa kama hali ni tofauti sana. Mawazo yenu tafadhali.