Hivi mbona VODA na TIGO zimekuwa ghali sana???

Tatizo nimeliona kwa Tgo ukiweka vocha inalika bila hata kutumia huduma yoyote kwa mara 3 salio langu linatoweka situmii ring tone caller au upokeaji wa sms za taarifa yoyote. Voda, sijao tatizo sana na tarif zao, wapo na ughali fulani lkn ukifuata tarif yao wapo poa

Kaka ni wote hakuna tigo, voda, airtel wala zantel, mimi natumia zote kasoro airtell ila ni balaa!!!!
 
hata Airtel karibia mitandao yote nyakati za mchana hazishikiki, baada ya umeme sasa mawasiliano.
 
Tigo mmenilia hela yangu nawalaani, na kuanzia leo situmii mtandao wenu, na kuwataarifu jamaa zangu wasiutumie mtandao wenu kwani mlichokifanya ni dhambi, siku zote mnatangaza promotion zenu na ofa mbalimbali za kupunguza bei sasa mmeongeza viwango vyenu tena kwa gharama kubwa bila kuutaarifu umma, huu ni wizi na tena ni uchafu yani mnanuka pamoja na TCRA.
 
Mitandao imeungana sasa ina dictate bei! vile vita vya kushusha bei mpaka zero vimekwisha wengine wamegundua watakufa very soon so wameamua kukaa meza moja na kukubaliana bei elekezi

kama ni hivi, ni hatari sana. Oligopolies wakiungana, huzaa monopoly na hapa ndo mlaji anaponyonywa tn the maximum.
Sheria ya usindani (fair competition act) inakataza any attempt ya oligopolies kuungana.
Sijui TCRA wanataarifa gani katika hili.
 
Back
Top Bottom