Hivi mbona serikali inatumia mahakama kama chaka la kuficha maovu yake? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi mbona serikali inatumia mahakama kama chaka la kuficha maovu yake?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Mtumishi Wetu, Jul 30, 2012.

 1. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Wadau nimeona tujadili hili la serikali yetu kutumia mahakama zetu kama chaka la kuficha maovu yake!!! Tuliona swala la madaktari walipoanza tuu mgomo serikali ikakimbilia mahakamani kusitisha mgomo ikidai kuwa ni batili, limekuja swala la walimu wanasema swala liko mahakamani!! Sasa tuseme mahakama zetu ni dhaifu hazina sheria kali za kuweza kudhibiti watu kukimbilia mahakamani kuweka stop order??? Je ikiwa wakipeleka kesi wakashindwa adhabu zinazotolewa ni dhaifu kiasi hawaziogopi kama vile kutolewa amri ya kutaifisha na kuuza mali za serikali hadi walipe madai ya watu??? Nawasilisha!!!
   
 2. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Mahakama hawana nguvu yeyote ile kwa sababu ndio walewale ndio wapo huko, Ila Watanzania cha kufanya ni moja tu!
  Tumweleze MUNGU haya yote ya kwmb tumechoka na haya Mungu wetu.
  Na ni Imani tosha kabisa iko nyakati itafika na Watanzania watafurahia maisha bora lakini ni mpaka uongozi wote uliko madarakani ubwagwe chini!
  Mahakama wameifanya maficho yao.

  Mwisho wao waja hakika!
   
 3. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #3
  Jul 30, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Nashukuru mkuu kuliona hilo, mahakama zetu zinashushiwa hadhi siku hizi hata Majaji wanawekwa wa magumashi!!!
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Jul 30, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ni dalili ya udhaifu na kushindwa kutatua matatizo yanayowakabili wananchi wake
   
 5. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #5
  Jul 30, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hakuna kitu, mahakama ni zile zile wale wale!
   
 6. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #6
  Jul 30, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160


  Kauli ya PM hii hapa: (LIWALO na LIWE)
  Kweli mtu anapewa mamlaka ya kuongoza raia zaidi ya 40M halafu anadiriki kuja na kauli kama hiyo jamani tutafika?

  2015 Mi ningetamani iwe baadae nione ujeuri wa ccm iko wapi!
   
 7. Mkwai

  Mkwai JF-Expert Member

  #7
  Jul 30, 2012
  Joined: Feb 29, 2012
  Messages: 308
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kuna wakati nashindwa kuelewa utofauti uliopo kati ya serikali na mahakama, sometimes nashawishika huenda serikali na watawala ndio mahakama yenyewe. Katika patashika zote zilizotokea kwa wafanyakazi kudai stahiki zao, serikali ndio imekuwa ikitoa matamko kwa niaba ya mahakama. Nilitegemea mahakama ndio itoe stop order katika matimbwili haya lakini la hasha, ni matamko ya serikali tu.
   
 8. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #8
  Jul 30, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Kuna haja mkuu hata mahakama zetu kwenye katiba mpya kuwe na kipengele cha maadili mtu asipewe kazi ya Ujaji bila kufanyiwa vetting tena ipitie bungeni kuthibitishwa !!! Mtu mwenye dalili za rushwa asipitishwe kuwa hakimu hata wa mahakama ya mwanzo, wenzetu Kenya wanaendelea na zoezi hilo la kuondoa uozo kwenye judicially yao!!

   
 9. Lastname

  Lastname JF-Expert Member

  #9
  Jul 30, 2012
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 925
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Wahuni wenzao
   
 10. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #10
  Jul 30, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Mihimili ya ya dola si lazima itofautishwe, mahakama inatakiwa kuwa ndio kipimo cha utawala bora yenyewe iwe check and balance, sasa inasikitisha ikigeuzwa ni njia ya kukandamiza wanyonge???

   
 11. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #11
  Jul 30, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,947
  Likes Received: 2,093
  Trophy Points: 280
  Ukiangalia kwa undani Tanzania kuna mihimili miwili - Bunge an executive. Mahakama ni mkono wa state hivyo kusema ni mhimili sion sahihi kwa sababu inawajibika kwa state!
   
 12. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #12
  Jul 30, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Ndio maana tunasema lazima katiba mpya iwe wazi kuhusu mahakama ili ipate haki yake inayostahili, kuliko kutumiwa na serikali kama tambala la kufuta uchafu wake!!!

   
Loading...