Hivi mbona maji ya Uhai, Afya au Pangani hayanywewi kwenye hafla kubwa? Maji ya Kilimanjaro yana nini?

Dabil

JF-Expert Member
Sep 30, 2021
1,675
2,000
Mkuu hivi hujawahi kupiga maji ya uhai au afya mara ile lebo ianguke yenyewe sijui gundi wanaweka ndogo, sasa maji gani unakunywa unashangaa lebo inaondoka na upepo wa feni
Unabaki bila lebo watu wanakuona umeweka kvant au gongo kwenye chupa
 
Peril22

JF-Expert Member
Apr 15, 2020
540
1,000
Kwa sasa ni Dew Drop awa jamaa wapo vizuri sana kilimanjaro wameyaaribu sana kwa tamaa zao wenyewe watu wengi sana wanafoji kilimanjaro water
Huu ni ukweli, haya maji kwa sasa yamekuwa tofauti na zamani. Kwa mara ya kwanza niligundua shida hii nikiwa kule Rufiji kwenye mradi wa umeme nikadhani labda wale waarabu wa JV wamefanya yao ila nilikuja kwenye training flani Dodoma tukawa tunapewa haya maji nikakutana na the same shit nikagundua ni tatizo la hawahawa majamaa.
 
mfianchi

JF-Expert Member
Jul 1, 2009
10,826
2,000
Leo nilikuwa nafuatilia Tuzo za TFF, pamoja na mambo mengine nimefuatilia maji yaliyokuwa yananywewa na wadau, hakuna zaidi ya Maji ya Kilimanjaro.

Haya maji ya Uhai, Pangani au Afya yanayouzwa sana kwa mama lishe kule Tandika na Kariakoo imekuwaje huko kwa wakubwa?
Maji ya Uhai yanywewa huko Chamazi complex mkuu na hayana viwango,kuna tofauti kati ya maji ya visima na maji ya chemchem,pia jua maji ya Kilimanjaro ni chapa kubwa ya maji ambayo haifikiwi na maji yoyote haya ya visima vyetu vya Mbagala.Mzee machache aliwaingiza chaka CocaCola ambayo nao wana hisa kiasi, walipoleta maji yao Dasani tayari walikuwa washachelewa, lakini hata wewe mwenyewe mleta maji ukinywa maji ya Kilimanjaro na unywe hayo ya Chamazi yapi utajisikia kweli umekunywa maji? Kiwango cha Kilimanjaro ni kile kile hakibadiliki ni sawa na maji ya zamani ya kampuni ya PepsiCola Glacier(watoto wa jana) hawajui kwamba maji ya kwanza ya chupa (mineral water ) yalikuwa yanaitwa Glacier,enzi zile maji tulikuwa tunakunywa bure kwenye mabomba,hakukuwa na maji ya chupa labda mtu atoke nayo hijja huko Mecca, baada ya Glacier kutoweka ndio yakaja Kilimanjaro.
 
mfianchi

JF-Expert Member
Jul 1, 2009
10,826
2,000
Maji ya kilimanjaro ndo yaliyoanza ya kwanza TZ, hivyo hata ufanyaje, hata iweje, mkubwa ni mkubwa tu.
Si kweli maji ya kwanza Tanzania yalizalishwa na kiwanda cha PepsiCola yaliitwa Glacier, ndio yakaja Kilimanjaro na Maji Afrika ya Iringa.
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
89,756
2,000
Maji ya Uhai yanywewa huko Chamazi complex mkuu na hayana viwango,kuna tofauti kati ya maji ya visima na maji ya chemchem,pia jua maji ya Kilimanjaro ni chapa kubwa ya maji ambayo haifikiwi na maji yoyote haya ya visima vyetu vya Mbagala.Mzee machache aliwaingiza chaka CocaCola ambayo nao wana hisa kiasi, walipoleta maji yao Dasani tayari walikuwa washachelewa, lakini hata wewe mwenyewe mleta maji ukinywa maji ya Kilimanjaro na unywe hayo ya Chamazi yapi utajisikia kweli umekunywa maji? Kiwango cha Kilimanjaro ni kile kile hakibadiliki ni sawa na maji ya zamani ya kampuni ya PepsiCola Glacier(watoto wa jana) hawajui kwamba maji ya kwanza ya chupa (mineral water ) yalikuwa yanaitwa Glacier,enzi zile maji tulikuwa tunakunywa bure kwenye mabomba,hakukuwa na maji ya chupa labda mtu atoke nayo hijja huko Mecca, baada ya Glacier kutoweka ndio yakaja Kilimanjaro.
Umenikumbusha Glacier hadi nimelia , ndio maji pekee yaliyouzwa club za dsm , tena yaliuzwa bei sawa na bia , sasa sisi vijana wa kishua wa Tandika tulikuwa tunajiuliza tununue bia au maji ? Da Da Dah .
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
89,756
2,000
Si kweli maji ya kwanza Tanzania yalizalishwa na kiwanda cha PepsiCola yaliitwa Glacier, ndio yakaja Kilimanjaro na Maji Afrika ya Iringa.
Hivi nyie kyela lini mtatengeneza maji ya kwenu , mtakunywa ya Tukuyu hadi lini ? au mpaka nije mimi niwatengenezee ?
 
Santos06

JF-Expert Member
Mar 11, 2019
2,149
2,000
Leo nilikuwa nafuatilia Tuzo za TFF, pamoja na mambo mengine nimefuatilia maji yaliyokuwa yananywewa na wadau, hakuna zaidi ya Maji ya Kilimanjaro.

Haya maji ya Uhai, Pangani au Afya yanayouzwa sana kwa mama lishe kule Tandika na Kariakoo imekuwaje huko kwa wakubwa?
Maji maji tu
 
Thidanganyiki

Member
Mar 25, 2015
39
125
1. Dew Drop
2. Cool blue
3.Udzungwa

Hakuna maji kama hayo kwa Bongo!
Pia haya maji ya Cool Blue sijui kwanini hayapatikani sehem nyingi hata kwa Dar kuyapata ni shida!!
_20211023_110637.JPG
_20211023_111358.JPG
_20211023_112700.JPG
 
mfianchi

JF-Expert Member
Jul 1, 2009
10,826
2,000
Hivi nyie kyela lini mtatengeneza maji ya kwenu , mtakunywa ya Tukuyu hadi lini ? au mpaka nije mimi niwatengenezee ?
Sisi yanatutosha ya mto Kiwira,Songwe,Mbakka,Lufilyo na visima vilivyosheheni kila nyumba. Huko Kyela pamoja na kuwa na maji mazuri kutoka kwenye safu ya Milima ya Livingstone hakuna anayewaza kujenga kiwanda chochote ukiacha mbali hivi visido vya kukobolea mpunga. Kyela tuna safari ndefu sana kwenye mambo ya maendeleo, watu wakishalima mpunga na kupata gunia 5 basi shughuli imeisha hakuna tunachowaza zaidi ya starehe za Mang'oma.
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
89,756
2,000
Sisi yanatutosha ya mto Kiwira,Songwe,Mbakka,Lufilyo na visima vilivyosheheni kila nyumba. Huko Kyela pamoja na kuwa na maji mazuri kutoka kwenye safu ya Milima ya Livingstone hakuna anayewaza kujenga kiwanda chochote ukiacha mbali hivi visido vya kukobolea mpunga. Kyela tuna safari ndefu sana kwenye mambo ya maendeleo, watu wakishalima mpunga na kupata gunia 5 basi shughuli imeisha hakuna tunachowaza zaidi ya starehe za Mang'oma.
Amang'oma , Isamba na amagosi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom