Hivi mbona maji ya Uhai, Afya au Pangani hayanywewi kwenye hafla kubwa? Maji ya Kilimanjaro yana nini?

kilimanjaro tu tayari una utangaza mlima mrefu barani africa pia hizo hafla zina fuatiliwa na mataifa mengi hivo kuwepo kwa maji yenye jina kilimanjaro ni vzuri zaidi kuliko kuweka masafi mezani
 
hili jambo linashangaza, wakati kwa test maji ya Afya na Hill ndiyo yanaongoza.
Kilimanjaro the best asikudanganye mtu, Kilimanjaro upate yale yenyewe ya kutoka shirimatunda Moshi na siyo haya ya Tandika wanayochakachuwa.

Pili Hill water.

Tatu Udzungwa kutoka Moro, hawa wameshindwa tu countrywide distribution.
 
Leo nilikuwa nafuatilia Tuzo za TFF, pamoja na mambo mengine nimefuatilia maji yaliyokuwa yananywewa na wadau, hakuna zaidi ya Maji ya Kilimanjaro.

Haya maji ya Uhai, Pangani au Afya yanayouzwa sana kwa mama lishe kule Tandika na Kariakoo imekuwaje huko kwa wakubwa?
Ni kwel..ila pia tambua hayo maji yanaingiza hasara iliyotukuka maana yanatumika mara moja moja sana compared na haya mengne ambayo ni kama basic need ya watu...tembea mitaan utajionea..so kampun imebak na brand kubwa tu ila haina mauzo..hayo ndo maajabu
 
Hahahah, sahihi kabisa mkuu...Wanahitaj darasa kwenye branding
Ukiweka takwimu maj ya kilimanjaro ndo yenye mauzo hafifu kuliko hizo kampun zingne....yaan limebak jina tu ila mauzo hakuna..mtaan kwenye wanunuz weng huwez kuyakuta hayo..hayo yanauzwa kwenye mikutano tuu ambayo ni moja moja..sasa hyo hasara kubwa kwa kampun..uhai unayakuta had vichochoron huko..so wajifunze...bila hvyo naamin hyo kampun inaenda kuanguka sooon
 
Maji matamu Sana . Huo uhai hayana yofauti ni viroba. Package na quality ya maji hayana mpinzani .
Lakin ndo anaongoza kwa mauzo.....uhai water...hiv wa Tz lin tutakua na akil...uhai analenga watu wa hali ya chin ambo ndio 95% ya watu wote Tz..hao kilimanjaro wanalenga 5% ya watu...hata siku1 mfanyabiashara mwenye akil na anaetaka pesa na faida hawez lenga hilo soko dogo..ndiomana bakhresa ataendelea kuwa juu..ana akil..na hao kilimanjaro wasipokua makin kiwanda kitakufa..watakua wanapata hzo tenda za mikutano michache na kuliacha soko kubwa la mtaan
 
Leo nilikuwa nafuatilia Tuzo za TFF, pamoja na mambo mengine nimefuatilia maji yaliyokuwa yananywewa na wadau, hakuna zaidi ya Maji ya Kilimanjaro.

Haya maji ya Uhai, Pangani au Afya yanayouzwa sana kwa mama lishe kule Tandika na Kariakoo imekuwaje huko kwa wakubwa?
Ilo jina tu la Kilimanjaro lina tangaza kivutio cha utalii hapa Nchini,
 
Ule mlima maarufu ni brand tosho kwa hayo maji, hata maelezo yake yanavutia kuyanywa kwani yanatoka kwenye chemchem zilizoko mlima kilimanjaro. Kingine ni maji ya kwanza kutengenezwa na kuuzwa kwenye chupa, pia yalitangazwa sana kwenye media na kuaminiwa na watu
 
Nadhani utamaduni wetu wabongo kutopenda vitu vya bei ya chini sana tukiamini kitu kikishakuwa bei ya chini tunahisi kina kasoro fulani mf; Kilimanjaro water imekaa kwenye bei halisi miaka mingi kwa ujazo ule ule bila kubadilika.
Linganisha matumizi pia ya bidhaa za Coca-Cola na Pepsi,Coca ipo juu daima,ukienda sehemu mwenzio apewe coca wewe uliepewa Pepsi utajisikia hovyo
Kuna Colgate na Whitedent,whitedent watasubiri sana kwa colgate
Bidhaa za Toyota na Tata,Tata watasubiri sana japo bidhaa zao ni za bei ya chini.
Sisi Watanzania tunapenda kujiaminisha kupitia bei tukiamini kitu cha bei kubwa ndicho kizuri,hatuangilii cha bei ya chini kwani tunaamini udogo wa bei ndio mapungufu yake
Kwenye pepsi na coca mzee umepuyanga saivi pepsi iko juu hatari
 
Back
Top Bottom