Hivi mazingira yangeruhusu Marais watumbuliwe kama wateule wengine tungekuwa na Marais wangapi?

MWITONGO MAARIFA

JF-Expert Member
Aug 11, 2018
276
1,428
Nimeona namna wateule wanavyoteuliwa na kutenguliwa kila leo nikajiuliza endapo tungepewa rungu la kutengua Marais na kuweka wapya je toka kuundwa kwa nchi yetu tungekuwa na Marais wangapi?

Kwanini tusiwaze kuwa na njia ngumu za uteuzi na njia ngumu za kutengua Kama walivyo Kenya? Utenguliwe kwa sababu na uzijue na wananchi wazijue na unapoteuliwa pia tujue kwanini umeteuliwa .
 
Huo utenguzi upo ila mwenye mamlaka hayo ni mkuu wa majeshi c.d.f lakini hadi afanye hivyo kuna prosesi ndefu inategemea na kosa laa rais mwenyewe
 
kutumbuliwa au kujitumbua ni moja ya uwajibikaji kwa mtu ambaye kaenda kinyume na maadili ya kazi yake. kwa nchi zilizoendelea , mtu akiona kakosa anajiwajibisha mwenyewe ila ni utamaduni usizoeleka kwa Afrika hivyo kutumbuliwa ni haki yao.

unaposema kwamba marais wangapi wangekuwepo kama wangekuwa wanatumbuliwa ni kukosa ufahamu wa majukumu na uongozi. Taasisi lazima iwe na kiongozi imara anayewajibika vyema na kuwawajibisha wale wasiofanya vyema. kuna makosa ya kiongozi, uongozi na wanaongozwa na kiongozi katu asionekane mbaya kwa kuwawajibisha wanaokosea na pia duniani kote , mara nyingi Rais anapotenda kosa linachukuliwa kama kosa la uongozi, huwezi kuwajibisha uongozi mzima na ukifanya hivyo tambua lazima uongozi mzima uyumbe.
 
..Raisi anapokosea, kama alivyofanya Magufuli, kwa kuvuruga na kuhujumu uchumi, anawajibishwa kwa kupitia sanduku la kura.

..Demokrasia yetu ingekuwa imekomaa hivi tunavyoandika kusingekuwa na ubishi kwamba Raisi Magufuli na CCM wanakwenda kushindwa ktk uchaguzi wa 2020.

Mag3, Quinine
 
kutumbuliwa au kujitumbua ni moja ya uwajibikaji kwa mtu ambaye kaenda kinyume na maadili ya kazi yake. kwa nchi zilizoendelea , mtu akiona kakosa anajiwajibisha mwenyewe ila ni utamaduni usizoeleka kwa Afrika hivyo kutumbuliwa ni haki yao.

unaposema kwamba marais wangapi wangekuwepo kama wangekuwa wanatumbuliwa ni kukosa ufahamu wa majukumu na uongozi. Taasisi lazima iwe na kiongozi imara anayewajibika vyema na kuwawajibisha wale wasiofanya vyema. kuna makosa ya kiongozi, uongozi na wanaongozwa na kiongozi katu asionekane mbaya kwa kuwawajibisha wanaokosea na pia duniani kote , mara nyingi Rais anapotenda kosa linachukuliwa kama kosa la uongozi, huwezi kuwajibisha uongozi mzima na ukifanya hivyo tambua lazima uongozi mzima uyumbe.
Inabidi uweke ukada pembeni nna ubaki na uhalisia kimsingi hao wote waliotumbuliwa wamefanya makosa ya kiuongozi maana wao walikua ni viongozi kwenye taasisi walizokua wakifanya kazi na vile vile Raisi ni kiongozi kama ulivyosema kimsingi Raisi na yeye anatakiwa awajibishwe maana makosa yote hayo yanaanzia kwake yeye alieteua watu bila kuangalia vigezo vya msingi na hata uteuzi huu mpya na wenyewe umekaa vile vile mleta mada ameongea jambo ambalo kada kama wewe huwezi ona unapoteua mtu inabidi useme sababu za kumteua na vile vile kwenye utenguzi lazima sababu zisemwe...maana unamtengua mtu gizani unaficha nini
 
Back
Top Bottom