Hivi mawaziri kuto maelezo kwa wabunge kwa kuchanganya kiingereza na kiswahili wananchi wanawaelewa

simaye

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
426
214
Kumekuwa na kasumba ya watendaji wakuu wa serikali kutoa maelekezona majibu kwa kutumia lugha ya kiingereza na kiswahli, Hali hii imepelekea wananchi wengi kubaki wasikilzaji wa sauti pasipo kuelewa nini wameelekezwa na mwisho wanawapigia makofi ya mkumbo baado ya kuona mheshimiwa wa aliye jirani na msemaji akipiga makofi.Waugwana mnafikiri nini kinaweza kufanyika ili viongozi hawa wanapozungumza na watanzania walio wengi watumie kiswahili ambacho kinaeleweka?
 
Unajua hao ndiyo wanasiasa wa Tanzania. Wanadhania wataonekana kuwa ni wasomi na wamebobea kwenye elimu. Mimi naona ndiyo ushamba wenyewe huo!!

Mfano mwingine ni huo ma Ma Dkt. Kila mwanasiasa anajututumua awe Dkt(Dr), kama shule ikimgonga au imemgonga atanunua cheti na kujipachika huo u Dkt au ataanza kujiita tu pale atakapotunikiwa shahada ya heshima!

Kujiita Dkt kwa shahada ya heshima ni utovu wa nidhamu, kama vile ambavyo kiongozi anavyokuwa anazungumza na watu kiswahili halafu anaingiza neno au maneno ya kiingereza ili aonekana kaenda shule!

Wengine wanafanya hivyo ili kuwakoga watu, kwa ajili ya mbwembwe na mikogo, lengo lake likiwa lile lile kutaka kuonekana wameenda shule na wanajuwa kiingereza. Kinachosikitisha ni kuwa wengi wao wanazungumza kiingereza kibovu (broken)- Na wakienda kwenye mikutano ya kimataifa wanakuwa wanajibana bana na hawachangii chechote kwa sababu lugha ya watu inawapiga chenga:bored:
 
Kumekuwa na kasumba ya watendaji wakuu wa serikali kutoa maelekezona majibu kwa kutumia lugha ya kiingereza na kiswahli, Hali hii imepelekea wananchi wengi kubaki wasikilzaji wa sauti pasipo kuelewa nini wameelekezwa na mwisho wanawapigia makofi ya mkumbo baado ya kuona mheshimiwa wa aliye jirani na msemaji akipiga makofi.Waugwana mnafikiri nini kinaweza kufanyika ili viongozi hawa wanapozungumza na watanzania walio wengi watumie kiswahili ambacho kinaeleweka?
Inaonesha ufinyu wa elimu zao.

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom