Hivi Marekani akiiwekea vikwazo Tanzania ndio upinzani unaingia Ikulu? Zimbabwe imewekewa vikwazo lakini chama ni kile kile ZANU PF

Corticopontine

JF-Expert Member
Sep 20, 2019
664
1,272
Ukimwangalia ZITO tabia ya usaliti alianza nayo toka zamani tangu enzi akiwa CHADEMA mabeberu wake walikuwa ni Serikali ya Kikwete iliyokuwa inamtumia kula hela zaidi

Alipoingia Magufuli alijua kuwa utaratibu ule wa awali utaendelea kwamba Magufuli ataendelea kumtumia Zito kudhoofisha Upinzani ndiyo maana wakati wabunge wenzie wa Upinzani wanasusia bunge yeye alibaki bungeni

Wakati Tundu Lissu anazunguka Ulaya na Marekani kumtukana Rais yeye alimtukana pia Lissu

Baada ya kujipima na kuangalia nguvu ya Ushawishi imeisha na hayupo wa kumbeba ikabidi ajisalimishe kwa Mabeberu wamtumie kuharibu Taswira ya nchi

Aliona wivu jinsi Lisu alivyokuwa maarufu kwa hiyo ameamua kumvuruga Lisu

Lakini tujiulize Marekani akiweka Vikwazo Tanzania ndo CCM itaondoka? Jibu hapana pia Zito akumbuke kwamba Nchi ikiwekewa Vikwazo huwa inajiweka kwenye State Urgency yaani wananchi huungana kuyakabili matatizo
 
Cuba je???, tangu 1900s mpaka leo mwendo ni ule ule, Castro alikaa akazeeka akamwachia kaka yake naye kachoka kamwachia mtu wake. US wanaongeza vikwazo kila siku ila wanaoumia ni watu wa kawaida na sio viongozi.

Mfano mwingine ni Venezuela, wananchi ndio walioishia kuikimbia nchi lakini jamaa wa upinzani pamoja na push ya US imeshindikana kuingia Ikulu.

Kwa hyo wapinzani wawe waangalifu US siyo rafiki mzuri, anaangalia maslahi, akiona hulipi anakugeuka kama nn vile.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania ikiwekewa vikwazo hivo, ndio tutajua kama CCM ni wazalendo wa kweli kwenye nchi hii au sio wazalendo (Kama ni wazalendo basi watakubali waachie madaraka, ili kuwanusuru wananchi kutaabika na shida za vibano hivo kutoka kwa mataifa yenye nguvu duniani).

Robert Mugabe hakuwa mzalendo wa nchi yake, alikua na tamaa ya madaraka na alikua muoga wa maisha yake (alikua na Personal Interest), na ndio maana baada ya kuwekewa vikwazo vikali Zimbabwe yeye aliendelea kung'ang'ani madaraka kwa nguvu mpaka wananchi waliadhirika kwa shida na njaa. Angekua mzalendo halisi basi angeachia madaraka ili kuwaokoa wananchi wake (hata kama ingetakiwa afungwe jela ili kuokoa taifa lake, basi angekubali).

Kuna toafuti kati ya "PERSONAL INTEREST" na "CIVILIAN INTEREST", yaani tofauti ya matakwa binafsi ya mtawala na matakwa ya wananchi/watawaliwa.
 
Corticopontine,
Mkuu kwani CCM ni nini? kama tu wajinga kihivyo kwamba tuwe kama Zimbabwe but ccm na magufuli waendelee kuwa madarakani sawa,but kama sisi si wajinga basi tutamtosa Yona baharini ili sisi,watoto wetu na nchi yetu tupone
 
Kuna watu hawaijui hii nchi vizuri, mpaka leo hakuna high profile political figure defection kama ya Oscar Kambona na alikimbilia huko huko kwa akina Beberu alirudi nyumbani baada ya umauti kumkuta huko.

Alikuwepo mtaalam Prof. Babu, yeye alirudi home wakati aneshazeeka sana na kupoteza mvuto wake wa kisiasa...

Sisi yetu macHO. Corticopontine,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni afadhali tuwekewe vikwazo ili sote tuteseke (pamoja na wale wanaotutesa sasa i.e Meko na Bashite)

Tukiwekewa vikwazo mauaji yatapungua, kutekana na kubambikiana kesi pia kutapungua kwani hawa madhalimu watakuwa busy kutafuta namna ya kupata fedha za kuendesha serikali yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cuba je???, tangu 1900s mpaka leo mwendo ni ule ule, Castro alikaa akazeeka akamwachia kaka yake naye kachoka kamwachia mtu wake. US wanaongeza vikwazo kila siku ila wanaoumia ni watu wa kawaida na sio viongozi. Mfano mwingine ni Venezuela, wananchi ndio walioishia kuikimbia nchi lakini jamaa wa upinzani pamoja na push ya US imeshindikana kuingia Ikulu.
Kwa hyo wapinzani wawe waangalifu US siyo rafiki mzuri, anaangalia maslahi, akiona hulipi anakugeuka kama nn vile.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mnahalalisha unyama wenu? Kama mnadhani tutadanganyika kwa mifano yenu ya kidikteta jueni hatidanganyiki.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu usidanganye vikwazo tukiwekewa tutakaoumia ni sisi wananchi wa kawaida viongozi kamwe usitegemee kuwa watakua na shida.
Ni afadhali tuwekewe vikwazo ili sote tuteseke (pamoja na wale wanaotutesa sasa i.e Meko na Bashite)

Tukiwekewa vikwazo mauaji yatapungua, kutekana na kubambikiana kesi pia kutapungua kwani hawa madhalimu watakuwa busy kutafuta namna ya kupata fedha za kuendesha serikali yao.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom