Hivi Maprof na PHD candidates wanapublish wapi paper Zao Bongo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Maprof na PHD candidates wanapublish wapi paper Zao Bongo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nicholas, Apr 9, 2015.

 1. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #1
  Apr 9, 2015
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,220
  Likes Received: 2,447
  Trophy Points: 280
  Nimejaribu sana kufuatilia PHD za US na Maprof wao..Aisee watu wanapigika sana paper zao kuwa published ktk journals za kueleweka.Watu wote wanapigika hadi wanaonyesha kiwango na weledi ndio wanapita.Si weupe,si wekundu,si wa njano na hata weusi..wengine hadi wanakimbilia kusema ni ubaguzi wa rangi..ila wakipita huwa wanaonyesha hiyo mambo haswa ktk real life.Hapa Bongo naona design km watu wanachukua tuu gamba..labda tuu km kuna siasa ndio zinawakwamisha.Kuna watu wa uchumi,Political science,vyuo vipya km vinapiga promo kwa staff wao fasta fasta fulani.Hivi kuna hizo journal ambazo haziwezi kuwa influenced kisiasa kweli?
   
 2. kivike9

  kivike9 Member

  #2
  Apr 9, 2015
  Joined: Aug 11, 2013
  Messages: 30
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Hapa cjui WAP itabid kufuatilia
   
 3. lusungo

  lusungo JF-Expert Member

  #3
  Apr 9, 2015
  Joined: Jan 4, 2014
  Messages: 18,661
  Likes Received: 10,145
  Trophy Points: 280
  Zipo makatini mkuu!!!

  Zikishapitishwa ni mwendo Wa pombe... zinaa na kungojea kustaafu hakuna la ziada ktk ufwatiliaji Wa walichoandika ndio maana akina Mwakyembe walisahau hata walichowahi andika!!!!!!
   
 4. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #4
  Apr 9, 2015
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,220
  Likes Received: 2,447
  Trophy Points: 280
  Kuna watu nawaona wamechukua PHD haraka haraka ,na wengine associate profs ....na wanazitumia sana km gia ya kuruhusiwa ongea chochote,popote, ila hata raia wa kawaida tuu wakiingia ktk fikra wanaumia kichwa sana wakijaribu reconcile na fikra zao km kweli wanachokiona na kusikia ni kweli au ni macho yao na msikio yanashida.Si utani kumwona prof kakosea kirahisi namna watanzania wengi wanaona.Mwakyembe alipiga ujerumani ilibidi aumie sana ili kuipata hata km hakuamini sana alichokisoma ilibidi auate tuu aipate.Ila sijui kwanini hajawa prof mapema km akina Kitila,au walimu wengine wengi wa vyuo vilivyokuwa University faster.Nawajua watu wamelia sana marekani aisee kuchukua nafsi kuwa mwalimu wa chuo..wamesota wamjichomeka ktk project kibao,wameanzisha project kibao na kuziacha ,hadi kuandika minimu ya paper 2 zitakazopita na kuchapishwa ndipo ukatetee paper yako.Huwa si mchezo....
   
 5. lusungo

  lusungo JF-Expert Member

  #5
  Apr 9, 2015
  Joined: Jan 4, 2014
  Messages: 18,661
  Likes Received: 10,145
  Trophy Points: 280

  Hivi mtu Kama Kitila Mkumbo utamweka ktk kundi lipi? maana anatia Huruma!!!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #6
  Apr 9, 2015
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,220
  Likes Received: 2,447
  Trophy Points: 280
  Jamama ukimuulzia kuhusu Democrasia anakimbilia kusema vyama vinakandamiza democrasia,vyama ni miungu watu etc..huku akipoint cdm km vile ndicho chama tawala,Na hiyo akili yake imeganda hapo hapo...nilitaka kwenda soma paper iliyompatia huo Uprof...itakuwa published wapi..inaweza kuwa inahusu CDM na safai ya Ayatuoullah?au unaweza kuta ni ile paper ambayo Ben saanane anitwa 8 oclock...ile iliyofanya waambie wafunge mlango kwa nje?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #7
  Apr 9, 2015
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,725
  Likes Received: 4,185
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  kwa mara ya kwanza nimeona swala legit kabisa. This is a very good question. It seems kama watanzania tungekuwa tunauliza maswali Kama haya tusingekuwa tunachezewa akili na Hawa Watu wanaojiita wasomi. Kiukweli majority ya PHD holders wetu hawajaandika popote. Wengi ni wasanii tupu. Hata hao associate professors unakuta publications Zao ni kidogo mno na wamepublish kwenye journals za hapa hapa TZ ambazo kiukweli hawawezi kukataliwa. Wengi wanapenda kuitwa Dr? So and so lakini hawajui Kama it requires more to earn that title. The negative side ni kwamba hata watoto wetu tunawafundisha short cuts za maisha. Mf. Sijawahi ona msomi wetu hapa bongo kapublishi kweny journal ya uhakika Kama Harvard Law Review, Yearbook za ukweli....I mean Mifano ni mingi...huko kwenye medics, engineering nk. The point is journals Kama hizi mpaka paper yako ipite Uwe published........unajua kweli....I have earned that accolade. In all wabongo wengi wetu bado sana....ndo maana hata uprofesa wetu ni ujanja ujanja kwa kufahamiana.

  again swala lako ni zuri sana.
   
 8. Mantissa

  Mantissa JF-Expert Member

  #8
  Apr 9, 2015
  Joined: Jul 24, 2010
  Messages: 876
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Wengine huwa naona wanaweka utafiti journal, Dar es salaam. But ni wachache sana. Kuna watu ni asso. prof saa hizi, but hata nitkitafuta kwa jina alichokwisha publish, sipati. Mpaka naduwaaa tu
   
 9. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #9
  Apr 10, 2015
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,220
  Likes Received: 2,447
  Trophy Points: 280
  proplems zinaanzia ktk maeneo km haya..Prof aliyepigika ktk route wanzopitia wengine..utawaona aisee wana mwaga nondo na wanapenda sana kutoa kitu sahihi kwani kinawapa ridhiko na mara nyingi kina mizizi ktk juhudi na ndoto zake ktk kudefend paper zake.Na wengi hupenda paper zao ziwe makini ili zikienda zisirudishwe kwani kurudishwa huwa kunapelekea hata ikishapishwa inakuwa na onyesho hilo.Kitu kinachofanana na kufundishwa au kusaidia.Hii inasaidia sana mtu kujifunza kupeleka kitu sahihi ata the first place.Hapa bongo hata wachambuzi wetu ambazo ndio hawa maprof...huwa wanaingia ktk midahali na fikra au ufahamu wenye mashaka,yaani wafike pale na kua adjust kutokana na changamoto wanayoikuta,wengine pia huweka kwapani walichopanga kuongea wakiona mziki sio.Sasa jiulize wasipopewa ushindani na wasipoongea baada ya kusikia wengine?
   
 10. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #10
  Apr 10, 2015
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,220
  Likes Received: 2,447
  Trophy Points: 280
  Hata vitabu vyao vin amakosa mengi sana ya kifikra, kiuandishi, na hata kimaana.Na waliopitia ku hariri wengine huwa hawaoni kwa sifa zakijinga ziwezi hariri habari ya gwiji..sijui SHivji etc ambao wameshindwa pita test ya hapa JF tuu.
   
 11. K

  Kimweri JF-Expert Member

  #11
  Apr 10, 2015
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 3,998
  Likes Received: 1,095
  Trophy Points: 280
  Bahati nzuri wasomi wengi wa Tanzania wamechukulia PhD zao Ulaya, Asia, na Marekani.

  Grad school yoyote ya Kueleweka duniani ina-tie faculty members wao kufanya publication, hivyo hadi wakati unafanya VIVA si jambo la ajabu kuwa umefanya publication zaidi ya 5, kutokana na uwezo binafsi wa candidate na financial might ya faculty.

  Shida yako unataka publication za kitaaluma ukazitoe kwenye google au JF. Si kila publication iko available to public, some of the most respected journals in the world are members only journals. Hivyo madenge wa kawaida ni ngumu kupata access.

  Pili, kwenye baadhi ya Sekta, hasa sayansi ya jamii, medical research (diseases), Tanzanian academics and research centers are very good.the facilities at Ifakara for example are some of the very best in Malaria research. Kuna sehemu tuko nyuma kama tafiti za Engineering, lakini maprofesa wengi wa TZ wamesoma nje,ambako wamefanya publication kiasi, shida iko kuwa wakisharudi TZ Hakuna funding.

  hivi leo hii serikali ikiambiwa itoe $100M kufanya setup ya telecommunications lab ya kueleweka,in 5 years itatoa hizo pesa?sasa hauwezi kufanya research wakati hauna proper lab setup. Ndio maana unaona wanaishia kufanya market research tu.aka Siasa.

  Kuhusu hivi vyuo vichanga, you may have a point regarding their promotion practices, But there is nothing wrong with receiving promotion faster than another university since in some universities, someone might be an associate professor for longer than another university, because the university does not have enough positions to make him/her a full professor. Remember these universities started from scratch. The issue of being made full professorship hence becomes an administration issue and not an academic one.

  I will give you an example, I work for a world class research company that has lots of Scientists that produces excellent research and are extremely qualified. From time to time big universities in UK and Europe would poach some of them for full professorship positions without having to go through the Senior lecture>Associate Professor>Professor route. Since when you have an opening at a university, you do not look at who is next in line, rather you look for who is the most qualified to lead a department. So, sometimes an expert from industry can catapult from being a Normal PhD guy with no teaching affiliation to being a full professor at a University. It's all based on Qualifications, and what the department is looking for.
   
 12. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #12
  Apr 10, 2015
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,220
  Likes Received: 2,447
  Trophy Points: 280
  Ulichoandika kina ukweli nusunusu na misconceptions nusunusu,,ujumla wake unapelekea kuthibitisha linalotutatiza sana.Sasa km hata hapo UDSM journal yao haina watu wake wa kutosha si shida hiyo? Mfano umetoa IFAKARA km mfano ktk malaria..Ina maana nchi nzima ni malaria tuu ndio inafanyiwa kazi na wataalamu wote wa afya tz na bado Malaria ni issue?Mbaya zaidi bado zinafanywa kwa utaalamu wa nje na fund ya nje,na hata concepts za mwanzo zimetoka nje..na hizo tafiti zipo hata mkoani Tanga...Sidhani km ni lazima serikali tuu ndio iwekeze hela Hizo university zimekosa hata watu wenye akili timamu kuzalisha hela kwa vile havina ubunifu wa kuuza wala patents za maana za kutosha zinazotoka hapo, hazina mbinu wala weledi wakujiongoza kufikia financial stability ans self supporting.Sasa km wamechoka kifikra kihivyo hata serikali ikitoa hela bado wataishia kudai hela za kumaintai hizo lab na kudai speciments..Wenzetu wanatoa tafiti hadi makampuni binafsi yanawekeza sana kwa ubia wenye maana.
   
 13. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #13
  Apr 10, 2015
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,220
  Likes Received: 2,447
  Trophy Points: 280
  Pia nchi nyingine km za East Europe na kwingine walianza kwa kutumia Lab za wenzetu na hata walipoondoka walimaintain link na hivyo wakawa wanapost papers zao kila mara,nahivyo paper zao kuwa dili sana na nyingi zimekuwa patented....wengine makampuni makubwa kuwadhamini ili waende kuunganisha nguvu ktk project kadhaa...au hata kupata access ktk labs.Sasa hawa wetu wakishapa basi wanarudi kuna kuwabania wengine na kutumia hilo gamba kuwa ma ayatoullah z
   
 14. K

  Kimweri JF-Expert Member

  #14
  Apr 10, 2015
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 3,998
  Likes Received: 1,095
  Trophy Points: 280
   
 15. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #15
  Apr 10, 2015
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,220
  Likes Received: 2,447
  Trophy Points: 280
  Naona umeamua fagilia ifakara kwa vile unafanya hapo.Na hiyo kusema nasema kitu nisichokijua ,ndipo unakosea sana.Bora ungetoa maelezo yako yenyewe ndio yaseme km najua au sijui.Hujajibu nilichokuuliza hapa ,Pia Hivi Ina maana watu wote ktk afya mpo kwenye Malaria tuu?Hizo project za malaria wazo la jumla limetoka kwa wenyewe na zinafanyika duniani kote.US wana historia ya kupambana sana na malaria na tafiri wanazofanya duniani kote ili kupata vimelea wa aina zote.Wamarekani waliwahi tuma marine wao kwenda kuiba dawa ya malaria ambayo ilikuwa ikipatikana ktk mmea ambao ulikuwa ukiota china na wachina waliwhai tangaza kuwa wana dawa inayoweza fagia wadudu haraka sana.Kwa US ilikuwa ni kitu cha kutafuta km dhahabu kwa ajili ya askari wao wanaotembea dunia nzima.Waliiweka operation kabisa na wakafanikiwa uiba huo mmea na kuupelea us na kufanya tafiti zote na kupata formula ya hiyo dawa.Unachoongea hapa ni km wakenya na MPESA..huwa wanaamini ni yao na wao ndio wagunduzi....wakati safaricome na wengine wanapigwa sana makato ya royalty ya patent na services.unasema mafua ya ndege...mbona usisem mabusha,ukoma, kukatika pua, makengeza kwa watz watoto na wakubwa..etc?Kuna shida sana jinsi mnavyofikiri...ndio maana mnaita washina na waarabu ndugu zetu..wakati wao hawataki mbegu zenu.Sidhani hata km setting nzima ni idea ya m bongo.Hizo kelele kuwa hata vyuo vya huko haviwezi na huku kuna sales branches ni lame excuses tuu..kwani Bill gate alipoleke miradi ya malaria Handeni na Ifakara Micorsoft walikuwa hata branch ya sales hapa TZ?Makampuni ya kihindi ya kipumbavu tuu yanamwagiwa hela hadi za kufanya upasuaji wa urembo.... Kuna mengi umeongea kutetea roho yako ktk maeneo uliyo na maslahi nayo...hembu nikuulize ktk vyuo vyetu ni ni asilimia ya masomo yanapata external invigilators kutoka hata nje ya east africa? Kuna fani ambazo hazihitaji labs za kutisha ,je ni patents kiasi gani zinafunguliwa pale UDSM?ujue kila tafiti ina nafasi ya kuja patent ambayo ni hela.Watu wengi wanapewa title na Maprof wao,wanaweza endeleza au anza km ni jipya,au wanaweza badilisha.Ku Excel kwa watu km nyie ni kawaida sana kwa vile ni masters wa concepts za watu,hilo halina shida mtacrame mnarudiarusia sana na kuandika vyema hata km hamuani mlichoandika ila baada ya hapo hakitokuwa na connection ktk real practice kwa vile hakina origine ndani yenu.
   
 16. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #16
  Apr 10, 2015
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,725
  Likes Received: 4,185
  Trophy Points: 280
  Nicholas na Kimweri you both have legit points. Lakini kikubwa tufanye investments kwenye research. We can't pretend and use these excuses kwamba hatuna pesa. Mfano ubadhirifu ambao umefanyika pale Ifakara wote tunaujua. Wale siyo wanasiasa ni wasomi.... Most scientists wanashinda kwenye conferences wikitafuna pesa..kiukweli wasomi wetu ingawa ni wasomi, majority research siyo priority. They are there to make money. Ndo maana Nicholas anachallenge hapa tujikite ku address matatizo yanayoikabili jamii yetu. Yes Resources ni Finyu...lakini ndo maana mkaitwa wasomi..muweze kubuni mbinu za kupata resources? Again tukubali bado kwenye publications wasomi wetu wa Kibongo bado sana. Na ninachokiona hatupendi kushughulisha ubongo wetu. By the way faculty nyingi za ulaya na US wana encourage PhDs students wapublish kusudi wauzike wakimaliza shule.......but it's not a condition to get your phd. I have many examples. Jaribu kufanya utafiti wako wa harakaharaka pale mlimani, mzumbe, udom nk.....Angalia associate professors na senior lecturers wamepublish journals gani most recently.......hutaamini macho yako.....ni full ujanja ujanja....
   
 17. baro

  baro JF-Expert Member

  #17
  Apr 10, 2015
  Joined: May 12, 2014
  Messages: 2,055
  Likes Received: 1,315
  Trophy Points: 280
  Dogo acha ubishi ,research nyingi hufanyika na kuwa published kwenye journals na inategemea ni journal ipi kuna journal za kimataifa na aina ya watu n lazima uwe member ,

  Pia kuna IHI, ni moja ya taasisi nzuri sana katika research nenda pale uone acha ubishi, pia kuna vyuo viko kwenye research kila siku mfano SUA na MUHAS wako kwenye research ya Ebola , pia kwa SUA kuna research nyingi sana hufanyika na huendelea kufanyika hivyo usiwadhalilishe maprofesa pia kupata PHD miaka 4 hadi 5 kwa wanaosoma sayansi na kuipata inategemea na facilities zilizopo kwa ulaya n miaka 4 sababu ya facilities na kwa Tanzania inaenda hadi 5 hadi 6 miaka sababu ya uhaba wa facilities ,

  Huo ndio ukweli labda kama una agenda iliyojificha
   
 18. TEKNOLOJIA

  TEKNOLOJIA JF-Expert Member

  #18
  Apr 10, 2015
  Joined: Jan 6, 2014
  Messages: 4,306
  Likes Received: 754
  Trophy Points: 280
  Kimweri akirudi hapa na jibu nitamwona mwanaume wa shoka hasa.umemsambaratisha kabisa ktk hoja ya concepts za kuazima kutoka abroad.
   
 19. zimmerman

  zimmerman JF-Expert Member

  #19
  Apr 10, 2015
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 578
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 80
  Kama mdau wa elimu ya juu, mi sina cha kujitetea hapa. Kiukweli mifumo yetu ya kufanya utafiti katika vyauo vyetu ni duni sana. Na matunda ya tafiti hizo ni duni sawia. Baadhi ya sababu zinazopelekea uduni huo ni za kihistoria lakini zingine ni za kujisababishia hivi karibuni.

  Sababu za kihistoria ni kwamba falsafa na mazingira yaliyoanzisha vyuo vyetu vya kwanza kabisa(UDSM kwa mfano) kufanya tafiti zilizoiva na zenye kutatua matatizo au changamoto halisi za asili katika nyanja zote za maisha haikuwa kipaumbele.

  Vingi vya vyuo hivi katika afrika vilianza kama taasisi za kutengeneza wasomi walau watakaoweza kuchukua nafasi za kiutawala mara baada ya wakoloni kuachia madaraka. Hiyo ndio falsafa, msukumo ulioanzisha vyuo hivi. Liberal arts universities. Na tumebaki katika mfumo huo hadi leo hii. Wasomi wengi usomi wao hutambulika PhD zao zinapowabeba kwenye siasa au kufanya waonekane katika mambo ya kisiasa.

  Tanzania hatujawahi kuwa na vyuo ambavyo uwanzilishi wake kifalsafa(iwe ni mtu binafsi, watu binafsi, au serikali kwa maana ya vision) unalenga utatuzi wa matatizo halisi katika sayansi ya jamii, sayansi ya asili, applied science, na mengineyo.

  Kuwa na msukumo sahihi wa kifalsafa kunapelekea hata aina ya chuo kinavyo operate kufikia malengo yake: namna kinavyoajili lecturers and professors, namna kinavyodahili wanafunzi, namna kinavyotaka wanafunzi wa graduate, namna kinavyotaka kitambulike na kuheshimika, na kadhalika.

  Kwa mfano UDSM au chuo chochote Tanzania, hakina mfumo wa ulipaji mishahara kulingana na ubora wa tafiti za researchers wake. Pale nyote, so long as mnaitwa professors mtakuwa na mshahara mmoja. Uwe professor wa Kiswahili au professor wa medicine. Huyu awe anaingiza grant zero per year, mwingine anaingiza 1 M USD per year. Nyote ni mshahara mmoja.

  Si ajabu UDSM au any other public university for that matter ni vigumu kushawishi watu innovative, wenye IQ kubwa, wenye weledi sawia kubaki bongo kufanya tafiti. Wapo Harvard huko(wakienda kusoma hawarudi), vyuo vya bongo vinabaki na makapi(si tusi mi ni mmoja wao, kama ni tusi najitukana pia).

  Wenzetu msukumo wao ni kuzawadia ubunifu na ubora katika utatuzi wa matatizo halisi, sisi msukumo wetu ni upate PhD ili uitwe msomi miongoni mwa wasiosoma ili useme chochote kizuri kwa watawala ili uwe mmoja wao. Research Intensive universities versus Politically motivated universities!

  Vitu viwili tofauti, matokeo tofauti kabisa.
   
 20. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #20
  Apr 10, 2015
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,139
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  What a good analysis! That's actually what happens in the academic world, Tanzania inclusive.
   
Loading...