Hivi Mamlaka ya Usajili wa Vizazi na Vifo (RITA) Mko Serious kweli?

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
29,451
29,128
Kuna Human Error ila hili la kwenu mmezidi aisee,

Kuna mtoto wa Dada yangu alileta maombi yake ya Cheti cha Kuzaliwa kama miezi kama Saba iliyopita hivi. Baada ya danadana za kama mwezi hivi akapata cheti chake, lakini jina la Babake na Mamá yake wote wakaandikiwa Middle Name na Surname sawa.

Yaan tuseme Kama Baba anaitwa John Joseph Mdangu na Mama anaitwa Janeth Allen Mzava (majina ya kubuni), kwenye cheti waandikwe John Joseph Mdangu na Mamá nae Janeth Joseph Mdangu, as if babake na mamake ni mtu watoto wa baba mmoja.

Baada ya kurudisha hicho cheti akapigwa tena danadana kama mwezi na nusu hivi, kuja kupata cheti Safari hii wametumia middle name na surname ya mamake. Kile cheti akakirudisha tena akapigwa njoo next week za kama miezi miwili hivi, Safari hii wakatoa majina ya wazazi sawa ila la kwake wamekosea, yaani Ni kama vile makusudi wanamfanyia.

Sielewi ni watu hawana weledi na kazi yao ama Vipi, lakini kuna tatizo sana RITA. Inawezekana pia kuna makusudi yanafanyika ili kuhujumu mamlaka au pia tatizo la kuajiri kwa kujuana.

Ukienda pale ukakuta msongamano na ukawauliza tatizo la kila mtu utashangaa. Wakurugenzi wanakaa tu ofisini wanakula viyoyozi badala ya kuja pale pool kutatua changamoto wazipatazo wananchi.
 
Katika taasisi ya umma ambayo hovyo ni RITA haswa ya magomeni kuna dada wa printing nyodo balaa halafu anakosea sana.
Ukitoa rushwa cheti unapata hata siku hiyo hiyo.
Sioni sababu kwa nini vyeti kina mama wasichukue wanapoenda kliniki hospital walipojifungulia.Mama akishajifungua analipa sh3500 ya cheti siku akija kliniki anachukua cheti chake.
Pia mtu mwingine aombe kwa njia ya mtandao mbona unicef mbeya walisajili watoto bure kwa kutumia mtandao na vyeti wakapata?nilitarajia mradi ule uendelee
 
Nilikuwa na plan ya kwenda hapo magomeni kesho,kwa maelezo yako nahisi kubadili upepo,.ila itabidi niende tuu kumuona huyo dada mwenye nyodo zake🤓
 
Katika taasisi ya umma ambayo hovyo ni RITA haswa ya magomeni kuna dada wa printing nyodo balaa halafu anakosea sana.
Ukitoa rushwa cheti unapata hata siku hiyo hiyo.
Sioni sababu kwa nini vyeti kina mama wasichukue wanapoenda kliniki hospital walipojifungulia.Mama akishajifungua analipa sh3500 ya cheti siku akija kliniki anachukua cheti chake.
Pia mtu mwingine aombe kwa njia ya mtandao mbona unicef mbeya walisajili watoto bure kwa kutumia mtandao na vyeti wakapata?nilitarajia mradi ule uendelee
RITA ya mjini hakuna weledi kabisa. Watu wanafanya Kazi kwa kubahatisha na mazoea, mradi mwisho wa mwezi wanadaka salary zao. Ufanyaji Kazi wao ni ishara kua Ajira za kujuana zipo.

Mtu mnarudishwa pale kila wiki Mpaka sasa mnazoeana wenyewe kwa wenyewe, Yaan mkionana tu mnajuana wahanga.
 
Mtoto wa sister Badala ya Male wakaandika Female! Sasa kasheshe nlipokirudisha ili warekebishe....! Sina hamu!
 
RITA pamoto sana asee, binafsi nilienda chukua cheti changu 2014 RITA ya ilala kipindi hiko wapo muhimbili nilisota sana na nikapata lakini pia kilikosewa, nikaenda jaribu kubadili jina nilizungushwa sana. Mara nipeleke cheti cha ndoa ya mzee mara cheti cha kifo ijapokuwa mzee wangu hakuwahi kuwa na docs hizo zote....

Sasa now nafikiria kwenda kutengeneza kipya lakini kwa jinsi navyopata marejesho namna hiyo napata wasi wasi kidogo....
 
Hivi hivyo vyeti c nilisikia wanatoa buree kwenye kituo ulichojifungulia?
 
Ndio Tatizo la kutumia makaratasi kutunza kumbukumbu, kila siku utatengemezewa karatasi lina jina lingine.
 
RITA Arusha , pale kwa mkuu wa wilaya utaratibu ndio hovyo kabisa.... kama unaenda kujaza na kulipia fomu siku nzima itaishia hapo.
 
Back
Top Bottom