Hivi mambo ya Ulinzi ya Muungano inakuwaje Rais wa Zanzibar badala ya Makamu wa Rais anawakilisha Jamhuri?

Screenshot_20210426-153005.jpg

Soma namba 3
 
Naomba kujua Katiba inasema vp hapa? Maana kama Rais wa Jamhuri hawezi kwenda, mbona Makamu wa Rais asimuwakilishe? Je Waziri wa Ulinzi na Waziri wa Mambo ya nje hawawezi kumuwakilisha Rais wa jamhuri wa Muungano kama Rais na Makamu wa Rais hawawezi?

Tusikae kimya tukiona katiba inasiginwa kwa kisingizio Rais wa Zanzibar alikuwa waziri wa Ulinzi na sasa si Waziri wa Ulinzi tena! hapa hii ni insubordination kwa wahusika wanaotambulika Kikatiba.

Kwa hali ilivyo inavyoelekea hata Ushauri wa mambo nyeti ya Muungano mama anaweza kuwa anakwenda kuufuata Zanzibar! si sawa hili kwa maslahi mapana ya Jamhuri ya Muungano.

Katiba inaelezea majukumu ya kila upande na haikai sawa Rais wa serikali ya Zanzibar isiyo na mwakilishi wa Bara ndo anaenda kuongelea masuala ya Ulinzi wa Tanzania, uwiano wa madaraka lazima uzingatiwe kwa maslahi mapana ya nchi.

Mama usituangushe fuata Katiba inavyotaka! Isije ikafika mahali kwenye mambo ya Taharura ya nchi Makamu wa Rais na Waziri wa Ulinzi wakashindwa kutoa maamuzi kikatiba kwa vile mamlaka kapewa Rais wa Zanzibar isivyo.











Nit Picker at best- hakuna maelezo yanayojibu swali lako kwenye katiba ya JMT.
 
Hii ni mara ya pili anafanya hivyo wakati kikatiba rais wa Zanzibar ni waziri katika serikali ya muungano lakini huyu mama ama haelewi au anapotoshwa anapokuwa anamtumna rais wa Zanzibar kwenye maswala muhimu ya muungano.
 
Back
Top Bottom