Hivi mambo ya Ulinzi ya Muungano inakuwaje Rais wa Zanzibar badala ya Makamu wa Rais anawakilisha Jamhuri?

Geza Ulole

JF-Expert Member
Oct 31, 2009
59,032
79,015
Naomba kujua Katiba inasema vp hapa? Maana kama Rais wa Jamhuri hawezi kwenda, mbona Makamu wa Rais asimuwakilishe? Je Waziri wa Ulinzi na Waziri wa Mambo ya nje hawawezi kumuwakilisha Rais wa jamhuri wa Muungano kama Rais na Makamu wa Rais hawawezi?

Tusikae kimya tukiona katiba inasiginwa kwa kisingizio Rais wa Zanzibar alikuwa waziri wa Ulinzi na sasa si Waziri wa Ulinzi tena! hapa hii ni insubordination kwa wahusika wanaotambulika Kikatiba.

Kwa hali ilivyo inavyoelekea hata Ushauri wa mambo nyeti ya Muungano mama anaweza kuwa anakwenda kuufuata Zanzibar! si sawa hili kwa maslahi mapana ya Jamhuri ya Muungano.

Katiba inaelezea majukumu ya kila upande na haikai sawa Rais wa serikali ya Zanzibar isiyo na mwakilishi wa Bara ndo anaenda kuongelea masuala ya Ulinzi wa Tanzania, uwiano wa madaraka lazima uzingatiwe kwa maslahi mapana ya nchi.

Mama usituangushe fuata Katiba inavyotaka! Isije ikafika mahali kwenye mambo ya Taharura ya nchi Makamu wa Rais na Waziri wa Ulinzi wakashindwa kutoa maamuzi kikatiba kwa vile mamlaka kapewa Rais wa Zanzibar isivyo.










 
Yule chawa wa Magufuli anajulia wapi mambo ya ulinzi!
Rais ana mamlaka ya kuweka competent leaders basi kama hao waliopo ni chawa wa Magufuli! Si sawa Rais wa Zanzibar kwenda kwenye mikutano ya Masuala ya Ulinzi yanayohusu Jamhuri wakati Kikatiba ukiacha Rais, na Makamu wa Rais, Waziri wa Ulinzi ni mhusika mkuu wa mambo ya Ulinzi!
 
Rais wa Zanzibar bado ni raia wa Tanzania.

Na rais ana power za kumtuma Mtanzania yoyote kumuwakilisha nje ya nchi kama akijisikia kufanya hivyo
Kikatiba Masuala ya Serikali ya Muungano yapo nje ya mamlaka yake! Ni sawa utume waziri wa Michezo kwenye Mkutano wa Kiusalama SADC! wacheni utani aisee!
 
Mbona huulizi anafanya nini kwenye Baraza la Serikali ya Muungano?
Ndo maana nimekuambia ni sawa kumtuma waziri wa Michezo kwenda kwenye mkutano wa masuala ya Ulinzi wa Kikanda juu ya Ugaidi! Masuala ya Ulinzi Kikatiba Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Muungano anapaswa kuwakilisha! Ni hilo tu, unless kuna yanayoendelea tusiyoyajua yanayolazimisha Hussein Mwinyi Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuchukua Majukumu ya Waziri wa Ulinzi ama Amiri Jeshi Mkuu mama Samia! Plse Katiba ifuatwe, isije ikafika kipindi cha kuhitajika maamuzi Magumu kwa Waziri wa Ulinzi akashindwa kufanya!
 
'Mtu akisha kula nyama ya mtu, haachi hata kidogo!' Sauti ya Kambarage.
Katiba inasemaje? Majukumu ya Waziri wa Ulinzi yafanywe na Waziri wa Ulinzi! Ama basi Katiba ibadilishwe Rais wa Zanzibar awe pia Waziri wa Ulinzi wa serikali ya Muungano!
 
Ndo maana nimekuambia ni na sawa kumtuma waziri wa Michezo kwenda kwenye mkutano wa masuala ya Ulinzi wa Kikanda juu ya Ugaidi! Masuala ya Ulinzi Kikatiba Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Muungano anapaswa kuwakilisha!
Mwinyi ni Cabinet member, ni rais wa upande mmoja wa Muungano, pia amekuwa waziri wa ulinzi kwa muda mrefu sana.

Ukisema kikatiba, leta kifungu cha katiba.
 
Kama alipokuwa tume ya mipango aliboronga, akawa waziri wa fedha akawa anapika takwimu (fake data) sasa kwenye ulinzi si ataliangamiza Taifa?
Zabayanga Hatoshi
Anajifanya Kumtanguliza Mungu
Hana Lolote
Kupika Data
 
Mjumbe wa baraza la mawaziri la Muungano na Rais wa SMZ serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mh. Dr. Hussein Mwinyi mwezi April 8, 2021 aliongoza ujumbe wa Tanzania uliojumuisha waziri wa mambo ya nje Dr. Liberata Mulamula ktk kikao cha dharura Maputo Mozambique. Dr. Hussein Mwinyi aliwahi kuhudumu kama waziri wa ulinzi wa serikali ya Muungano kabla ya kuchukua nafasi ya Urais SMZ November 2020

8 Apr 2021
SADC Double Troika Session address by President of Mozambique

Source : GovernmentZA
 
Katiba inasemaje? Majukumu ya Waziri wa Ulinzi yafanywe na Waziri wa Ulinzi! Ama basi Katiba ibadilishwe Rais wa Zanzibar awe pia Waziri wa Ulinzi wa serikali ya Muungano!
Kilaza katika ubora wake!
 
Katiba inasemaje? Majukumu ya Waziri wa Ulinzi yafanywe na Waziri wa Ulinzi! Ama basi Katiba ibadilishwe Rais wa Zanzibar awe pia Waziri wa Ulinzi wa serikali ya Muungano!
Na maanisha mtu atendaye jambo lolote kinyume na taratibu, usitegemee kumuona akibadilika.
 
Rais ana mamlaka ya kuweka competent leaders basi kama hao waliopo ni chawa wa Magufuli! Si sawa Rais wa Zanzibar kwenda kwenye mikutano ya Masuala ya Ulinzi yanayohusu Jamhuri wakati Kikatiba ukiacha Rais, na Makamu wa Rais, Waziri wa Ulinzi ni mhusika mkuu wa mambo ya Ulinzi!
Waziri wa Ulinzi ni Ceremonial Figure hata VP mwenyewe yupo yupo tu unless litokee kama lilotokea kwa mwendazake
Infact Cheo cha VP na Minister of Defence kwa muundo wetu vipo vipo tu na ukikaa vibaya wengi wanakuvimbia tu , JR ame serve for a while na ana security clearance kubwa tu
 
Back
Top Bottom