Hivi makusanyo ya jiji la Dodoma inawezekanaje yakazidi ya Dar es Salaam?

Kikiwo

JF-Expert Member
Nov 30, 2017
1,967
1,046
Wana JF naomba msaada katika kujua haya mapato yanapimwaje? Eti Dodoma imekusanya Tsh 70Billion na ikawa ya kwanza alafu Dsm kwenye viwanda kibao eti mapato Tsh 50 Billion.

Nashindwa kuelewa kwani Dodoma kuna viwanda na vitega uchumi kuliko Dsm au Arusha hata Mwanza?
 
Wana JF naomba msaada katika kujua haya mapato yanapimwaje? Eti Dodoma imekusanya 70Billion na ikawa ya kwanza alafu Dsm kwenye viwanda kibao eti mapato 50 Billion. Nashindwa kuelewa kwani Dodoma kuna viwanda na vitega uchumi kuliko Dsm au Arusha hata Mwanza?
Bongo wajanja wengi, upigaji mwingi
 
Wana JF naomba msaada katika kujua haya mapato yanapimwaje? Eti Dodoma imekusanya 70Billion na ikawa ya kwanza alafu Dsm kwenye viwanda kibao eti mapato 50 Billion. Nashindwa kuelewa kwani Dodoma kuna viwanda na vitega uchumi kuliko Dsm au Arusha hata Mwanza?

Ni kweli inawezekana kabisa.

1. Mapato ya Jiji la Dar ( Kutokana na vyanzo vilivyoahinishwa) hayajumuishi mapato ya manispaa tano za Dar. Hii maana yake ni kuwa mapato ya manispaa za ilala, ubungo, kigamboni, kinondoni na temeke hayapo katika mapato yaliyokubalika ya jiji la Dar.

2. Jiji la Dom limepata mapato makubwa kutokana na uuzaji wa viwanja na ongezeko la biashara na wageni wengi walioingia mji huo. Hapo hujaweka vyanzo vya kawaida vya halmaishauri ambapo kwa halmashauri ya jiji la Dar vipo ' limited's

Hii inaweza kuwa sababu kubwa ya hicho unachoona. Wadau wengi wenye taarifa sahihi zaidi watakuelewesha.
 
Huwa kuna lengo au target huwekwa ,ukishindwa kukukusanya kufikia lengo, huhesabika kushindwa,sasa Dodoma ilikusanya na kuvuka lengo lililowekwa.

Ni kweli mapato ya Dar yanaizidi Dodoma kwa mbali sana ,ispokua lengo walilowekewa Dar hawakulifikia ,logic iko hapo
 
Pato kubwa linalotegemewa na jiji ni
1. Ubungo terminal
2. Machinga na
3. Parking za magari
Mapato mengine ni ya manispaa 5.
Lakini Dodoma ni nji mzima unaweka vyanzo vyote bila kugawana na manispaa.
 
Ni kweli inawezekana kabisa.

1. Mapato ya Jiji la Dar ( Kutokana na vyanzo vilivyoahinishwa) hayajumuishi mapato ya manispaa tano za Dar. Hii maana yake ni kuwa mapato ya manispaa za ilala, ubungo, kigamboni, kinondoni na temeke hayapo katika mapato yaliyokubalika ya jiji la Dar.

2. Jiji la Dom limepata mapato makubwa kutokana na uuzaji wa viwanja na ongezeko la biashara na wageni wengi walioingia mji huo. Hapo hujaweka vyanzo vya kawaida vya halmaishauri ambapo kwa halmashauri ya jiji la Dar vipo ' limited's

Hii inaweza kuwa sababu kubwa ya hicho unachoona. Wadau wengi wenye taarifa sahihi zaidi watakuelewesha.
Rudi skuli mazee

Watu kama ninyi ni laana kwenye jamii
 
Na NBAA wamepitia hii standard mpya???
 
Pato kubwa linalotegemewa na jiji ni
1. Ubungo terminal
2. Machinga na
3. Parking za magari
Mapato mengine ni ya manispaa 5.
Lakini Dodoma ni nji mzima unaweka vyanzo vyote bila kugawana na manispaa.

Sahihi kabisa. Watu wakisikia jiji wanaunganisha na vyanzo vya manispaa nyingine hawaelewi kuwa karibu manispaa zote za Dar zimelizidi jiji la Dar kwa mapato. Ilala peke yake ina kama 44bn
 
Ni kweli inawezekana kabisa.

1. Mapato ya Jiji la Dar ( Kutokana na vyanzo vilivyoahinishwa) hayajumuishi mapato ya manispaa tano za Dar. Hii maana yake ni kuwa mapato ya manispaa za ilala, ubungo, kigamboni, kinondoni na temeke hayapo katika mapato yaliyokubalika ya jiji la Dar.

2. Jiji la Dom limepata mapato makubwa kutokana na uuzaji wa viwanja na ongezeko la biashara na wageni wengi walioingia mji huo. Hapo hujaweka vyanzo vya kawaida vya halmaishauri ambapo kwa halmashauri ya jiji la Dar vipo ' limited's

Hii inaweza kuwa sababu kubwa ya hicho unachoona. Wadau wengi wenye taarifa sahihi zaidi watakuelewesha.
Mku sijakuelewa katika point yako namba 1. Sasa kama mapato ya manisipaa zote 5 za Dsm hayahesabiki, kwahiyo manisipaa ipi nyingine ya mkoa wa Dsm inayohesabika katika taarifa ya mapato hayo?
 
Pato kubwa linalotegemewa na jiji ni
1. Ubungo terminal
2. Machinga na
3. Parking za magari
Mapato mengine ni ya manispaa 5.
Lakini Dodoma ni nji mzima unaweka vyanzo vyote bila kugawana na manispaa.
Kwani Dodoma haina manisipaa zilizogawanyika? Kama ni hivyo, kwanini majiji mengine kama Arusha, Mwanza, Mbeya, Dsm waliweka utaratibu wa kugawanya manisipaa? What is the logic behind this?
 
Rudi skuli mazee

Watu kama ninyi ni laana kwenye jamii
tatizo la shule ada ukimlipia anaweza kurudi lakini sidhani kama ni busara kwa swala la kutojua kitu ikawa ni laana kwa jamii kwa kuwa si kila mtu anajua kila kitu. yeye amaetoa mawazo yeke kwa kadri anavyoelewa sasa ni vizuri ukatueleza wewe kwa usahihi zaidi tukaelewa
 
Mku sijakuelewa katika point yako namba 1. Sasa kama mapato ya manisipaa zote 5 za Dsm hayahesabiki, kwahiyo manisipaa ipi nyingine ya mkoa wa Dsm inayohesabika katika taarifa ya mapato hayo?

Mkuu ishu IPO hivi;
1. Hilo jiji la Dar unavyowaza kichwani mwako sio Jiji la Dar linalozungumziwa katika taarifa ya mapato ya tamisemi. Nadhani unapowaza Jiji unafikiria zile manispaa tano, hiyo sio sahihi.
2. Jiji la Dar katika tamisemi ni taasisi peke yake na inatengenishwa na manispaa zake kiutawala na kiutendaji. Jiji linasimamia mambo mbalimbali ya jiji la Dar kwa ujumla wake lakini haihusiki na mapato yanayopatikana katika manispaa zake isipokuwa tu pale ilipokubaliwa.
3. Hivyo basi, mapato ya jiji la Dar ukijumlisha manispaa zake kiuhalisia ni makubwa kuliko sehemu zozote Tanzania ila kama nilivyosema mwanzo kwa tamisemi manispaa ni manispaa na jiji ni jiji.
 
Kwani Dodoma haina manisipaa zilizogawanyika? Kama ni hivyo, kwanini majiji mengine kama Arusha, Mwanza, Mbeya, Dsm waliweka utaratibu wa kugawanya manisipaa? What is the logic behind this?

Kwa Dodoma ile iliyokuwa manispaa mfano chukulia ilala yenye vyanzo vyote vya mapato ndiyo imekuwa jiji. Ikiwa mji utakua sana zitazaliwa manispaa nyingine ambazo zitajitenga toka Dodoma jiji japo zote zitabaki katika mkoa wa Dom
 
Wana JF naomba msaada katika kujua haya mapato yanapimwaje? Eti Dodoma imekusanya Tsh 70Billion na ikawa ya kwanza alafu Dsm kwenye viwanda kibao eti mapato Tsh 50 Billion.

Nashindwa kuelewa kwani Dodoma kuna viwanda na vitega uchumi kuliko Dsm au Arusha hata Mwanza?
Mapato ya Dodoma yanayoelezwa kupanda ni ya msimu mfupi tu.Sasa hivi Jiji la Dodoma lina mradi wa kupima na kuuza viwanja yakiwa ni maandalizi ya kulijenga Jiji hilo upya.Kufuatia zoezi hilo, maelfu ya Watanzania wameitikia wito wa kununua viwanja.Hivyo mara watakapomaliza biashara hiyo, wataporomoka na kuwa wa mwisho kimapato.Ukitaka kulithibitisha hilo waambie wataje chanzo na sababu ya mapato yao kupaa.
 
Ni kweli inawezekana kabisa.

1. Mapato ya Jiji la Dar ( Kutokana na vyanzo vilivyoahinishwa) hayajumuishi mapato ya manispaa tano za Dar. Hii maana yake ni kuwa mapato ya manispaa za ilala, ubungo, kigamboni, kinondoni na temeke hayapo katika mapato yaliyokubalika ya jiji la Dar.

2. Jiji la Dom limepata mapato makubwa kutokana na uuzaji wa viwanja na ongezeko la biashara na wageni wengi walioingia mji huo. Hapo hujaweka vyanzo vya kawaida vya halmaishauri ambapo kwa halmashauri ya jiji la Dar vipo ' limited's

Hii inaweza kuwa sababu kubwa ya hicho unachoona. Wadau wengi wenye taarifa sahihi zaidi watakuelewesha.
Hata ikiwa hivyo kwa namna yeyote ile haiwezekana Halmashauri ya Jiji la Dodoma ikazidi Halmashauri ya Ilala, Ndio maana tunaambiwa tuna cook data
 
Back
Top Bottom