Hivi Makonda alipokuwa anatenda uhalifu wake viongozi wakuu wa Nchi kama Rais na Waziri Mkuu hawakuwa na Taarifa? Hawakujua ama hawakufahamu?

najaribu kumfwatilia kigogo 2014
ili nijue kinachoendelea huko magogoni
baada ya ripoti ya pompeo lkn simwoni au Bashite kesha mla kichwa?
 
Makonda hakuna anayempenda ndani ya Serikali. Kuanzia Makamu wa Raisi, Waziri Mkuu, Mawaziri, wakuu wa Mikoa wenzake hadi watendaji wakuu wa serikali ikiwemo vyombo vya dola.

Hata kwenye Chama hawamtaki na ameonywa hadi na Katibu Mkuu wa Chama. Shida ni mamlaka ya uteuzi wake na isiwe tabu kuliko CCM kupoteza kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu au Taifa kuingia kwenye economic crisis ni bora waende yeye na ayembeba. Hata Jumbe alikuwa one term president Zanzibar

Pole sana. Huna hoja. Economic crisis GANI. Unadhani ukipendwa na USA Mwananchi wa kawaida atapona. Nichts ist gratis im Leben.
 
Ikiwa kama Paulo Makonda ametenda unyama uliotajwa na Serikali ya Marekani na ambao umepelekea kudhalilisha nchi yetu kuliko ilivyowahi kudhalilishwa tangu Mungu aumbe mbingu na ardhi, nina swali dogo sana la kuuliza.

Je alipokuwa anatenda uhalifu huo viongozi wakuu wa nchi hii akiwemo Rais, Makamu wake na Waziri Mkuu hawakujua ? Je viongozi wa idara za Usalama wa Nchi nao hawakujua? ikiwa kama raia ambaye hakuwahi hata kuhudhuria mafunzo hata ya JKT au Mgambo anaweza kutenda mambo mabaya kiasi hiki na vyombo vya usalama vikashindwa kumuona hadi waone wazungu basi nchi yetu inahitaji huruma ya Mungu.

Vinginevyo Serikali ya Tanzania ikanushe jambo hili na kuitangaza Marekani kama Taifa la waongo wakubwa ili dunia ituelewe

Hhaiwezekani jambo kubwa la kudhalilisha nchi kama hili likapita bila kujadiliwa, hatulengi kutukana wala kuhatarisha chochote, hii ni kwa sababu kilichotajwa kufanywa na Makonda ndio cha hatari zaidi kwa Taifa letu kuliko kuhoji

Naomba kuwasilisha
Nisaidie tafadhali.Kwani wazungu wamesema amefanya nini kibaya hivyo huyu makonda b.Tujuze kidogo
 
Pole sana. Huna hoja. Economic crisis GANI. Unadhani ukipendwa na USA Mwananchi wa kawaida atapona. Nichts ist gratis im Leben.
South Korea anapendwa na USA. Hali ya uchumi na ya mwananchi wa Kawaida ikoje??

Singapore anapendwa na USA. Hali ya kiuchumi na ya mwananchi wa kawaida ikoje?

Taiwan anapendwa na USA, hali ya kiuchumi na ya mwananchi wa Kawaida ikoje?

Kuwait anapendwa na USA, hali ya kiuchumi na ya mwananchi wa kawaida ikoje?

Israel anapendwa na USA, hali ya kiuchumi na ya mwananchi wa kawaida ikoje?

Qatar anapendwa na USA, hali ya kiuchumi na ya mwananchi wa kawaida ikoje?

Saudi Arabia anapendwa na USA, hali ya kiuchumi na ya mwananchi wa kawaida ikoje?

Jordan anapendwa na USA, hali ya kiuchumi na ya mwananchi wa kawaida ikoje?

Punguza ujinga ndugu. CCM mnapata wapi vijana wa namna hii?
 
Makonda ametenda uovu wake wote kwa baraka za Rais Magufuli, haiwezekani Makonda afanye uhalifu wake huku akilindwa na walinzi wa kikosi maalum cha Rais (PSU) halaf eti Rais asijue....afterall Rais amemsifia mara kwa mara kuwa anafanya "KAZI NZURI" na akamtaka aendelee "KUCHAPA KAZI".

Magufuli anajua kila kitu
Umemaliza kila kitu,thread iishie hapa.
 
Ikiwa kama Paulo Makonda ametenda unyama uliotajwa na Serikali ya Marekani na ambao umepelekea kudhalilisha nchi yetu kuliko ilivyowahi kudhalilishwa tangu Mungu aumbe mbingu na ardhi, nina swali dogo sana la kuuliza.

Je alipokuwa anatenda uhalifu huo viongozi wakuu wa nchi hii akiwemo Rais, Makamu wake na Waziri Mkuu hawakujua ? Je viongozi wa idara za Usalama wa Nchi nao hawakujua? ikiwa kama raia ambaye hakuwahi hata kuhudhuria mafunzo hata ya JKT au Mgambo anaweza kutenda mambo mabaya kiasi hiki na vyombo vya usalama vikashindwa kumuona hadi waone wazungu basi nchi yetu inahitaji huruma ya Mungu.

Vinginevyo Serikali ya Tanzania ikanushe jambo hili na kuitangaza Marekani kama Taifa la waongo wakubwa ili dunia ituelewe

Hhaiwezekani jambo kubwa la kudhalilisha nchi kama hili likapita bila kujadiliwa, hatulengi kutukana wala kuhatarisha chochote, hii ni kwa sababu kilichotajwa kufanywa na Makonda ndio cha hatari zaidi kwa Taifa letu kuliko kuhoji

Naomba kuwasilisha
Lakini pia la kujiuliza Ni kwamba vyombo vya ulinzi na usalama vilikuwa wapi?
 
Kwa hiyo, kwa maelezo yake haya hataki matatizo yetu ikiwemo ukiukwaji wa haki za binadamu ikiwemo kutekana na watu kupigwa risasi na ukandamizwaji wa demokrasia ujulikane huko nje? Alitaka watu wapotee na kuumia kimnya kimnya? Kwa faida ya nani?
Toka maktaba
August 18, 2019

Mabalozi wa Tanzania tuna wakati ngumu

Dr. Wilbroad Slaa ambaye ni balozi wa Tanzania nchini Sweden : Maajabu zaidi yanakuja, wenzetu wana maadili na demokrasia. Dr. Slaa anasema wao kama wawakilishi wa Tanzania nje ya nchi wanapata wakati ngumu sana kutetea nchi kwa vile 'wapinzani' wanatoa siri za matatizo ya haki za binadamu na demokrasia nje kwa wadau wa maendeleo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo la Magufuli anauishi utoto wake katika utu uzima wake.

Wenzao wanavyofanya ni hivi.

Mkubwa anabariki mambo kimyakimya, halafu ana ji distance. Kiasi kwamba, yakiharibika, anakuwa ana kauwezo fulani hivi ka kukana kwamba alijua watu wakamuamini.

Ndipo hapo utakaposikia habari za "Rais ana nia nzuri, lakini washauri wake wanamuangusha".

Kumbe walikula njama wote. Kwa kuelewa kwamba, rais asiwe exposed, kwa sababu ni mtu muhimu sana, hayupo disposable, hawa wa chini hata wakiwa exposed, inaweza kuonekana wamefanya kwa siri bila kumshirikisha rais.

Ndivyo wajanja wanavyofanya hivyo, inaitwa "plausible deniability". Yani, kukataa jambo ambako kunaweza kukubalika kwamba ni kweli.

Sasa huyu Magu yeye hana breki ya mdomo. Rais anamwambia Spika waziwazi "washughulikie bungeni, tutawashughulikia nje huku".

Rais anasema atawapiga wapinzani mpaka shangazi zao.

Hata siku mambo yakibumbuluka, kujitetea kwamba yeye hakuwahi kuwa na nia ya kuwadhuru wapinzani hawezi.

Kuna makala moja ya Washington Post iliwekwa hapa inasema Magufuli hana "plausible deniability" kwa mabaya aliyotenda Makonda na yanayotokea nchini.

Magufuli is a country bumpkin.

And maybe, at this point, that is not a bad thing.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom