Hivi Makao Makuu ya nchi ni Chato au Dodoma? Mzee anatuchanganya

Matumizi mabaya tu ya kodi zetu, ingekua pesa yake asingetumia hovyo hovyo hivi.
Tatizo ni hawa MaCCM yanamvimbisha zaidi lile bichwa, wamezidi UPUMBAVU. Anawaita WAPUMBAVU wake.
Wamebaki kusujudia kila aina ya ujinga aufanyao.
Nchi ya wajinga sana hii
 
technically,
kumbuka huyu ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ofisi,makazi ya rais ni ikulu na karibia kila mkoa na baadhi ya wilaya kuna ikulu rasmi hivyo anaweza kufanya kazi kutokea popote katika jamhuri hii ya tanzania. nakubali kukosolewa.
 
Toka Rais Magufuli aamue kwenda kijijini kwake Chato kwa mapumziko, tumeshuhudia ziara za mfululuzo za viongozi wa nje kuja nchini kwetu.

Hatukuziona ziara hizo alipokuwa Dar wala alipohamia Chamwino-Dodoma, ambako ndiko tuliambiwa kuwa ndiyo makao makuu ya nchi kwa hivi sasa, lakini tunaziona ziara hizo zikifululiza alipokwenda Chato!

Tumeshuhudia ziara ya waziri wa nje wa China na ujumbe wake mzito wakifanya ziara yake huko Chato.

Baadaye tumeshuhudia ziara ya Rais wa Msumbiji naye akifanya ziara ya kiserikali huko Chato na hapo jana tukamuona Rais wa Ethiopia na ujumbe wake nao wa kifanya ziara yao huko Chato.

Wananchi tunachojua ni kuwa makazi ya Ikulu yalikuwa Dar na hivi sasa yamehamishiwa rasmi huko Dodoma na wala hatujajulishwa kuwa huko Chato ndiyo makao makuu ya nchi kwa hivi sasa

Ni kwanini hivi sasa tunaona shughuli zinazoendelea za kiserikali huko Chato, kama ndiyo makao makuu ya nchi yasiyo rasmi?

Hatujui kama huko Chato nako kumeongezwa miongoni ya makao makuu ya nchi kwa hivi sasa.

Tufahamu kuwa kuna madhara makubwa kiuchumi kwa shughuli zinazoendelea huko Chato kwa hivi sasa, kwa kuwa kila unapokuja ugeni toka nje ya nchi, viongozi waandamizi wa serikali "wanayahama" makazi yao rasmi ya Dodoma na kwenda Chato, ambako kunaliingizia hasara kubwa Taifa hili kiuchumi.

Hebu tufikirie ni mafuta ya kiasi gani yanaunguzwa na viongozi hao wa kiserikalikwenye magari yao ya kifahari ya kwenda huko Chato?

Vile vile tufikiri ni per diem kiasi gani inayolipwa kwa viongozi hao kwa kuwa nje ya vituo vyao vya kazi?

Ninavyofahamu Mimi ni kuwa mkakati huo umepangwa mahsusi kwa ajili ya kuufanyia "promotion" hiyo Chato na kuzijaza Hoteli za huyo Jiwe huko Chato, lakini unaliingizia hasara kubwa kama nchi kiuchumi na ifahamike pia gharama zote hizo anayezibeba ni mwananchi wa kawaida Mimi na wewe kutokana na kodi tunayoilipa serikali hii!

Hayo ni matumizi mabaya kabisa ya rasilimali zetu ambapo tunapaswa wananchi wote tuzikemee kwa nguvu zetu zote ili zikomeshwe
 
mwacheni ajenge uchumi wa kwao,bahati nzuri hajaenda "kuzurura" huko nje ambako gharama zake zingekuwa mara dufu!
acha watu wale,ulitaka wale akina nani hiyo pesa?
ulitaka wale watu wachache kwa singizio cha kuzurura huko nje?
hii hela si inabaki hapa hapa?
we subiria tu,nikiwa rais,iramba inakuwa ni mkoa,anayo yafanya magufuli yatakuwa ni cha mtoto!
 
Sielewi ziara za viongozi wakubwa zote Chato.

Naona harakati za kuikuza Dodoma zinadumaa kwa style hii.

Na kwa style hii tunachanganya watendaji hatujui nguvu waeke wapi Dodoma au Chato?

Kuna muda itafika tutawalaumu mawaziri na manaibu wao bure tu.

Naendelea kuuliza je mipango hii ilikuwepo kwenye bajeti iliyopita?

Mi nadhani hili jambo la umimi sio sawa kwasababu kila rahisi angejenga kwao kuna mikoa ingekuwa mapori hadi leo

View attachment 1151860
Hapo ni ikulu ya chatou
 
Back
Top Bottom