Hivi mahindi ndio kipimo cha njaa au chakula kuwepo nchini?

Maghayo

JF-Expert Member
Oct 5, 2014
13,672
28,970
Mzuka wanajamvi!

Serikali au wadau mbalimbali wakitoa data kuhusu upungufu ama chakula kuwepo wanatumia mahindi. Baa la njaa ikiikumba nchi mahindi yanatumiwa kama kipimo cha chakula pekee kuonesha kama kuna njaa au la. Tuna ona serikali kupitia wizara ya kilimo inanunua mahindi tu meengii nakuagiza mengine kuepusha njaa.

Sasa najiuliza mahindi peke yake ndio chakula cha Mtanzania anakula. Mbona serikali hainunui mazao mengine mengi? Pia vyakula vingine kwanini visitumike kwa kupima hali ya chakula nchini?

Kuna ngano, mchele na cereals zingine maharage n.k ambazo zinaliwa sana na Watanzania. Kwa nini iwe mahindi tu?
 
Ukishakuwa na pumba za kutosha umemaliza njaa ya nguruwe. Serikali wanajua ukishakuwa na mahindi basi njaa ya watanzania imekwisha.

Pia ukishawachimbia watanzania visima vya maji vya mdundiko umemaliza tatizo la maji. Na wanaharakati dawa yao polisi.
 
Mkuu mbona wali na vyakula vya ngano vinalika sana.
Havijazidi ugali ila, ngano huko ndani ndani kuna wengine inaweza kukata hata mwaka hajagusa chakula kilichotengenezwa kwa ngano ila ugali kwa wengi kukata mwezi tu bila kuugusa ni ngumu
 
Mkuu Kumbuka pia watu wengi sana siku haipiti bila kula wali
Kwa miaka mingi wali ni chakula cha matajiri. Katika historia ya mpunga ulijiotea katika mabonde ya milima China na Brazil.

China walijiongeza kulima na kupanga mpunga kwa jembe la mkono. Mpungunga enzi hizo ulikua ni nafaka ya tunu iliyotajirisha wafanya biashara na kuliwa na wafalme pamoja na matajiri. Watu wengi walikula wali siku za sikukuu tu.

Mapinduzi ya kilimo pamoja na njia rahisi za usafiri kumebadili taswira nzima ya mchele, sasa unaonekana ni chakula cha kawaida.
 
Mkuu Kumbuka pia watu wengi sana siku haipiti bila kula wali
Watu wengi wangapi wanazidi wala ugali?
Hauko Tanzania mkuu
We unajua kuna watu wanakula wali jumapili hadi jumapili na wengine itokee bahati tu
 
Jirani yetu anakula wali kama kiburudisho, akiwa na njaa anakula kwanza ugali mpaka akikaribia kushiba ndio anagonga wali, anadai wali hua haukai tumboni, akila wali pekee hua haimalizi nusu saa anasikia njaa.
 
Huyo keshajiroga kisaikolojia isee!

Lakini si huyo tu, wengi wana imani sana na ugali!

Ukifuatilia kitaalamu, "food value" ya unga wa mahindi haizidi "food value" ya ngano, ulezi, mchele, mtama na uwele.

Kwenye kundi la vyakula vya nafaka, mahindi ni ya mwisho kwa thamani.

Sema tu watu wanasifu ugali kwa ajili ya mazoea na si kwamba vyakula ambavyo si ugali havishibishi hizo ni dhana tu.
 
Na ndio maana nchi za wenzetu mahindi yanatumika sana kwenye malisho ya mifugo kuliko matumizi ya binaadamu.
 
Ukitaka kujua thamani ya mahindi katika uchumi na kukabiliana na njaa jikumbushe miaka ya 70 na 80 wakati wa ukame mahindi ya njano kutoka Marekani yalivyookoa maisha! Pia kumbuka Zimbabwe ilivyoteseka miaka ya 80!
 
Back
Top Bottom