Hivi mahari wakati wa ndoa siyo biashara ya Utumwa/binadamu?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,162
12,640
Wakuu hivi hii ishu ya mahari siyo biashara ya utumwa kweli. Maana wazazi wanampa kijana binti kisha wao wanachukua ng'ombe, mashuka, mablanketi, pesa na vikorokoro vingine.

Bila kulipa hii mali huruhusiwi kuondoka na binti yao. Na siku nyingine ikitokea binti kateswa, akirudi kwao huwa wanamwambia kuwa tumeshakula mali ya watu, rudi kavumilie. Wengine wamefikia hadi kuozesha mabinti ambao hawajakomaa kisa wapate mahari.

Mahari ina tofauti gani na biashara ya utumwa/binadamu?
 
Itakuwa biashara na utumwa kama mahari itapewa kipaumbele zaidi kuliko utu, ubinadamu na haki za msingi za kijana husika kujiamulia amwoe au aolewe na nani.

Maamuzi haya yakifanywa kwa kigezo cha pesa na uchu wa kujikweza & kujitajirisha at the expense ya mambo-msingi haya, bila shaka huwa utumwa mkubwa usiopaswa kuvumilika.
 
Mkuu kidini ya Uislamu!

Mahari ni zawadi ya binti inayompasa aipokee kutoka kwa mumewe!

Hivyo basi kulingana na sheria ya uislamu ni haramu au haipaswi kwa mzazi au mlezi kuhitaji chochote kutoka kwa muoaji!

Narudi, kwa sharia za Kiislamu Mahari ni zawadi anayopewa binti anayetakiwa kuolewa!

Mzazi kutaja mahari ni sawa na kumuuza binti
 
Itakuwa biashara na utumwa kama mahari itapewa kipaumbele zaidi kuliko utu, ubinadamu na haki za msingi za kijana husika kujiamulia amwoe au aolewe na nani. Maamuzi haya yakifanywa kwa kigezo cha pesa na uchu wa kujikweza & kujitajirisha at the expense ya mambo-msingi haya, bila shaka huwa utumwa mkubwa usiopaswa kuvumilika.
Siku hizi hali imebadilika lakini vijijini bado ipoipo. Wazazi wanakubaliana na muoaji na kuchukuwa mahari na binti anataarifiwa tu kuwa mumeo ni huyo. Wale wa vijijini wanaooa mabinti wa shule za msingi unafikiri mabinti wale wanauhuru wa kuchagua?
 
Siku hizi hali imebadilika lakini vijijini bado ipoipo. Wazazi wanakubaliana na muoaji na kuchukuwa mahari na binti anataarifiwa tu kuwa mumeo ni huyo. Wale wa vijijini wanaooa mabinti wa shule za msingi unafikiri mabinti wale wanauhuru wa kuchagua?
Ndiyo maana Baba wa Taifa aliaidentifai maadui wakuu wa nchi yetu (na kwa kweli, maadui wanaoitesa dunia nzima) --- UJINGA, MARADHI & UMASKINI.
 
Wanaoharibu ni hawa wazazi wa siku hizi mahari wanataja wao, badala ya muolewaji, aliyeweka sheria ya mahari ni mungu aliyetuumba, "katu siwezi kumuhoji baba yangu kwanini anataka saa 12 jioni niwe ndani, ni sheria kaweka yeye kwa hekima zake pana"

Mungu ndio aliyesema tuwape wanawake mahari yao, mahari ni ZAWADI ya muolewaji, kuna kahekima fulani kamefichika, mie ngumu kukapata, mwanamke kukwambia mie nataka laki 1, tuchukulie mwanamke akwambie zawadi yangu(mahari) yangu ni ngozi ya chui, ukaenda ukaipata kuna uanaume fulani unajihisi, ama aombe umchunie ngozi ya mbuzi kisha umtengenezee kiti wewe mwenyewe,kuna ushujaa fulani,kuna kafaraja fulani hivi, shida tupo kwenye zama za "PESA NDIO KILA KITU"

Hivyo mahari imekuwa zawadi ya pesa, na tukitoa pesa ni sawa na kununua kwa uelewa wa haraka haraka.
Shida tunachagua kufanya jambo bila kufata misingi yake, tunataka kufunga ndoa, je nani katwambia tufunge ndoa, kama tunafunga ni kwa utaratibu upi na masharti yapi, sio tunachagua sheria fulani sababu inatupendeza machoni tunaacha yale tunaona yanatukwaza

Kuna elimu pana sana, mengine yako juu ya uwezo wangu.
 
Wanaoharibu ni hawa wazazi wa siku hizi mahari wanataja wao, badala ya muolewaji, aliyeweka sheria ya mahari ni mungu aliyetuumba, "katu siwezi kumuhoji baba yangu kwanini anataka saa 12 jioni niwe ndani, ni sheria kaweka yeye kwa hekima zake pana"...
Hakuna mahali popote Mungu aliagiza mwanaume atoe mahali ndo apate mke ,ni tamaduni tuu kama mwanamke kupiga magoti anaposalimia.
 
Kila kitu kinategemea mtu unakionaje. Mahari kwangu mimi naiona kama appreciation kwa familia ya binti kwa kumtunza binti mpaka akafikia hatu wewe ukamuona anafaa kuanzisha naye familia.
 
Mahari ni heshima kwa tamaduni zetu za kiafrika kuonyesha thamani ya mkeo na kutoa angalau fadhila kwa wazazi wake.Kwa nyie mliokulia 'kwa malkia' hamuwezi elewa.

Aminini nawaambia huwezi kufananisha ndoa iliyofungwa kwa kufuata taratibu zote (kulipa mahari) ,na kubebabeba kusikoeleweka.
 
Kila kitu kinategemea mtu unakionaje. Mahari kwangu mimi naiona kama appreciation kwa familia ya binti kwa kumtunza binti mpaka akafikia hatu wewe ukamuona anafaa kuanzisha naye familia.
Appreciation huwa haupangiwi bali unatoa kwa hiyari yako na pia appreciation si lazima kutoa ila bila majari hupati mke na unapangiwa bei juu.
 
Mahari ni heshima kwa tamaduni zetu za kiafrika kuonyesha thamani ya mkeo na kutoa angalau fadhila kwa wazazi wake.Kwa nyie mliokulia 'kwa malkia' hamuwezi elewa.

Aminini nawaambia huwezi kufananisha ndoa iliyofungwa kwa kufuata taratibu zote (kulipa mahari) ,na kubebabeba kusikoeleweka.
Mahari haipo tu Africa, kihistoria ilikuwepo duniani kote, toka enzi za biblia suala la mahari lipo. Mahari siyo ishu ya waafrika.
 
Back
Top Bottom