Hivi maharage ndiyo mboga kuu ya Serikali?

tang'ana

JF-Expert Member
Apr 3, 2015
11,809
15,059
Wakuu,kama kuna anaeelewa anielimishe,kwanini katika kila taasisi inayomilikiwa na Serikali,iwe shule,chuo au hata sherehe yoyote inayoandaliwa na Serikali, basi utakuta mboga kuu na rasmi ni maharage?Huwa najiuliza hivi maharage yalipitishwa lini kuwa mboga kuu ya Serikali?
 
Wakuu,kama kuna anae elewa anielimishe,kwa nin katika kila taasisi inayomilikiwa na serikali,iwe shule,chuo au hata sherehe yoyote inayoandaliwa na serikali, basi utakuta mboga kuu na rasmi ni maharage?huwa najiuliza hivi maharage yalipitishwa lini kuwa mboga kuu ya serikali?
Kwa mashule sawa..mle kuku kwa hela zipi

unataka kusema kukiwa na shughuli/dhifa pale magogoni unalika wali maharage tu.?
 
Haahaa yeye baba. Ndio mboga kuu hiyo kwa Serikali.

Mboga iliyorisishwa tangu enzi za mkoloni mpaka serikali ya jamuhuri ati.
 
Nadhani kuna tatizo na kupewa madaraka kwenye taasisi za serikali. Mtu akiwa hana madaraka anakua na akili timamu. Akishapewa madaraka tu basi ubunifu woote anaurudisha kijijini. Yeye anabaki kichwa wazi. Utakuta anafikiria kuwalisha watu makande au ugali dagaa au ugali maharagwe na uji. Hakuna anayewaza kuwalisha watu nyama ya kuku au chai na mkate au hata maandazi. Wasilokumbuka ni kwamba siku hizi kilo moja unga wa ngano ina bei rahisi by far kuliko kilo ya unga wa mahindi. Hawawezi kujiongeza kutengeneza mini bakery ili watu wale mikate au hata keki siku za jumapili
 
Wakuu,kama kuna anaeelewa anielimishe,kwa nin katika kila taasisi inayomilikiwa na Serikali,iwe shule,chuo au hata sherehe yoyote inayoandaliwa na Serikali, basi utakuta mboga kuu na rasmi ni maharage?Huwa najiuliza hivi maharage yalipitishwa lini kuwa mboga kuu ya Serikali?
Ni mboga ya wanyonge na hii ni serikali yaoo. Akili kichwani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tunayaita BAEDI .....
ngoja nikale wali na Baedi nitarudi
Wakuu,kama kuna anaeelewa anielimishe,kwa nin katika kila taasisi inayomilikiwa na Serikali,iwe shule,chuo au hata sherehe yoyote inayoandaliwa na Serikali, basi utakuta mboga kuu na rasmi ni maharage?Huwa najiuliza hivi maharage yalipitishwa lini kuwa mboga kuu ya Serikali?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
majumbani Mwetu nao hawako nyuma..ni mwendo wa maharage kwa kwenda mbele
 
Nadhani kuna tatizo na kupewa madaraka kwenye taasisi za serikali. Mtu akiwa hana madaraka anakua na akili timamu. Akishapewa madaraka tu basi ubunifu woote anaurudisha kijijini. Yeye anabaki kichwa wazi. Utakuta anafikiria kuwalisha watu makande au ugali dagaa au ugali maharagwe na uji. Hakuna anayewaza kuwalisha watu nyama ya kuku au chai na mkate au hata maandazi. Wasilokumbuka ni kwamba siku hizi kilo moja unga wa ngano ina bei rahisi by far kuliko kilo ya unga wa mahindi. Hawawezi kujiongeza kutengeneza mini bakery ili watu wale mikate au hata keki siku za jumapili
JIBU MASWALI HAYA KWANZA
1.KILO MOJA YA NGANO MPAKA UPATE MKATE AU MANDAZI GHARAMA YAKE IPOJE NA WATAKULA WATU WANGAPI?

2.KILO MOJA YA UNGA WA MAHINDI MPAKA UPATE UGALI GHARAMA YAKE IPOJE NA WATAKULA WATU WANGAPI?
 
Back
Top Bottom