Hivi Mahakama ya Rufaa ilikwisha kumfutia jinai Bw. Aden Rage au la? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Mahakama ya Rufaa ilikwisha kumfutia jinai Bw. Aden Rage au la?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Oct 7, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280
  Kulingana na sheria za uchaguzi aliyefungwa kwa zaidi ya mwaka mmoja hana sifa za kuwa mgombea.

  Bw. Aden rage ambaye hivi sasa anagombea jimbo la Tabora Mjini na ambaye hivi karibuni amekuwa akijifananisha na mmiliki wa klabu ya A.C mIlan ambaye ni Waziri Mkuu wa Italia kutokana na Bw. Rage kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba alikwishafungwa miaka mitatu. Kosa la jinai alilotiwa nalo hatiani ni kwa kumwibia mwajiri wake FAT/TFF alipokuwa ni katibu mtendaji wa chama hicho. Alienda mahakama kuu kupinga adhabu hiyo lakini rufani yake ilitupwa. Alinufaika na msamaha wa raisi Mkapa lakini hilo halimaanishi adhabu ilikuwa imefutwa. Kwa kuelewa hilo alikataa rufani mahakama ya rufaa. Sijawahi kusikia mahakama ya rufaa kama ilikwisha kuisikiliza rufani yake na kumsafisha vinginevyo hana sifa ya kuwa mgombea na sijui NEC walimpitishaje. Au kisingizio chao ni kuwa hakuwekewa pingamizi na mtu yoyote?

  Kama aliwahi kusafishwa nijulisheni. Vinginevyo hata akishinda watakaoshindwa naye wana sababu nzito ya kwenda mahakamani na sheria ikafuata mkondo wake.
   
 2. T

  Tz Asilia Member

  #2
  Oct 7, 2010
  Joined: Oct 30, 2009
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acha unasi wa simba na uyanga
   
 3. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280

  Jibu swali kama hujui si lazima uandike upupu hapa.
   
 4. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Ndio!!
   
 5. M

  Mkulima JF-Expert Member

  #5
  Oct 7, 2010
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 698
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Alishinda rufaa yake na hivyo ni kama hajawahi kufungwa hata kama alitumikia kifungo chake kwa muda mrefu. Ingelikuwa sehemu zingine hata angelipwa mapesa mengi kwa kumtesa jela kimakosa.
   
Loading...