Hivi MAGUFULI ndio nini kuzindua stendi ambayo haina choo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi MAGUFULI ndio nini kuzindua stendi ambayo haina choo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by idawa, Mar 7, 2012.

 1. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #1
  Mar 7, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,537
  Likes Received: 10,458
  Trophy Points: 280
  ni ile ya mbezi mwisho hata kwa kukojoa hamna.napata wasiwasi na umakini wa waziri.!
   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  Mar 7, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu kumbe kituo hakina sehemu ya kujihifadhi pindi wito wa asili ukiwadia? Mbona hatari kama sehemu ambazo kuna vyoo hali huwa si ya kuridhisha kutokana na kutapakaa kwa maji machafu yatokayo miilini, itakuwaje hapo ambapo hata vyoo hakuna?
   
 3. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #3
  Mar 7, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,537
  Likes Received: 10,458
  Trophy Points: 280
  kwa hali ya jiji letu tutarajie nini kama sio kipindupindu
   
 4. Escobar

  Escobar JF-Expert Member

  #4
  Mar 7, 2012
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 576
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 60
  Aaah ndugu yangu mbona mnasahau mapema namna hii? Si majuzi tu tulisikia wajanja wamejenga matundu manne ya choo cha shimo sijui wapi vile kwa shilingi milion kama 700 hivi sasa wewe unataka wajenge choo cha bilion moja halafu akafungue Magufuli unategemea nini kama sio kuharibiana kazi! Wameiliapozi kwanza project ya vyoo ili aje Mzee wa takwimu na makamera yake halafu watamwambia "mzee tumelezimika kuifungua hii stendi haraka haraka ili kuokoa hali mbaya ya stendi iliyokuwepo hivyo choo kitaanza kujengwa wiki ijayo" then baada ya hapo wazee wapige bingo yao tratiiiibu na wakimaliza kujenga choo chao kibovu cha bei kubwa kitafunguliwa na diwani wa eneo husika with no makamera wala nini. Mjini ni raha tupu hasa kama unaakili.
   
 5. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #5
  Mar 7, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Maana yake kila mtu akajisaidie kwao na kama kazidiwa ajisaidie kwenye rambo.
   
 6. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #6
  Mar 7, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,593
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  duh! mwanzisha thread napata wasiwasi na umakini wako wa kufuatilia habari...do ur h/work plz
   
 7. I

  IFRS 9 Senior Member

  #7
  Mar 7, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 168
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwan umeambiwa stand ndo sehemu ya kufutua?
   
 8. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #8
  Mar 8, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,537
  Likes Received: 10,458
  Trophy Points: 280
  mkuu sio swala la kufwatilia ..... Kama kuna vyoo tuambie manake nilikuepo hapo jana tu vyoo hamna....au nimekusoma vibaya.!!
   
 9. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #9
  Mar 8, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,537
  Likes Received: 10,458
  Trophy Points: 280
  kwa hiyo haturuhusiwi kushikwa na haja stendi...au we kwako huna choo kwa hiyo unarahizisha....!
   
 10. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #10
  Mar 8, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,437
  Likes Received: 19,789
  Trophy Points: 280
  sasa wale wajezi walikuwa wanajisaidia wapi? mkandarasi ina maana anakichwa cha panzi? ana design vipi stendi bila kuweka vyoo? siwezi kuamini
   
 11. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #11
  Mar 8, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Kaka walikuwa wanajisaidia kwenye helmet..lol
   
 12. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #12
  Mar 8, 2012
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Nionyeshe choo kilichopo stendi za POSTA,AKIBA,K'KOO,BOMA,MANZESE,SHEKILANGO,SINZA(kwaremi,mori,madukani etc)MAKUMBUSHO,KAWE,PALM BEACH, ETC..... ! LETENI VITU VYA MSINGI VYA KUJADILI.....! INGEKUWA STENDI YA MIKOANI HAPO SAWA!
   
 13. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #13
  Mar 8, 2012
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Ila nakupa hongera maana mtu unapotafuta kosa la kukosoa halafu ukakosa inaonyesha ni jinsi gAni walivyojitahidi!!! Sawa na trafik wetu atakutafutia kosa hata kama gari mpya!!!!
   
 14. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #14
  Mar 8, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Umenikumbusha polisi wa TAznania na njaa zao.
  wanaweza kukutafutia kosa hata ukiwa umelala na mke wako!
   
 15. M

  Makupa JF-Expert Member

  #15
  Mar 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Hivi wale ombaomba wa katikati ya jiji wanatumia vyoo vipi
   
 16. MAGEUZI KWELI

  MAGEUZI KWELI JF-Expert Member

  #16
  Mar 8, 2012
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 1,943
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Kigamboni waliambiwa piga mbizi, na nyie acheni ujinga, Cheueni nyumbani kwenu kabla hamjatoka
   
 17. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #17
  Mar 8, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,537
  Likes Received: 10,458
  Trophy Points: 280
  kwani ile stendi inatofauti gani na stendi ya mkoa ikiwa gari zinapaki kwa muda mrefu kusubiri abiria...mkuu hivi kile ni kituo kidogo kikose choo mbona unahalalisha mapungufu ya mbezi na vituo vidogo tiptop, shek,kagera nk.nawasiwasi kama umewai kusimama hata kidogo kwenye hiyo stendi
   
 18. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #18
  Mar 8, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,898
  Likes Received: 5,360
  Trophy Points: 280
  mkuu ungejua tabu tuliyokuwa tunapata kutokana na foleni sisi wakazi wa huko hata usingesema hivyo,magufuli natofautiana naye kwa mambo kadhaa lakini kwa hili nampa hongera,.for your info,choo kipo kwenye progress kinajengwa,ni busara ya hali ya juu kukizindua kituo hiki maana kilimalizika siku nyingi,tatizo lilikuwa choo,.tabu ya foleni na mtu mmoja au wawili walioshikwa na tumbo la kuharisha,ni bora hao walioshikwa tumbo hapo kituoni wataenda kujisitiri kwenye nyumba ya mtu yyote au baa lakini sio kwenye foleni...mnyika alitishia kuitisha nguvu ya umma kukifungua kile kituo.
   
 19. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #19
  Mar 8, 2012
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu, usiwe na kichwa cha senene!!!! Vituo vilivyo katikati ya route havithitaji kuwa na vyoo ingawaje kwa nchi za wenzetu vituo vy train za umeme kunakuwa na vyoo. Standi ya Mbezi ni stand ya mwanzo wa Route na mwisho wa ruote vile vile kwa hiyo tunatarajia katika mazingira ya kawaida kabisa kituo kile kiwe na vyoo hata kama ni vya kulipia. Jaribu kufikiria abiria apande daladala posta na anakwenda mbezi, na hizo foleni zetu hatumii chini ya masaa mawili kufika, halafu akifika amebanwa na haja kubwa/ndogo akajihifadhi wapi?

  Tukubali tusikubali walio design hiyo stand walichemsha lakini Waziri amechemsha zaidi kwa kuifungua ikiwa katika hali ile!!!!!

  Tiba
   
 20. stephot

  stephot JF-Expert Member

  #20
  Mar 8, 2012
  Joined: Mar 1, 2012
  Messages: 5,023
  Likes Received: 2,645
  Trophy Points: 280
  Kaka wazo lako zuri sana bila choo pale stand ni chaos maana jana kwenye mida ya saa moja jioni nimezunguka nyuma ya basi nikakutana na mama mtu mzima kachuchumaa anajisaidia na amegeukia upande ninaotokea ikabidi nirudi nilikotokea mbio,sasa you can see yourself how bad the situation is!:yawn:
   
Loading...