Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Mie nashindwa kuelewa. Kila siku nasoma na kusikia matatizo lukuki ambayo watu wanapata kuhusiana na suala la vitambulisho vya taifa. Na tatizo limefanywa kubwa zaidi kwa sababu kwa sasa vitambulisho vya taifa vimeunganishwa na utolewaji wa passport, usajiri wa kampuni, kupata TIN nk.
Kuna watu tumekaa zaidi ya miaka miwili tangu tuwakilishe maombi lakini na kuchukuliwa alama za vidole na bado hatujapata vitambulisho. Watu wamepoteza nafasi za maisha kama kusajiri biashara au kwenda nje masomoni kwa ajili tu ya kutokuwa na kitambuisho cha taifa. Watu wa diaspora kila siku wanalia vitambulisho vya taifa.
Sasa huyu Raisi Magufuli na Waziri wake Lugola, wanataka wapigiwe ngoma gani ili wasikie kilio cha Watanzania kuhusu vitambulisho vya taifa? Hivi katika kufikiri kwao wameona hili sio suala muhimu jambo linaleta usumbufu sana kwa kwa Watanzania?
Kwa nini mnaanzisha mambo makubwa bila kujipanga, huo sio uzembe mnaotaka Watanzania tuondokane nao?